Madee: Ferouz alizingua kufanya chorus kwenye wimbo wangu

Madee: Ferouz alizingua kufanya chorus kwenye wimbo wangu

Kama kuna wimbo ambao madee anaupa heshima ya pekee ni wimbo wa Yote maisha aliomashirikisha Pfunk.
Wimbo huo anadai ulimtambulisha kwa mara ya pili na pia kumfanya watu waamini kuwa hakubahatisha baada ya kutambulishwa na wimbo wa kazi yake Mola.
Madee anasema ilikuwa 2006 mwishoni na kwamba ule wimbo ilitokea kwamba alikuwa amekwenda Bongo records kurekodi wimbo wake wa Cheza kidogo aliomshirikisha CP.
Baada ya kurekodi na kumaliza Pfunk akaweka beat, madee akaielewa sana Pfunk akamuuliza umeipenda, madee akakubari akamwambia basi chukua ukaiandikie ngoma.
Anadai kipindi hicho uliokuwa waweza pewa beat ukae nalo hata mwezi unaandika ngoma tu (huenda hii ndiyo ilikuwa sababu walikuwa wanaimba nyimbo zenye maana).
Baada ya muda akarudi studio akiwa ashaandika mashairi na kuanza kumchania Pfunk ambapo aliipenda akamwambia hii ngoma kwa jinsi ulivyoandika ina feeling za kusikitisha sasa hapa akae Ferouz kwenye chorus ambaye kipindi hicho alikuwa katisha sana kwa michorus.
Basi kutokana na kwamba Ferouz alikuwa chini ya Bongo records chini ya Boss Majani, Majani akamtafuta ila kila mara Ferouz akawa hatokei. Madee anasema hajui ni kwanini alikuwa anazingua japokuwa Pfunk alikuwa ni boss wake kwa maana Ferouz alikuwa chini ya Bongo records.
Pfunk alivyoona muda unakwenda akaamua atie Chorus na back Vocal mwenyewe maana alitokea kuifeel kwakuwa ilikuwa kwa namna moja ama nyingine inamgusa kutokana na kwamba kwa kipindi hicho alikuwa amekorofishana na mzazi mwenzie ambaye alikuwa bado anampenda Kajala Masanja.
Pfunk aliipendezesha ngoma huenda hata Ferouz asingeweza kufanya kile alichofanya majani humo ndani.
Ngoma ilikuwa hit sana na iliwagusa wengi na nina imani wengi mpaka leo wakiusikia huu wimbo unawarudisha enzi hizo za Bongo Records
Mpaka leo ipo kwenye playlist yangu. Hakika majani aliitendea haki hii nyimbo
 
Madee nyimbo zake kali mbili tu:
1. Kazi yake Mola.
2. Yote Maisha.

Alipofiwa na Pendo akachanganyikiwa hadi leo anachoimba sikielewi.

Hivi pendo ni yule aliyekuwa anasoma st. Jones dodoma?
 
Dah mapenz bhna Mungu amrehemu pale chuo alikuwa na mchumba pia daah
Walikuwa washaachana ila Madee inaelekea alikuwa bado anampenda sana demu hata alivyokufa jamaa alizimia
 
Ferooz utamwambia nini enzi hizo ndio alikua kama diamond, siku hizi sijui yupo wapi.....kweli haya yote ni maisha
 
Hivi mpaka leo maproducer wanamiliki wasanii!??
 
Ferooz utamwambia nini enzi hizo ndio alikua kama diamond, siku hizi sijui yupo wapi.....kweli haya yote ni maisha
Yani kajaribu kila njia kashindwa kurudi..
Juzi nilikuwa nasikiliza nyimbo za dazbaba nipe tano, elimu dunia, daz mwalimu, nikabaki natafakari zilivyo kali na jinsi alivyo kwa sasa.
Kweli time tells everything
 
Kuna goma moja la kitambo sana tip top connection walimshirikisha TID.....Jina lla mwimbo nmelisshau
Mwenye kuijua aniwekee basi

OvA
 
Niliwahi kumsikia madee planet bongo akisema kwamba ile ngoma ya kazi yake mola ndio ilipaswa aifanye ferouz ila feruouz akawa haeleweki baadae p funk akamwambia kwamba kuna watu toka arusha watafanya chorus badala ya feruz
 
Back
Top Bottom