Madee amekufuru!

Madee amekufuru!

Mimi sijausikia huo wimbo lakini ningesema, 1. Kama alisema alipata mateso kuliko ISA basi nikiwa kama mkristo najua ISA Bin Mariam anayezungumzwa na wenzetu sio yule Yesu Kristo wa Nazareth aliyesulubiwa zamani za pontio Pilato, 2. Kama amesema YESU akimaanisha YESU Kristo wa Mnazareth mwana wa Mungu sitaona bado ni kufuru kwani mateso ni comparison term, na hakuna katika biblia ambapo panasema mtu hawezi kujifananisha na YESU, Biblia inasema yesu alizaliwa duniani kama Mtu na aliishi kama mtu kwanini tuanze kutumia maneno ya "Kufuru" huu sio msamiati wa kikristo, sisi tuna maneno ya Heri yao au Ole wao basi mumeaanza kuchanganya mambo wakuu wangu! Mnaogopa kuwa kama wao wakati huo huo mnaanza ku-reason kama wao

Inawezekana hakuna sehemu kwenye bible iliyosema hivyo lkn nadhani si busara kujifananisha au kijilingalisha na mitume, manabii au mungu. Personally sioni kama ni busara kufanya hivyo ndio maana ktk uislam haturuhusu vitu kama hivi...

Yesu mwana wa mungu ktk ukristo na Mtume ktk uislam is not just a person unaweza kumwimba imbaa tu


Regards
 
Mateso ya Yesu hayakuwa unique kwa wakati wake, hiyo ndo ilikuwa standard way ya kuwaadhibu wahukumiwa. Ndo maana kulikuwa na wezi wawili waliosulubiwa na Yesu.

Nadhani jamaa alikuwa anajenga picha tu, hakuwa anajifananisha.
 
Jamani hivi mmesahau kilipochorwa kikatuni tena Ulaya lkn ndugu zangu WAISLAM bongo waliandamana au walitaka kuandamana kupinga hicho kikatuni,huyo madee kamuimba yesu still wakristu wako kimya,tujiulize kama angesema jambo kuhusu Muhamad ingekuwaje?mhhhh
 
nyie vipi kwani yesu nani? hebu nipisheni hapa.....yesu si alikuwa binadamu kama sisi tu au
 
Madee mwanamuziki wa midundo ya bongo flavor amekufuru kwenye wimbo wake anaosema amepata mateso makali kuliko ya Yesu.

Wakristo wanaamini kuwa hamna mtu amewahi kuteswa kama yesu. Madee akiwa ni muislamu, hakupaswa kulinganisha taabu zake na mateso ya yesu.

Madee amekufuru.
Angekuwa ni Mtume Mohamed amefanyiwa hivyo huyo Madee angetangaziwa Fatwa,na huko Manzese asingekaa,hakika wakristu hawana noma,nakumbuka marehemu Mwanyiro alichimbwa mkwara na waislamu kwa kuvaa kanzu stejini akingurumisha nyuzi bin nyuzi,hata Madega wa Yanga alikiona cha moto alipochapisha tiketi zikiwa na dua na hizo tiketi kutupwa chini na kukanyagwa mpira ulipoisha,ndugu zetu walimjia juu kwa kudharirisha dini yao
 
mimi mijadala kama hii huwa siipendi!!! acha wafu wazke wafu wao.................
 
Inawezekana hakuna sehemu kwenye bible iliyosema hivyo lkn nadhani si busara kujifananisha au kijilingalisha na mitume, manabii au mungu. Personally sioni kama ni busara kufanya hivyo ndio maana ktk uislam haturuhusu vitu kama hivi...

Yesu mwana wa mungu ktk ukristo na Mtume ktk uislam is not just a person unaweza kumwimba imbaa tu


Regards

Kuna mdosi mmoja ana kanisa Tegeta na tv yake Agape anajiita mtume. vipi huyo amekufuru nisaidie mkuu
 
double thumbs up for Jesus.. he is my one and only Saviour...shine Jesus shine
 
jamani si ndio lugha za kisanii??

Mtu anavyojiita ATM, bunduki, jua, mwezi nabii nk. si ndio expresions zenyewe?
 
Kuna mdosi mmoja ana kanisa Tegeta na tv yake Agape anajiita mtume. vipi huyo amekufuru nisaidie mkuu

Naye ametangaza kupata mateso kama ya Yesu msalabani? Je Madee amechapwa mijeledi na nani? Je amesulubiwa lini na wapi?
 
ujosefu wa akili na fikra dumavu as you know wasanii wengi elimu hakuna! Tumsamehe tu coz hajui hatendalo kama biblia inavyotuagiza!!!!
 
Mateso ya Yesu hayakuwa unique kwa wakati wake, hiyo ndo ilikuwa standard way ya kuwaadhibu wahukumiwa. Ndo maana kulikuwa na wezi wawili waliosulubiwa na Yesu.

Nadhani jamaa alikuwa anajenga picha tu, hakuwa anajifananisha.

Je wale wahalifu walipigiliwa misumari? Je walichomwa mkuki ubavuni? Mateso ya Yesu yalianza alhamis saa mbili usiku hadi Ijumaa saa 9 alipokufa.
 
Jesus Christ is GOD and we have no other one........watu wengi humtaja Mwenyezi Mungu lakini hawajui kuwa hata shetani naye hujiita GOD>>>>>>>>>>>>>>>>

GOD ought to have a name to distinguish Him from pretenders like Satan or should I call him a fallen angel???????????
 
Mungu wa Kweli apiganiwi, ila anajipigania, na ikiwa hivyo mapigo yake ni ya uhakika. Huyu dogo aende back in times amu ulize Farao kilichomtokea. Kama ameamua kufanya kufuru kwa umaarufu wake wa kitambo kidogo wa hapa duniani, tuone kama huo umaarufu utaendelea baada ya kifo. Usharobaro wake amalize kwenye usanii na siyo aanze kufanya mizaa na imani, moto utaanza kumuakia hapa duniani mpaka ziwa la moto. Ushauri wa bure tu kama anataka kuchezea mboni za jicho, achezee za wanadamu na masharobaro wenzake lakini si za Mungu, maanake mapigo yake ni ya uhakika, shika Biblia soma na ujionee wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom