Madawa ya Kulevya: Mfanyabiashara Mharami Mohamed na wenzake 4 wakamatwa na kilo 7 za Heroin

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680
Hii imetokea usiku wa kuamkia leo maeneo ya Magomeni Kagera.

Polisi walilazimika kutumia risasi (kufyatua hewani) katika kuhakikisha wanawatia mbaroni. Anaitwa Mharami Chonji Mohamed.

Taarifa zaidi zinakuja

du hii inchi viongozi hadi wanaichi matatizo, uyo mdini nae kesho ndo kiongozi tena.
 
huyu jamaa ametupotezea vijana wengi sana na ata wengine kunyongwa,kutokana na kuwafanya Punda Madawa
 
Ndugu, Jamaa na wapambe wake wanajichanga muda huu kupeleka fungu kwa wazee wa favor. Kesho utaskia katoroka au ilikiwa ni aspirin hizo kwa kuwa mtuhumiwa ni mfanyabiashara wa maduka ya dawa. Policcm wetu bhana
 
ngoja tuone kama hizo kilo 7 za Heroin zitaonyesha zote kesho
 
Amekatwa na madawa ya kulevya au vitu vinavyohisiwa kuwa ni madawa ya kulevya? polisi wanatembea na vitendanishi (reagents) siku hizi? ukikamatwa na bidhaa inahiswa kuwa ni madawa wanapima faster at crime scene? au ndo zile hukumu zetu mtu kasema mwiziiiiiii basi tunaanza mawe, lete mafuta then kiberiti?
 
Hii imetokea usiku wa kuamkia leo maeneo ya Magomeni Kagera.

Polisi walilazimika kutumia risasi (kufyatua hewani) katika kuhakikisha wanawatia mbaroni. Anaitwa Mharami Chonji Mohamed.

Taarifa zaidi zinakuja

ok mbona jina lake linafafana na kipa WA zamani ?
 
ok mbona jina lake linafafana na kipa WA zamani ?
Tajiri wa Magomeni huyu. Ana ghorofa na ni mtu "anawaweka mjini maaskari kadhaa" kitendo kilichompa kibri na kujigamba 'kaiweka serikali mkononi'
 
Tajiri wa Magomeni huyu. Ana ghorofa na ni mtu "anawaweka mjini maaskari kadhaa" kitendo kilichompa kibri na kujigamba 'kaiweka serikali mkononi'

ngoja tuone Dpp mpya hatafanyaje,maana yule WA zamani nasikia alikuwa corupt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…