Pre GE2025 Madaraka Nyerere aeleza maoni ya Mama Maria Nyerere kuhusu Uchaguzi wa CHADEMA, asema uchaguzi umeenda vizuri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Saa100 amejifunza nini kufuatia uchaguzi wa Chadema!!!
 
Attachments

  • 5938169-3f8437b06df44d0a7c8b8e175f481762.mp4
    23 MB
Wakuu

Madaraka Nyerere, mtoto wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ameandika kuhusu mazungumzo aliyofanya na Mama Maria Nyerere (ambaye ni Mama yake) kuhusu mwenendo wa Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA uliomalizika hivi karibuni na Tundu Lissu kuibuka mshindi wa Uenyekiti akimbwaga Freeman Mbowe. Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mitandao ya kijamii, akisema:

Mama Maria: Nashukuru uchaguzi wa CHADEMA umeenda vizuri.
Mimi: Nikiulizwa niseme hayo?
Mama Maria: Hayo ni mawazo yangu binafsi. Subiri uulizwe, siyo unaanza wewe, kama vile mimi mganga wako wa kienyeji."

Soma, Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Madaraka aliendelea kusema kwamba ingawa hakuwa ameulizwa rasmi, aliona ni muhimu kushiriki maoni hayo kwa sababu ni ya manufaa na muhimu kwa wakati huu.
Soma, Pia
- Freeman Mbowe akubali kushindwa, awapongeza Lissu na Heche kwa ushindi
- Ushindi wa Lissu unamaanisha nini kwa Watanzania? Tunapata picha gani Uchaguzi Mkuu 2025? Samia atapumua? Ukabila kuisha?

So bwana madaraka anataka kutupa Ujumbe gani?
 
Yeye Madaraka alitaka akaseme bila kuulizwa?
 
Mama Maria Nyerere yuko vizuri upstairs
Kule Geita aliwashushua CCM kwenye kumbukizi ya Mwalimu ambayo ingestahili kufanyika Mwitongo, alisema "mimi niliona mmenibeba na kunileta hapa mnataka niseme, sijui niseme nini huku!".
 
Uyu mama wa Taifa yuko vizuri pamoja na uzee , kuna mkutano mmoja alifanya mwenda zake pale mwanza ,mama yetu alitaja ,kwamba ameletwa kuongozea vichwa
Tangu siku ile hawataki tena kumuona mjini.
 
Back
Top Bottom