Madaraka ni dhamana ya muda mfupi sana, kutoka kupigiwa magoti hadi kusindikizwa nje ya Ikulu

Kama huo ujasiri wao hatuna, narudia tena, hapa kwetu bila Katiba Mpya hatuwezi kuwaondoa CCM, wanetapakaa kila mahali, mpaka kwenye vyombo vya usalama.
Hivi kinachotakiwa ni Katiba mpya au katiba yenye maudhui mazuri? Kenya walidhani katiba mpya ndio suluhisho, baada ya mwaka tu ikaanza kulalamikiwa na kurekebishwa. Sasa wanapambambana na BBI. Hata iwe kubwa kama biblia, Katiba mpya sio suluhisho la kudumu.
 
Ukitaka kujua katiba ya Tz ni nzuri ngoja siku upinzani ushike nchi hautataka kuibadili hata kidogo
Tukubaliane kimsingi, Watanzania ndio tatizo na sio katiba. Vyama vilivyo leta ukombozi katika nchi za Kiafrica ambavyo bado vipo madarakani nadhani havizidi 6, ccm ikiwa ni mojawapo, hivyo vya nchi zingine walau sababu za msingi zipo but not Tanzania. Kwa faida tu ya vijana, vyama hivyo ni Frelimo cha Msumbiji, Angola, Namibia, Africa Kusini na Zimbabwe, the rest of Africa, vyama vyote vilivyopo madarakani sio vilivyo pigania Uhuru. Hizo nchi zingine (ukiondoa Zimbabwe ambayo ni kama kwetu tu ) nchi zao zimekua na matatizo lukuki baada ya Uhuru na zingine zimepata uhuru hata miaka 30 bado, SA na Namibia. So Bongo tusije jilinganisha na nchi zingine, siye tuna matatizo makubwa mno ya kifikra.
 
Usichojua ni kwamba upinzani Zambia wameshinda urais chini ya Tume inayoteuliwa na rais na pia chini Katiba ya zamani.

Hata Kenya, KANU ilipotezwa chini ya Tume iliyoteuliwa na rais.

Hakuna uhusiano Kati ya Katiba mpya, Tume huru na ushindi kwa upinzani kwenye kura
 
Tatizo la TZ siyo tume ya uchaguzi, tatizo la TZ ni wapinzani vigeugeu wasio na mipango endelevu (Ref uchaguzi wa 2015)
 
Viongozi wa Tanzania mjifunze kwa huyu jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…