Madarasa ya Rais Samia, Jimbo la Namtumbo

Madarasa ya Rais Samia, Jimbo la Namtumbo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MADARASA YA RAIS SAMIA- JIMBO LA NAMTUMBO

Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya miundombinu ya Elimu yaani madarasa 102.

Wanafunzi Wameripoti Shuleni

Wilaya ya Namtumbo kwa Mwaka 2021/2022 ilipata jumla ya mgao wa Madarasa 102 kwa Shule za Sekondari mbalimbali na baadhi kwa Shule Shikizi. Madarasa hayo yalitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa lengo la kupungua uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye Shule mbalimbali nchini ikiwemo na NAMTUMBO. Sasa madarasa yote yamekamilika na wanafunzi wameanza kuyatumia mwezi Januari 2023 mara baada ya Shule kufunguliwa tarehe 09.

NAMTUMBO TUNASEMA "AHSANTE MAMA ENDELEA KUUPIGA MWINGI"

#KaziIendelee......

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Namtumbo

IMG-20230110-WA0121.jpg

IMG-20230110-WA0122.jpg

IMG-20230110-WA0123.jpg
 
Kiukweli mama anaupiga mwingi! Tumpe moyo tu, japo wanafunzi wa siku hizi ni tatizo lakini kwenye suala la miundombinu serilakali imejitahidi sana
 
UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO - JIMBO LA LONGIDO

MADARASA YA RAIS SAMIA YAMEKUWA MUAROBAINI KWA WANAFUNZI.

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewezesha ujenzi wa Shule, miundombinu ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido.

"Halmashauli ya Wilaya ya longido tulipokea Shilingi za Kitanzania Milioni 380 Kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa 19 Kwa ajili ya upokezi wa wanafunzi wa kidoto cha kwanza. Madarasa yote 19 yamekamilika yakiwa na viti 50 na meza 50 kila moja" - Amesema hayo Dkt. Steven Kiruswa ambaye ni Mbunge wa Longido na Naibu Waziri wa Madini.

Shule zilizopata vyumba vipya vya madarasa ni pamoja na;
✅ Shule ya Sekondari Namanga
✅ Shule ya Sekondari Longido
✅ Shule ya Sekondari Matale
✅ Shule ya Sekondari Engarnaibor
✅ Shule ya Sekondari Lekule

Shukrani zetu za dhati Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pichani ni Mbunge na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt Steven Kiruswa akiangalia vyumba hivyo vya madarasa wakati wa ziara yake Jimboni hapo.

#CCMImetimia
#ChamaImara
#KaziIendelee

index.jpg
indexCVFG.jpg
indexSDER.jpg
indexWER.jpg
 
MADARASA YA RAIS SAMIA- JIMBO LA NAMTUMBO

Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya miundombinu ya Elimu yaani madarasa 102.

Wanafunzi Wameripoti Shuleni

Wilaya ya Namtumbo kwa Mwaka 2021/2022 ilipata jumla ya mgao wa Madarasa 102 kwa Shule za Sekondari mbalimbali na baadhi kwa Shule Shikizi. Madarasa hayo yalitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa lengo la kupungua uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye Shule mbalimbali nchini ikiwemo na NAMTUMBO. Sasa madarasa yote yamekamilika na wanafunzi wameanza kuyatumia mwezi Januari 2023 mara baada ya Shule kufunguliwa tarehe 09.

NAMTUMBO TUNASEMA "AHSANTE MAMA ENDELEA KUUPIGA MWINGI"

#KaziIendelee......

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Namtumbo

View attachment 2477249
View attachment 2477250
View attachment 2477251
Kiukweli Rais Samia Suluhu amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu zamani elimu bure ilikua inatolewa lakini mazingira ya kusomea yalikua hayarizishi lakini sasa elimu bure inatolewa katika mazingira mazuri ya kuomea
 
Back
Top Bottom