Madawa ya kienyeji yana athari yoyote katika afya ya uzazi?

Madawa ya kienyeji yana athari yoyote katika afya ya uzazi?

Mkuu nafikiri ni kosa kuweka fungu moja dawa zote za kienyeji. Maana yangu ni kuwa kuna dawa za asili ambazo kwa kweli zinasaidia sana. Ila tatizo nafikiri ni kutokana na maendeleo na utapeli (kikombe cha babu) mila hii haipiti kwa karne inayofuatia kwa uhakika. Mfano: bibi yangu pale Peramiho alikuwa anajua ni majani gani yakitwangwa na kutengenezewa chai, yanafunga uharisho within 15 min. Jani hilo hilo ukilipata Kibamba ndio linakuongezea mkato wa tumbo.
 
uzalendo mwingine utatuua bila sababu, dawa zetu ambazo tunazijua tu kwa majina wala hatujui ndani yake kuna nini si bora kuliko dawa za kigeni tuwe wakweli tu. Mara nyingi ukienda kutibiwa kwa dawa za asili hutoambiwa ni malaria wa typhoid utaambiwa vitu vya ajabu ajabu, kuna uwezekano kua dawa zetu zina vijitiba ndani lakini huaga hatuko certain wakati tunatoa tiba za asili, tunahisi tu kua mtu atapona akichanganya hii na ile. Kuelimika kupitia foreign knowledge sio kua corrupted ndugu yangu. Penye ukweli tuseme ukweli, tusitumie dhana ya uzalendo kupotoshana. Sijawahi kuona case kua kuna mtu kapata matatizo ya afya ya uzazi kwasababu ya kutumia dawa za kienyeji lakini isiwe kigezo cha kusema kua dawa za asili ni bora kuliko za kigeni. Tuseme ukweli hata kama ni wazalendo.

Nadhani usasa ndio unatuua zaidi kuliko uzalendo. Tangu kuanza kuishi maisha ya kisasa ainabinadamu imeshuhudia kuibuka kwa magonjwa mengi, baadhi yayo yakisababishwa na dawa za spitali ambazo zina salfa, haidrokwinon na kemikali zingine hatari sana.

Dawa zetu hazina vijitiba, ila zina tiba halisi ambazo wewe maamuma huwezi kuzijua kwa sababu SIO mganga na hujawahi hata kukaribia kujua taaluma ya tiba za Kiafrika. Kudai kwako kuwa ukiumwa unaambiwa vitu vya ajabu ajabu ni ubabaishaji tosha. Vitu gani vya ajabu uliambiwa visivyoandikika?

Umedai mwenyewe kuwa hujasikia dawa za kiAfrika zimesababisha matatizo ya afya ya uzazi, kiherehere cha nini sasa? Yapo magonjwa ambayo yanaaminika na hospitali za kisasa kuwa hayatibiki kama vile kansa, sukari na vidonda vya tumbo. Wewe umesikia shuhuda za watu waliopona kwa namna ya matibabu za Kiafrika lakini Serikali kwa kushirikiana na Wahisani wanaotuuzia dawa wanafinya tafiti hizi kwa manufaa yao ya kiuchumi. Tasnia ya dawa inahitaji wagonjwa ili iendelee kuwepo, na mashetani wa Ulaya wanalisimamia hili vema sana.
Mimi ni mzalendo na nitasema kweli siku zote!
 
Idadi ya vifo vya kina mama wakati wa uzazi barani Afrika amekua ikipungua na si kuongezeka. Hata hivyo kasi ya kupungua ni ndogo kuliko hali ilivyo kwenye nchi zilizoendelea.Sababu ni kuwa Africa hatujawekeza kiasi cha kutosha kwenye miundombinu, mifumo, watumishi, madawa na vyenzo nyngine za kupambana na hivi vifo. Kwa kifupi ni kuwa mama zetu hasa wa vijijini hawazifikii/hawapati huduma za dharula za uzazi kwa wakati na kiwango/ubora wa kutosha kuokoa maisha yao

Vifo vimeongezeka kwa kuwa watu wametolewa kutoka katika namna salama ya tiba na kuingizwa katika mfumo-sumu wa Kimagharibi walioutengeneza kwa manufaa yao.

Miaka 100 nyuma kusingekuwa na tatizo kwa mama kujifungua nyumbani hapa Afrika, lakini nyie wahuni kwa kushirikiana na Serikali na makampuni ya madawa yaliyowatuma mmefanikisha kampeni ya kuzika tiba zetu kisha kudai kuwa idadi ya vifo vya uzazi ni kubwa kuliko nchi walikoendelea.
 
Nadhani kama tatizo ni vipimo na mengineyo, yanaweza kufanyiwa lakini bila kubadilisha hali yake halisi, japo sijawahi kuyatumia wapo wengi wanaozisifu na ipo siku ningependa pia nibadilishe, dawa za hospitali pia zina madhara na nyingine ya muda mrefu sana na nyingine zinaleta madhara ya kudumu. Humjawahi kwenda hospitali ukaulizwa kuna dawa hutumii?
 
Phamakolojia ya dawa miti inajulikana sana zikitumiwa kwa usahihi zinaweza kufunga viwanda vyote vya drugs za kutibu.dawa hizi zina uwezo wa kutibu katika namna ambayo wanasayansi hawawezi kufafanua na madhara yake ni kidogo sana zikilinganishwa na drugs
 
Nadhani usasa ndio unatuua zaidi kuliko uzalendo. Tangu kuanza kuishi maisha ya kisasa ainabinadamu imeshuhudia kuibuka kwa magonjwa mengi, baadhi yayo yakisababishwa na dawa za spitali ambazo zina salfa, haidrokwinon na kemikali zingine hatari sana.

Dawa zetu hazina vijitiba, ila zina tiba halisi ambazo wewe maamuma huwezi kuzijua kwa sababu SIO mganga na hujawahi hata kukaribia kujua taaluma ya tiba za Kiafrika. Kudai kwako kuwa ukiumwa unaambiwa vitu vya ajabu ajabu ni ubabaishaji tosha. Vitu gani vya ajabu uliambiwa visivyoandikika?

Umedai mwenyewe kuwa hujasikia dawa za kiAfrika zimesababisha matatizo ya afya ya uzazi, kiherehere cha nini sasa? Yapo magonjwa ambayo yanaaminika na hospitali za kisasa kuwa hayatibiki kama vile kansa, sukari na vidonda vya tumbo. Wewe umesikia shuhuda za watu waliopona kwa namna ya matibabu za Kiafrika lakini Serikali kwa kushirikiana na Wahisani wanaotuuzia dawa wanafinya tafiti hizi kwa manufaa yao ya kiuchumi. Tasnia ya dawa inahitaji wagonjwa ili iendelee kuwepo, na mashetani wa Ulaya wanalisimamia hili vema sana.
Mimi ni mzalendo na nitasema kweli siku zote!

Mheshiwa Mphamvu,

Bado naona kama tunachanganya mambo.....nadhani kwa mawazo yangu... ni vigumu sana kutoa tiba kama haujui hasa tatizo ni nini.....kutoa dawa ni sehemu ya mwisho kabisa ya matibabu baada ya kujua ugonjwa/tatizo lenyewe. Kwa mfano kuumwa kwa tumbo hakusababishwi na jambo moja tu.... ni dalili ya matatizo mengi sana....inawezekana ni kwenye tumbo(mfuko wa chakula), utumbo, kidole tumbo, ngiri n.k.......na ikiwa ni kwa mama mzazi mtarajiwa ndiyo hali mbaya zaidi....

Katika tiba kuna njia mbili za kubaini ugonjwa/tatizo

.....njia ya kwanza ni kumuangalia mgonjwa viungo vyake kwa nje, kiasi cha joto alichonacho na hata mwenyewe kujieleza vile anajihisi.... mara nyingi tiba inayotolewa kutokana na matokeo ya njia hii hutumia uzoefu tu....na huwa ni ya kubahatisha kwani maradhi mengi ya ndani huwa na dalili tofauti tofauti za nje kutokana na mtu na mtu au hata kwa jamii moja na nyingine.

....Njia ya pili ni kumpima mgonjwa kwa kutumia vifaa vya kisasa....kuangalia damu, kutumia mawimbi/miale/mionzi kuangalia viungo vya ndani nk....mara nyingi tiba inayotolewa kwa njia hii ni ya uhakika zaidi kwani dawa inayotolewa huwa ni maalum kwa ugonjwa/tatizo lililoonekana.

....Pamoja na yote hayo.....lakini tatizo kubwa katika jamii yetu hasa nchi zinazoendela ni ukosefu wa vifaa pamoja na utaalam katika kubaini matatizo/magonjwa na hivyo kupelekea kupatiwa tiba ya dawa za kisasa/viwandani ambazo ni rahisi kupatikana kwa magonjwa yasiostahili kwani dawa hizo hutengenezwa kwa magonjwa maalum.....na madhara yake ni kutotibu tatizo lililodhamiriwa na pengine kuleta madhara mengine kwa mtumiaji.... . na hapa ndipo tunapokuja na mawazo ya kuwa dawa za kisasa zina hazitibu na zina madhara mengi.

Lakini pia...kwa dawa za asili/jadi...pamoja ya kutolewa kwa kubahatisha kwani utafutaji wa tatizo huwa ni wa kubahatisha...kwa sababu uzoefu hutumika zaidi....na hata vipimo vya utolewaji wake havina uhakika....haviangalii uzito wa mtumiaji wala kiwango cha tatizo/ugonjwa alionao...Labda kwa sababu dawa hutolewa zikiwa na mchanganyiko wa vitu vingi katika kiasi kidogo ndiyo maana hatuwezi kuona madhara yake katika muda mfupi...Kwa uzoefu wangu hadi mgonjwa apate kutibiwa kwa dawa za asili/jadi huwa ametumia aina nyingi sana za dawa....vilevile kitaalamu kiwango cha kemikali cha majani ya mpapai ulioota kando mto hayatalingana na majani ya mpapai uliiota kando ya zizi la ngombe... na bado hatujui madhara yatakayo tokea kwa mtumia akiwa mjamzito, ananyonyesha au hata kama ana magonjwa ya kudumu..kifafa,pumu nk.

Kuhusu kemikali kama za sulphur ambazo umezitaja kama hatari kwa maisha ya binadamu..... bado sijajua tukisema hatari tuna maana gani....majani ya muarubaini yanayotibu magonjwa zaidi ya 200 kama yakinywewa kwa wingi na mama mtarajiwa basi kuna uwezekano wa kuharibika kwa tumbo lake au kujifungua mtoto aliye mfu. Vilevile....majani machanga ya mti ulaya ambayo husaidia kuondoa kikohozi maji yake huweza pia kusababisha vidonda vya tumbo....pia hiyo kemikali ya sulphur ambayo umeitaja kama ni hatari kwa mwanadam hupatikana kwa wingi kwenye majani ya mmea pamoja na mbegu.... kazi kubwa ya sulphur ni kuweka kiasi cha maji kinachowiana katika mimea.... pia hujenga aina nyingi za protini, vitamini na husaidia katika vichocheo......nashindwa kuelewa

Nadhani.....kitu cha msingi hapa ni kuwaweka pamoja wataalam wetu wa dawa asili/jadi na dawa za kisasa kwa kutumia vifaa vya kisasa waweze kufanya kazi pamoja......ilituweze kutengeneza madawa yetu wenyewe......kwa magonjwa yetu wenyewe na kwa mazingira yetu wenyewe.....ni mawazo yangu tu
 
Kwanza dawa za kienyeji si ramli...ni miti shamba...
Ukitoa swala la kutokuwa na dozi kamili mimi naziamini sana...
Na nadhani hazina madhara sababu hazina nguvu (concentration) kama dawa za viwandani...ni organic...

Haya tuje kwenye ushuhuda...

Mimi kama mwanamke wa kutoka BK nimetumia sana dawa za kienyeji nikiwa na mimba...kiroho saafi...
Na clinic nikiwa naenda...
Si kwa kuwa nilikuwa na tatizo..
Mama alinambia ni preventive measures...

Na ndio maana wahaya na wengine wa BK wengi si wasumbufu wakitaka kujifungua kama makabila mengine wanao shauti mpaka wodi aikaliki...

Hizi dawa mama alinambia zinasaidia vitu kama vifafa vya uzazi...
Ni very rare kukuta binti wa kihaya amepata kifafa cha uzazi...na akipata basi utaambiwa alikataa kunywa hizi dawa...

Kwa hiyo hata mimi nashauri wale wenye access na hizi dawa watumie...na mara nyingi wala haziuzwi...ni wamama wanarithishana ujuzi...kuwa ni majani haya na haya...na wengi uyapanda kama maua...

Ila siwezi tumia dawa ya kutoka mkoa mwingine...I only trust my mum...na ndugu wengine...dawa za kihaya tu ndio nazotumia...si za kimasai wala ki nini...

Ni hayo tuuu
 
Dawa za viwandani ni sumu...
Ndio maana nyingi wanaandika side effects...
Ila ndio hivyo doctor anaangalia cost na benefits kabla ya kuamua kukupa dawa...

Huwa nasoma articles za afya...ni shiiida...
Unajua pharmaceutical industry ni moja kati ya industry kubwa duniani..na dawa ni biashara zaidi ya utu...
Unaambiwa hadi madaktari wengine wanapewa chochote ili ku prescribe aina fulani ya dawa wakati mwingine unnecessarily...acha kabisa...

Na wakiwa wana prescribe ulishawasikia wanakwambia madhara? they don't tell the truth...the whole truth...nothing else but the truth...
Labda uwe mjanja (kama miye) uanze ku google..na huko google kwenyewe utapewa ukweli nusu...ambao ni wa lazima ili kiwanda kisishitakiwe...

Hii porojo ya kuwa zinafanyiwa utafiti na zinatokana na mimea imekuwa ikitumika muda mrefu kunadi mfumo wa kisasa wa tiba za viwandani, ambazo ni biashara zaidi kuliko tiba na mbaya ni kuwa zinatokana na kemikali kwa kiasi kikubwa na zina madhara mengi ya ziada kwa watumiaji.

Mimi si mtafiti, lakini takwimu chache zinaonesha kuwa kiwango cha vifo vya uzazi kimeongezeka huku Afrika kweusi baada ya kununua propaganda za biashara ya tiba kutoka kwa Wazungu, miaka inavyoenda pia, licha ya kukua kwa teknolojia ya madawa na vifaa tiba bado kiwango cha maisha kinapungua kwa kiasi kikubwa sana, kwanini?

Mataifa kama China na Japan, Serikali zao zimewekeza kwenye tiba za asili kwa teknolojia ya kisasa na nadhani ndizo nchi zenye watu wanaoishi muda mrefu.

Sisi tunacho kitengo cha tiba asili pale Muhimbili, lakini kinadumazwa kwa makusudi ili biashara ya madawa ya viwanda vya nchi za mabepari izidi kusitawi (na tuendelee kufa). Wewe ni shuhuda, kwa umri wako huu umeshuhudia tiba elekezi ya Malaria ikibadilika kila baada ya miaka kadhaa kwa sababu tofauti, unadhani ni kwanini?

Unadhani hawajui kuwa aloe vera, mbegu za jamii ya machungwa, mbegu za papai, shubiri, muarobaini na mimea lukuki inatibu Maleria kwa ufanisi wa asilimia mia na bila kuacha madhara mengine?

Ni vigumu na inataka akili ngumu kuwaamini watu wale wale waliodhamiria kukuua kwa madawa na sumu waje wakupe tiba sahihi. Teh!

#RevolutionWillNotBeTelevised
 
Mimea inayotumika kutibu magonjwa kwa ujumla ni ile inayojulikana kwamba ni mimea salama kwa miaka mingi.tofauti kubwa kati ya dawa za asili na za kizungu ni kwamba dawa za asili zina viasili vya asili ambavyo hutumika pamoja katika kutibu bila kuvitenganisha kutoka asili yake mfano mti, na hili ndilo linafanya dawa za asili ziwe na usalama mkubwa kuliko za kizungu kwa upande mwingine dawa za kizungu zina viasili ambavyo vimetengwa kutoka kwenye viasili vingine vya asili na hii ndiyo hufanya dawa za kizungu ziwe ni hatari kupita maelezo.

Mfano majani yaitwayo madagascar periwinkle au marufu kama star of jerusalem au mkaburi kwa hapa bongo yanatumika kutengeneza dawa za kutbu kansa za kizungu baada ya kuchuja viasili viwili tu-vincrastine na vincanine miongoni mwa viasili zaidi ya 100 vinavyopatikana katika mmea huo.mmea huu umetumika kutibu magonjwa mbalimbali huko madagascar bila madhara makubwa kama ilivyo kwa dawa hizi za kizungu zinazotokana na mmea huu.

Kibaya zaidi hawa wazunga huenda mbali zaidi baada ya kugundua mmea fulani una viasili vyenye uwezo wa kutibu hujifunza kemia ya viasili hivyo na kutengeneza viasili bandia-synthetic copies of pytochemicals-na hapa ndio balaa duniani.side effects za dawa moja unaandika kitabu cha kurasa ishirini.hii yote ni tamaa ya haya makampuni kuvuna mapesa.wanadhamini tafiti za kukatisha tamaa matumizi ya mimea ambayo imetibu miaka nenda rudi badala ya kutafiti kwamba dawa zao zimeua wangapi.jiulize kwa nini zinabadilishwa kila kunapokucha.tuko ktk vita vya kibailojia.soundhealth ubungo riverside wanakuomba urejee asili 0716 60 9916 au 0759 67 15 43
 
Hii porojo ya kuwa zinafanyiwa utafiti na zinatokana na mimea imekuwa ikitumika muda mrefu kunadi mfumo wa kisasa wa tiba za viwandani, ambazo ni biashara zaidi kuliko tiba na mbaya ni kuwa zinatokana na kemikali kwa kiasi kikubwa na zina madhara mengi ya ziada kwa watumiaji.

Mimi si mtafiti, lakini takwimu chache zinaonesha kuwa kiwango cha vifo vya uzazi kimeongezeka huku Afrika kweusi baada ya kununua propaganda za biashara ya tiba kutoka kwa Wazungu, miaka inavyoenda pia, licha ya kukua kwa teknolojia ya madawa na vifaa tiba bado kiwango cha maisha kinapungua kwa kiasi kikubwa sana, kwanini?

Mataifa kama China na Japan, Serikali zao zimewekeza kwenye tiba za asili kwa teknolojia ya kisasa na nadhani ndizo nchi zenye watu wanaoishi muda mrefu.

Sisi tunacho kitengo cha tiba asili pale Muhimbili, lakini kinadumazwa kwa makusudi ili biashara ya madawa ya viwanda vya nchi za mabepari izidi kusitawi (na tuendelee kufa). Wewe ni shuhuda, kwa umri wako huu umeshuhudia tiba elekezi ya Malaria ikibadilika kila baada ya miaka kadhaa kwa sababu tofauti, unadhani ni kwanini?

Unadhani hawajui kuwa aloe vera, mbegu za jamii ya machungwa, mbegu za papai, shubiri, muarobaini na mimea lukuki inatibu Maleria kwa ufanisi wa asilimia mia na bila kuacha madhara mengine?

Ni vigumu na inataka akili ngumu kuwaamini watu wale wale waliodhamiria kukuua kwa madawa na sumu waje wakupe tiba sahihi. Teh!

#RevolutionWillNotBeTelevised

safi sana mkuu, yani natamani ningekua na kitabu kinachoelezea dawa zote za asili na matumiz yake
 
Si kweli kuwa dawa za asilia hazina kemikali.
Kilichomo na kinachotibu ndani ya dawa hizo ni kemikali. Kemikali zote, ziwe za viwandani au za kwenye miti zinaweza kuwa na madhara iwapo utapata dozi fulani.

Baadhi ya mitishamba ina sumu kali kabisa na ilikuwa ikitumika kama sumu za kuulia adui kwenye vita, na kwenye mambo ya kichawi/kishirikina. Baadhi ya mitishamba kama muarobaini, arthemisia na mingineyo, inatoa dawa za kutibu watu na kuua wadudu. Quinine, dawa ya malaria ya kisasa inapatikana kutoka kwenye mtishamba, mti inaitwa Cinchona. Ukinywa sana mtishamba huo utapta tu madhara sawa na aliyeji-overdose Quinine ya dukani kwa mangi.

Moja ya sababu ya wengi wetu kujua kuwa dawa za kisasa zina madhara ni kwa sababu ya uwazi wa tafiti zinazohusiana na dawa hizo. Na wengi wetu tunafikiri dawa za asili hazina madhara kwa sababu tu hazijafanyika tafiti za kutosha na kuna usiri mwingi unaombatana na dawa hizo.
 
jamani dawa za asili pia inategemea mfano mimi mimba ya kwanza nilipewa ninawe huku ukeni kwa mda wa mwezi mmoja mara mbili kwa siku nisizidishe na yule mama aliniambia dawa ile itanisaida sana ht kujifungua sitokaa sana hosp.
nakumbuka saa sita mchana nilitapika nikaanza kujiskia vbaya kiuno kilivyoanza kuuma kilikua kinauma kawaida sana saa moja napelekwa temeke yaani km siendi kujifungua vile nimefika napiga stori mda wa saa tatu kasoro uchungu ukanishika na nkavunja chupa na kujifungua mda huohuo sikuchelewa wenzangu nliwakuta nikawaacha
 
uzalendo mwingine utatuua bila sababu, dawa zetu ambazo tunazijua tu kwa majina wala hatujui ndani yake kuna nini si bora kuliko dawa za kigeni tuwe wakweli tu. Mara nyingi ukienda kutibiwa kwa dawa za asili hutoambiwa ni malaria wa typhoid utaambiwa vitu vya ajabu ajabu, kuna uwezekano kua dawa zetu zina vijitiba ndani lakini huaga hatuko certain wakati tunatoa tiba za asili, tunahisi tu kua mtu atapona akichanganya hii na ile. Kuelimika kupitia foreign knowledge sio kua corrupted ndugu yangu. Penye ukweli tuseme ukweli, tusitumie dhana ya uzalendo kupotoshana. Sijawahi kuona case kua kuna mtu kapata matatizo ya afya ya uzazi kwasababu ya kutumia dawa za kienyeji lakini isiwe kigezo cha kusema kua dawa za asili ni bora kuliko za kigeni. Tuseme ukweli hata kama ni wazalendo.

mkuu hapo kuna zenye madhara na nzuri..... mfano si vyema kunywa dawa za ķuongeza uchungu wakat wa kujifungua ni hatari zaid.....
 
jamani dawa za asili pia inategemea mfano mimi mimba ya kwanza nilipewa ninawe huku ukeni kwa mda wa mwezi mmoja mara mbili kwa siku nisizidishe na yule mama aliniambia dawa ile itanisaida sana ht kujifungua sitokaa sana hosp.
nakumbuka saa sita mchana nilitapika nikaanza kujiskia vbaya kiuno kilivyoanza kuuma kilikua kinauma kawaida sana saa moja napelekwa temeke yaani km siendi kujifungua vile nimefika napiga stori mda wa saa tatu kasoro uchungu ukanishika na nkavunja chupa na kujifungua mda huohuo sikuchelewa wenzangu nliwakuta nikawaacha

hiuo nakubaliana na ww lkn hapo inategemea .....kama muda haujafika kuna hatar ya kufa coz inalazmisha chupa kupasuka kabla ya wakat
 
Habari Great Thinkers,

Katika shughuli zangu kama mtaalam nimekutana sana na suala la matumizi ya madawa ya kienyeji hususan wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua. Pamoja na heshima kubwa kwa tiba zetu asili, naomba tujadili kwa uwazi ili tujue faida na hasara za matumizi haya. Niko tayari kuanza mjadala. Karibuni wanajamvi!

HrEt haNdsssaulizA
 
Kwanza dawa za kienyeji si ramli...ni miti shamba...
Ukitoa swala la kutokuwa na dozi kamili mimi naziamini sana...
Na nadhani hazina madhara sababu hazina nguvu (concentration) kama dawa za viwandani...ni organic...

Haya tuje kwenye ushuhuda...

Mimi kama mwanamke wa kutoka BK nimetumia sana dawa za kienyeji nikiwa na mimba...kiroho saafi...
Na clinic nikiwa naenda...
Si kwa kuwa nilikuwa na tatizo..
Mama alinambia ni preventive measures...

Na ndio maana wahaya na wengine wa BK wengi si wasumbufu wakitaka kujifungua kama makabila mengine wanao shauti mpaka wodi aikaliki...

Hizi dawa mama alinambia zinasaidia vitu kama vifafa vya uzazi...
Ni very rare kukuta binti wa kihaya amepata kifafa cha uzazi...na akipata basi utaambiwa alikataa kunywa hizi dawa...

Kwa hiyo hata mimi nashauri wale wenye access na hizi dawa watumie...na mara nyingi wala haziuzwi...ni wamama wanarithishana ujuzi...kuwa ni majani haya na haya...na wengi uyapanda kama maua...

Ila siwezi tumia dawa ya kutoka mkoa mwingine...I only trust my mum...na ndugu wengine...dawa za kihaya tu ndio nazotumia...si za kimasai wala ki nini...

Ni hayo tuuu

na huu ndo ukweli kunywa dawa unazopewa na unaowaamini tu usikurupuke hovyohovyo
 
ukitaka kuelewa madhara ya mambo ya kizungu katika afya ya uzazi chunguza process wanazokupa wanapogundua una tatizo la uzazi ila ukirejea katika uasilia wetu ni kitu rahisi na gharama nafuu kama una tatizo la uzazi wasiliana nami kwa 0755155782 nikuonyeshe nguvu ya dawa za asili pasi na madhara yoyote
 
Kwa kiasi kiku bwa madawa ya kienyeji(local medicines) yanamchango mkubwa kwa wamama wajawazito kwani mama mjamzito anapofikisha miezi kadhaa karibia na kujifungua husumbuliwa na matatizm mbali mbali ambayo hata hukitumia modern medicines hakuna matunda yeyote yanayo patikana.
 
Back
Top Bottom