Madawa ya kienyeji yana athari yoyote katika afya ya uzazi?

Madawa ya kienyeji yana athari yoyote katika afya ya uzazi?

WLF Tanzania

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
38
Reaction score
22
Habari Great Thinkers,

Katika shughuli zangu kama mtaalam nimekutana sana na suala la matumizi ya madawa ya kienyeji hususan wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua. Pamoja na heshima kubwa kwa tiba zetu asili, naomba tujadili kwa uwazi ili tujue faida na hasara za matumizi haya. Niko tayari kuanza mjadala. Karibuni wanajamvi!
 
sometimes dawa za kienyeji kwa watu wanaoamini taboos zao wanahs zinasaidia but for what i know local medicines during pregnacy inaleta effect nying sana kwa mfano ,,can lead to maternal or child death due to overdosage,,,congestive cardiac failure eg some drugs certain digitali which may lead to cardiac failure,,,,liver failure due to intoxication coz dawa za kienyeji hazina dose maalum,,,,severe vaginal bleeding from uterus in child birth,,,Rupture of uterus some drugs cause very strong contraction but there maybe obstructed labour,,, then inaweza sababisha severe indfections,,,Thanks..
 
mimi ni mtoto wa mganga wa kienyeji na ninafahamu ni jinsi gani mama yangu alivyokuwa akiwasaidia wenye kutaka ujauzito au kujifungua.kwa wadada ambao walikuwa wanahitaji ujauzito walikuwa wakiambiwa waje na mbuzi mweupe jike.basi alikuwa akiletwa basi tulikuwa tunamlisha dawa kabla ya kumchinja na baadae tukisha mpa dawa tunamchukua na kwenda kumchinja.

Baada ya kumchinja kulikuwa na utaratibu maalumu wa kuchuna ngozi yake na baada ya kumchuna tulikuwa tukimpasua kwa utaratibu maalumu.tukianza kumpasua tulikuwa tunamkata vizuri na kutoa kiungo kimoja kimoja. Baada ya kumaliza kumkataka sehemu ya kiuno na via vya uzazi vilikuwa vinapelekwa kwa mgonjwa na anaonyeshwa kipi kimesababisha asipate mimba na baada ya hapo viungo hivyo tulikuwa tunavitupa.

Baada ya hapo tulikuwa tunachukua upande mmoja wa mbavu,kidali,mapafu,moyo,shingo na mguu mmoja na kuvipika huku ukichanganya na dawa.baada ya kupikwa mgonjwa alikuwa akipewa mchuzi kama lita moja na nyama nzuri kula na kunywa.

ITAENDELEA
 
sometimes dawa za kienyeji kwa watu wanaoamini taboos zao wanahs zinasaidia but for what i know local medicines during pregnacy inaleta effect nying sana kwa mfano ,,can lead to maternal or child death due to overdosage,,,congestive cardiac failure eg some drugs certain digitali which may lead to cardiac failure,,,,liver failure due to intoxication coz dawa za kienyeji hazina dose maalum,,,,severe vaginal bleeding from uterus in child birth,,,Rupture of uterus some drugs cause very strong contraction but there maybe obstructed labour,,, then inaweza sababisha severe indfections,,,Thanks..

Corrupted mind.

Dawa za Kiafrika ndio bora kuliko za Kisasa, vizungumkuti vya mortality rate vilianza baada ya watu kuhamasika sana wakajifungulie spitali na kwa njia za kisasa. Yawezekena wapo matapeli wanaowapa watu sumu kwa jina la dawa, lakini ubora wa dawa zetu si wa kutia shaka hata kidogo.
 
Mabibi na mababu zetu waliwahi muda mrefu Sana kwa matumizi sahihi ya dawa za kienyeji, dawa hizi zina virutubisho na kinga mbalimbali ambazo Mungu ameziandaa kwa mfumo wake tangu uumbaji isipokuwa tukitumia vibaya basi itasababisha madhara, lakini watu weupe wametusababishia madhara zaidi kwa dawa zao kwa makusudi na bahati mbaya.
 
Conservative Mind:

Dawa za kisasa na medication kwa ujumla wake zinafanyiwa tafiti. Na zinatolewa maelezo zitumike vipi na kwa kiwango gani kulingana na ukubwa wa tatizo. Sio kubahatisha kama dawa za asili.

It should also be noted kwamba dawa za kisasa (most) zinakuwa processed kutoka katika mimea (herbs) na kupelekwa maabara kwa ajili ya kuzalisha hizi dawa rasmi kwa ajili ya matumizi ya binadamu (human consumption) kwa uhakika na kuepusha ile dhana ya kubahatisha.

SIKATAI; zamani (na baadhi hadi sasa) walitibiana kwa hizi dawa za asili na kupona, lakini it was totally unsafe and insecure.... So kuja kubeza dawa za kisasa ni aidha huelewi umuhimu wa uwepo wake na mchango wake, au uko unachachafywa na maelezo kutoka kwa wapinzani wa biashara wanaongelea vibaya dawa hizi!

Hii porojo ya kuwa zinafanyiwa utafiti na zinatokana na mimea imekuwa ikitumika muda mrefu kunadi mfumo wa kisasa wa tiba za viwandani, ambazo ni biashara zaidi kuliko tiba na mbaya ni kuwa zinatokana na kemikali kwa kiasi kikubwa na zina madhara mengi ya ziada kwa watumiaji.

Mimi si mtafiti, lakini takwimu chache zinaonesha kuwa kiwango cha vifo vya uzazi kimeongezeka huku Afrika kweusi baada ya kununua propaganda za biashara ya tiba kutoka kwa Wazungu, miaka inavyoenda pia, licha ya kukua kwa teknolojia ya madawa na vifaa tiba bado kiwango cha maisha kinapungua kwa kiasi kikubwa sana, kwanini?

Mataifa kama China na Japan, Serikali zao zimewekeza kwenye tiba za asili kwa teknolojia ya kisasa na nadhani ndizo nchi zenye watu wanaoishi muda mrefu.

Sisi tunacho kitengo cha tiba asili pale Muhimbili, lakini kinadumazwa kwa makusudi ili biashara ya madawa ya viwanda vya nchi za mabepari izidi kusitawi (na tuendelee kufa). Wewe ni shuhuda, kwa umri wako huu umeshuhudia tiba elekezi ya Malaria ikibadilika kila baada ya miaka kadhaa kwa sababu tofauti, unadhani ni kwanini?

Unadhani hawajui kuwa aloe vera, mbegu za jamii ya machungwa, mbegu za papai, shubiri, muarobaini na mimea lukuki inatibu Maleria kwa ufanisi wa asilimia mia na bila kuacha madhara mengine?

Ni vigumu na inataka akili ngumu kuwaamini watu wale wale waliodhamiria kukuua kwa madawa na sumu waje wakupe tiba sahihi. Teh!

#RevolutionWillNotBeTelevised
 
Mabbibi na mababu zetu waliiahi muda mrefu Sana kwa matumizi sahihi ya dawa za kienyeji, dawa hizi zina virutubisho na kinga mbalimbali ambazo Mungu ameziandaa kwa mfumo wake tangu uumbaji isipokuwa tukitumia vibaya basi itasababisha madhara, lkn watu weupe wametusababishia madhara zaidi kwa dawa zao kwa makusudi na babati mbaya.
Shkamoo kaka mkubwa.

Weusi wenzangu hawaelewi ukweli kuwa Makampuni haya ya dawa ya kibepari ndio yaliyotengeneza sumu kali zilizotumika katika vita za maangamizi za Australia na Vietnam, yawezekanaje leo wakaja kukupa wewe tiba?

Inachekesha?
 
Corrupted mind.

Dawa za Kiafrika ndio bora kuliko za Kisasa, vizungumkuti vya mortality rate vilianza baada ya watu kuhamasika sana wakajifungulie spitali na kwa njia za kisasa. Yawezekena wapo matapeli wanaowapa watu sumu kwa jina la dawa, lakini ubora wa dawa zetu si wa kutia shaka hata kidogo.

Mheshimiwa Mphamvu,

Natanguliza heshima,

Mimi binafsi napata shida kidogo kuelewa hasa tunapozungumzia madawa ya kienyeji/asili na madawa ya viwanda.......
Kwa uelewa wangu neno dawa maana yake ni kemikali ya aina fulani kwa matumizi/matibabu ya tatizo fulani...... dawa ya kifua....dawa ya meno....dawa ya choo...dawa ya sumu ya nyoka nk.

Kwa mfano mti wa muarubaini (mizizi, shina na majani) yanatibu zaidi ya magonjwa 200 ya binadamu, wanyama na mimea kwa ujumla wake..... Sasa inapotokea mtu anayeumwa homa ya malaria na mwingine ana michango ya tumbo wote wanapewa juisi ya majani ya muaubaini kwa kiasi wanywe ili wapone...... Lakini mmea wa muarubaini una kemikali nyingi sana hivyo aliyekunywa kwa ajili ya kupona malaria mwili wake utachukua ile kemikali inayoponyesha malaria hivyo hiyo na yule mwenye michango ya tumbo........ Tatizo hapa hatujui madhara ya muda mfupi au muda mrefu wa matumizi wa zile kemikali nyingine ambazo hatuhizitaji katika kuponya tatizo letu......

Madawa ya viwandani ni muendelezo wa kitaalam wa madawa ya asili... Kama wagonjwa wote wa malaria na michango ya tumbo walipona kwa kunywa majani ya muarubaini utafiti hufanywa ili kujuani kemikali zipi zinatibu malaria na zipi zinaibu michango ya tumbo.......hivyo huchujwa na kutengenezwa dawa mbili tofauti....ili aliye na malaria anywe stahili yake vilevile aliye na michango ya tumbo....

Tofauti na dawa za kienyeji/asili ambazo huwa tunajiuliza kama zinaponyesha au la....dawa za viwandani huendelea kufanyiwa utafiti-muendelezo ili kuifanya iwe bora zaidi kwa kupunguza madhara ya ziada (side effects) kwa mtumiaji.

Africa tofauti ya ulaya na sehemu kubwa ya amerika.....tuna mimea na wanyama wengi wanaweza kutupatia dawa za kutusaidia katika matatizo yetu mbalimbali kama wataalam wa tiba za asili na wa tiba ya kisasa wakishirikiana kwa kiwango kikubwa................... ni mawazo yangu tu

Identification and characterization of chemical compounds in different crude extracts from leaves of Omani neem
 
Corrupted mind.

Dawa za Kiafrika ndio bora kuliko za Kisasa, vizungumkuti vya mortality rate vilianza baada ya watu kuhamasika sana wakajifungulie spitali na kwa njia za kisasa. Yawezekena wapo matapeli wanaowapa watu sumu kwa jina la dawa, lakini ubora wa dawa zetu si wa kutia shaka hata kidogo.
Mkuu Mphamvu nafurahi jinsi unavyozikubali dawa zetu za asili, kiukweli hata hizi dawa za kisasa nyingi zinazototumika sasa active ingredients zao zinatokana na mimea/mazao ya mimea. Nataka kupata maoni yako kuhusu uhakika wa dose unaotolewa kwenye dawa za asili kama, je inawezekana kujua pasi na shaka kuwa kiwango cha dawa ni toshelezi au pungufu ya mahitaji ya mgonjwa? Vipi kunaweza kuwa na dawa zisizotibu tatizo husika? Vipi overdose haiwezi tokea na ikawa sumu?
 
Last edited by a moderator:
Corrupted mind.

Dawa za Kiafrika ndio bora kuliko za Kisasa, vizungumkuti vya mortality rate vilianza baada ya watu kuhamasika sana wakajifungulie spitali na kwa njia za kisasa. Yawezekena wapo matapeli wanaowapa watu sumu kwa jina la dawa, lakini ubora wa dawa zetu si wa kutia shaka hata kidogo.
....Kuhusu kujifungulia kwenye vituo na mortality rato/rate ningependa kupata mtizamo wako kuhusu ni sababu zipi zinasababisha vifo vya watoto na wakinamama wakati wa ujauzito na kujfungua, na unadhani zinaweza tatuliwa kwa urahisi zaidi mama akiwa nyumbani au hospitali/kituo cha huduma za afya?
 
Hii porojo ya kuwa zinafanyiwa utafiti na zinatokana na mimea imekuwa ikitumika muda mrefu kunadi mfumo wa kisasa wa tiba za viwandani, ambazo ni biashara zaidi kuliko tiba na mbaya ni kuwa zinatokana na kemikali kwa kiasi kikubwa na zina madhara mengi ya ziada kwa watumiaji.

Mimi si mtafiti, lakini takwimu chache zinaonesha kuwa kiwango cha vifo vya uzazi kimeongezeka huku Afrika kweusi baada ya kununua propaganda za biashara ya tiba kutoka kwa Wazungu, miaka inavyoenda pia, licha ya kukua kwa teknolojia ya madawa na vifaa tiba bado kiwango cha maisha kinapungua kwa kiasi kikubwa sana, kwanini?

Mataifa kama China na Japan, Serikali zao zimewekeza kwenye tiba za asili kwa teknolojia ya kisasa na nadhani ndizo nchi zenye watu wanaoishi muda mrefu.

Sisi tunacho kitengo cha tiba asili pale Muhimbili, lakini kinadumazwa kwa makusudi ili biashara ya madawa ya viwanda vya nchi za mabepari izidi kusitawi (na tuendelee kufa). Wewe ni shuhuda, kwa umri wako huu umeshuhudia tiba elekezi ya Malaria ikibadilika kila baada ya miaka kadhaa kwa sababu tofauti, unadhani ni kwanini?

Unadhani hawajui kuwa aloe vera, mbegu za jamii ya machungwa, mbegu za papai, shubiri, muarobaini na mimea lukuki inatibu Maleria kwa ufanisi wa asilimia mia na bila kuacha madhara mengine?

Ni vigumu na inataka akili ngumu kuwaamini watu wale wale waliodhamiria kukuua kwa madawa na sumu waje wakupe tiba sahihi. Teh!

#RevolutionWillNotBeTelevised

Idadi ya vifo vya kina mama wakati wa uzazi barani Afrika amekua ikipungua na si kuongezeka. Hata hivyo kasi ya kupungua ni ndogo kuliko hali ilivyo kwenye nchi zilizoendelea.Sababu ni kuwa Africa hatujawekeza kiasi cha kutosha kwenye miundombinu, mifumo, watumishi, madawa na vyenzo nyngine za kupambana na hivi vifo. Kwa kifupi ni kuwa mama zetu hasa wa vijijini hawazifikii/hawapati huduma za dharula za uzazi kwa wakati na kiwango/ubora wa kutosha kuokoa maisha yao
 
Hizi dawa za kienyeji mimi sinaga imani nazo kwa sababu kuna mmasai aliniuzia dawa ya kienyeji nikaitumia badala ya kumaliza tatizo ndo likaongezeka zaidi ..
 
Jadilini mkihusisha na afya ya uzazi.
Nimeipenda mada kama ilivyo, najifunza hapa.
 
Dawa za kienyeji ni nzuri lakini hazijafanyiwa utafit.Pregnancy ni kipindi delicate sana na wamama wanapaswa kuwa makini na kila walacho.
 
Dawa za kienyeji@asilh ni bora kuliko dawa za kemikali\marekani.wanatunywesha sumu tunapata matatizo ya nguvu ya kiume kila siku.na hukuna solusheni ukitumia dawa za sumu-kemikali hautamudu tendo la ndowa na kusababisha mimba kuaribika kwasabab ya dawa za sumu.
 
Hii porojo ya kuwa zinafanyiwa utafiti na zinatokana na mimea imekuwa ikitumika muda mrefu kunadi mfumo wa kisasa wa tiba za viwandani, ambazo ni biashara zaidi kuliko tiba na mbaya ni kuwa zinatokana na kemikali kwa kiasi kikubwa na zina madhara mengi ya ziada kwa watumiaji.

Mimi si mtafiti, lakini takwimu chache zinaonesha kuwa kiwango cha vifo vya uzazi kimeongezeka huku Afrika kweusi baada ya kununua propaganda za biashara ya tiba kutoka kwa Wazungu, miaka inavyoenda pia, licha ya kukua kwa teknolojia ya madawa na vifaa tiba bado kiwango cha maisha kinapungua kwa kiasi kikubwa sana, kwanini?

Mataifa kama China na Japan, Serikali zao zimewekeza kwenye tiba za asili kwa teknolojia ya kisasa na nadhani ndizo nchi zenye watu wanaoishi muda mrefu.

Sisi tunacho kitengo cha tiba asili pale Muhimbili, lakini kinadumazwa kwa makusudi ili biashara ya madawa ya viwanda vya nchi za mabepari izidi kusitawi (na tuendelee kufa). Wewe ni shuhuda, kwa umri wako huu umeshuhudia tiba elekezi ya Malaria ikibadilika kila baada ya miaka kadhaa kwa sababu tofauti, unadhani ni kwanini?

Unadhani hawajui kuwa aloe vera, mbegu za jamii ya machungwa, mbegu za papai, shubiri, muarobaini na mimea lukuki inatibu Maleria kwa ufanisi wa asilimia mia na bila kuacha madhara mengine?

Ni vigumu na inataka akili ngumu kuwaamini watu wale wale waliodhamiria kukuua kwa madawa na sumu waje wakupe tiba sahihi. Teh!

#RevolutionWillNotBeTelevised
Umezungumza Point kaka Mphamvu Mimi sitotia neno hapo tena ninawangojea watu wengine wazungumze maneno yao Bravo kaka Mphamvu.
 
Last edited by a moderator:
It doesn't matter whether some one know or not bt all in all local medicine is safe than morden medicine considering that kuna mixing ya mavitu mengi katika madawa ya kixaxa kwa ajili ya kuweza kukaa dukani kwa mda mrefu bila kuharibika in totality vitu hivyo huwa ni sumu au chemicals ambazo huwa na madhara mengi katika mwili wa binadam compared na zle dawa za asili ambazo hazichanganyi na chemicals zozote!!!!!!!
 
Hizi dawa za kienyeji mimi sinaga imani nazo kwa sababu kuna mmasai aliniuzia dawa ya kienyeji nikaitumia badala ya kumaliza tatizo ndo likaongezeka zaidi ..

Hao wapiga dili tu dawa nenda vijijini ndani huko kuna dawa za kila aina na wengi wenye karama kama anatatizo au tatizo limetokea atapata ndoto ya kumuelekeza ampatie dawa gani na aitengenezaje,huko hakuna hospitali wala nini ni mwendo wa tamaduni mwanzo mwisho
 
Corrupted mind.

Dawa za Kiafrika ndio bora kuliko za Kisasa, vizungumkuti vya mortality rate vilianza baada ya watu kuhamasika sana wakajifungulie spitali na kwa njia za kisasa. Yawezekena wapo matapeli wanaowapa watu sumu kwa jina la dawa, lakini ubora wa dawa zetu si wa kutia shaka hata kidogo.

uzalendo mwingine utatuua bila sababu, dawa zetu ambazo tunazijua tu kwa majina wala hatujui ndani yake kuna nini si bora kuliko dawa za kigeni tuwe wakweli tu. Mara nyingi ukienda kutibiwa kwa dawa za asili hutoambiwa ni malaria wa typhoid utaambiwa vitu vya ajabu ajabu, kuna uwezekano kua dawa zetu zina vijitiba ndani lakini huaga hatuko certain wakati tunatoa tiba za asili, tunahisi tu kua mtu atapona akichanganya hii na ile. Kuelimika kupitia foreign knowledge sio kua corrupted ndugu yangu. Penye ukweli tuseme ukweli, tusitumie dhana ya uzalendo kupotoshana. Sijawahi kuona case kua kuna mtu kapata matatizo ya afya ya uzazi kwasababu ya kutumia dawa za kienyeji lakini isiwe kigezo cha kusema kua dawa za asili ni bora kuliko za kigeni. Tuseme ukweli hata kama ni wazalendo.
 
Back
Top Bottom