uzalendo mwingine utatuua bila sababu, dawa zetu ambazo tunazijua tu kwa majina wala hatujui ndani yake kuna nini si bora kuliko dawa za kigeni tuwe wakweli tu. Mara nyingi ukienda kutibiwa kwa dawa za asili hutoambiwa ni malaria wa typhoid utaambiwa vitu vya ajabu ajabu, kuna uwezekano kua dawa zetu zina vijitiba ndani lakini huaga hatuko certain wakati tunatoa tiba za asili, tunahisi tu kua mtu atapona akichanganya hii na ile. Kuelimika kupitia foreign knowledge sio kua corrupted ndugu yangu. Penye ukweli tuseme ukweli, tusitumie dhana ya uzalendo kupotoshana. Sijawahi kuona case kua kuna mtu kapata matatizo ya afya ya uzazi kwasababu ya kutumia dawa za kienyeji lakini isiwe kigezo cha kusema kua dawa za asili ni bora kuliko za kigeni. Tuseme ukweli hata kama ni wazalendo.
Idadi ya vifo vya kina mama wakati wa uzazi barani Afrika amekua ikipungua na si kuongezeka. Hata hivyo kasi ya kupungua ni ndogo kuliko hali ilivyo kwenye nchi zilizoendelea.Sababu ni kuwa Africa hatujawekeza kiasi cha kutosha kwenye miundombinu, mifumo, watumishi, madawa na vyenzo nyngine za kupambana na hivi vifo. Kwa kifupi ni kuwa mama zetu hasa wa vijijini hawazifikii/hawapati huduma za dharula za uzazi kwa wakati na kiwango/ubora wa kutosha kuokoa maisha yao
haya mzalendo mkweliTasnia ya dawa inahitaji wagonjwa ili iendelee kuwepo, na mashetani wa Ulaya wanalisimamia hili vema sana.
Mimi ni mzalendo na nitasema kweli siku zote!
Nadhani usasa ndio unatuua zaidi kuliko uzalendo. Tangu kuanza kuishi maisha ya kisasa ainabinadamu imeshuhudia kuibuka kwa magonjwa mengi, baadhi yayo yakisababishwa na dawa za spitali ambazo zina salfa, haidrokwinon na kemikali zingine hatari sana.
Dawa zetu hazina vijitiba, ila zina tiba halisi ambazo wewe maamuma huwezi kuzijua kwa sababu SIO mganga na hujawahi hata kukaribia kujua taaluma ya tiba za Kiafrika. Kudai kwako kuwa ukiumwa unaambiwa vitu vya ajabu ajabu ni ubabaishaji tosha. Vitu gani vya ajabu uliambiwa visivyoandikika?
Umedai mwenyewe kuwa hujasikia dawa za kiAfrika zimesababisha matatizo ya afya ya uzazi, kiherehere cha nini sasa? Yapo magonjwa ambayo yanaaminika na hospitali za kisasa kuwa hayatibiki kama vile kansa, sukari na vidonda vya tumbo. Wewe umesikia shuhuda za watu waliopona kwa namna ya matibabu za Kiafrika lakini Serikali kwa kushirikiana na Wahisani wanaotuuzia dawa wanafinya tafiti hizi kwa manufaa yao ya kiuchumi. Tasnia ya dawa inahitaji wagonjwa ili iendelee kuwepo, na mashetani wa Ulaya wanalisimamia hili vema sana.
Mimi ni mzalendo na nitasema kweli siku zote!
Hii porojo ya kuwa zinafanyiwa utafiti na zinatokana na mimea imekuwa ikitumika muda mrefu kunadi mfumo wa kisasa wa tiba za viwandani, ambazo ni biashara zaidi kuliko tiba na mbaya ni kuwa zinatokana na kemikali kwa kiasi kikubwa na zina madhara mengi ya ziada kwa watumiaji.
Mimi si mtafiti, lakini takwimu chache zinaonesha kuwa kiwango cha vifo vya uzazi kimeongezeka huku Afrika kweusi baada ya kununua propaganda za biashara ya tiba kutoka kwa Wazungu, miaka inavyoenda pia, licha ya kukua kwa teknolojia ya madawa na vifaa tiba bado kiwango cha maisha kinapungua kwa kiasi kikubwa sana, kwanini?
Mataifa kama China na Japan, Serikali zao zimewekeza kwenye tiba za asili kwa teknolojia ya kisasa na nadhani ndizo nchi zenye watu wanaoishi muda mrefu.
Sisi tunacho kitengo cha tiba asili pale Muhimbili, lakini kinadumazwa kwa makusudi ili biashara ya madawa ya viwanda vya nchi za mabepari izidi kusitawi (na tuendelee kufa). Wewe ni shuhuda, kwa umri wako huu umeshuhudia tiba elekezi ya Malaria ikibadilika kila baada ya miaka kadhaa kwa sababu tofauti, unadhani ni kwanini?
Unadhani hawajui kuwa aloe vera, mbegu za jamii ya machungwa, mbegu za papai, shubiri, muarobaini na mimea lukuki inatibu Maleria kwa ufanisi wa asilimia mia na bila kuacha madhara mengine?
Ni vigumu na inataka akili ngumu kuwaamini watu wale wale waliodhamiria kukuua kwa madawa na sumu waje wakupe tiba sahihi. Teh!
#RevolutionWillNotBeTelevised
Hii porojo ya kuwa zinafanyiwa utafiti na zinatokana na mimea imekuwa ikitumika muda mrefu kunadi mfumo wa kisasa wa tiba za viwandani, ambazo ni biashara zaidi kuliko tiba na mbaya ni kuwa zinatokana na kemikali kwa kiasi kikubwa na zina madhara mengi ya ziada kwa watumiaji.
Mimi si mtafiti, lakini takwimu chache zinaonesha kuwa kiwango cha vifo vya uzazi kimeongezeka huku Afrika kweusi baada ya kununua propaganda za biashara ya tiba kutoka kwa Wazungu, miaka inavyoenda pia, licha ya kukua kwa teknolojia ya madawa na vifaa tiba bado kiwango cha maisha kinapungua kwa kiasi kikubwa sana, kwanini?
Mataifa kama China na Japan, Serikali zao zimewekeza kwenye tiba za asili kwa teknolojia ya kisasa na nadhani ndizo nchi zenye watu wanaoishi muda mrefu.
Sisi tunacho kitengo cha tiba asili pale Muhimbili, lakini kinadumazwa kwa makusudi ili biashara ya madawa ya viwanda vya nchi za mabepari izidi kusitawi (na tuendelee kufa). Wewe ni shuhuda, kwa umri wako huu umeshuhudia tiba elekezi ya Malaria ikibadilika kila baada ya miaka kadhaa kwa sababu tofauti, unadhani ni kwanini?
Unadhani hawajui kuwa aloe vera, mbegu za jamii ya machungwa, mbegu za papai, shubiri, muarobaini na mimea lukuki inatibu Maleria kwa ufanisi wa asilimia mia na bila kuacha madhara mengine?
Ni vigumu na inataka akili ngumu kuwaamini watu wale wale waliodhamiria kukuua kwa madawa na sumu waje wakupe tiba sahihi. Teh!
#RevolutionWillNotBeTelevised
uzalendo mwingine utatuua bila sababu, dawa zetu ambazo tunazijua tu kwa majina wala hatujui ndani yake kuna nini si bora kuliko dawa za kigeni tuwe wakweli tu. Mara nyingi ukienda kutibiwa kwa dawa za asili hutoambiwa ni malaria wa typhoid utaambiwa vitu vya ajabu ajabu, kuna uwezekano kua dawa zetu zina vijitiba ndani lakini huaga hatuko certain wakati tunatoa tiba za asili, tunahisi tu kua mtu atapona akichanganya hii na ile. Kuelimika kupitia foreign knowledge sio kua corrupted ndugu yangu. Penye ukweli tuseme ukweli, tusitumie dhana ya uzalendo kupotoshana. Sijawahi kuona case kua kuna mtu kapata matatizo ya afya ya uzazi kwasababu ya kutumia dawa za kienyeji lakini isiwe kigezo cha kusema kua dawa za asili ni bora kuliko za kigeni. Tuseme ukweli hata kama ni wazalendo.
jamani dawa za asili pia inategemea mfano mimi mimba ya kwanza nilipewa ninawe huku ukeni kwa mda wa mwezi mmoja mara mbili kwa siku nisizidishe na yule mama aliniambia dawa ile itanisaida sana ht kujifungua sitokaa sana hosp.
nakumbuka saa sita mchana nilitapika nikaanza kujiskia vbaya kiuno kilivyoanza kuuma kilikua kinauma kawaida sana saa moja napelekwa temeke yaani km siendi kujifungua vile nimefika napiga stori mda wa saa tatu kasoro uchungu ukanishika na nkavunja chupa na kujifungua mda huohuo sikuchelewa wenzangu nliwakuta nikawaacha
Habari Great Thinkers,
Katika shughuli zangu kama mtaalam nimekutana sana na suala la matumizi ya madawa ya kienyeji hususan wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua. Pamoja na heshima kubwa kwa tiba zetu asili, naomba tujadili kwa uwazi ili tujue faida na hasara za matumizi haya. Niko tayari kuanza mjadala. Karibuni wanajamvi!
Kwanza dawa za kienyeji si ramli...ni miti shamba...
Ukitoa swala la kutokuwa na dozi kamili mimi naziamini sana...
Na nadhani hazina madhara sababu hazina nguvu (concentration) kama dawa za viwandani...ni organic...
Haya tuje kwenye ushuhuda...
Mimi kama mwanamke wa kutoka BK nimetumia sana dawa za kienyeji nikiwa na mimba...kiroho saafi...
Na clinic nikiwa naenda...
Si kwa kuwa nilikuwa na tatizo..
Mama alinambia ni preventive measures...
Na ndio maana wahaya na wengine wa BK wengi si wasumbufu wakitaka kujifungua kama makabila mengine wanao shauti mpaka wodi aikaliki...
Hizi dawa mama alinambia zinasaidia vitu kama vifafa vya uzazi...
Ni very rare kukuta binti wa kihaya amepata kifafa cha uzazi...na akipata basi utaambiwa alikataa kunywa hizi dawa...
Kwa hiyo hata mimi nashauri wale wenye access na hizi dawa watumie...na mara nyingi wala haziuzwi...ni wamama wanarithishana ujuzi...kuwa ni majani haya na haya...na wengi uyapanda kama maua...
Ila siwezi tumia dawa ya kutoka mkoa mwingine...I only trust my mum...na ndugu wengine...dawa za kihaya tu ndio nazotumia...si za kimasai wala ki nini...
Ni hayo tuuu