Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Anayetajwa kuwa Afisa wa Jeshi la Polisi, Fatma Kigondo, amejikuta akihusishwa na tuhuma nzito za kuratibu tukio la ubakaji wa kundi na ulawiti wa binti anayeishi Yombo Dovya, Dar es Salaam.
Tuhuma hizo zinamweleza kuwa aliwatuma vijana wanne, akiwemo askari wa vyombo vya usalama, kutenda uhalifu huo mnamo Mei 2024 jijini Dodoma.
Kesi hiyo, iliyofunguliwa na wakili Paul Kisabo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dodoma, inaendelea kusikilizwa tarehe 7 Oktoba 2024, baada ya kuahirishwa mnamo Septemba kutokana na uhamisho wa wakili aliyekuwa akisimamia, Francis Kisenyi.
Wakili Peter Madeleka, ambaye pia ni sehemu ya kesi hiyo, amesema kwamba kutokana na uzito wa tuhuma zinazomkabili Afisa Fatma, anapaswa kuwekwa gerezani akisubiri hukumu.
Madeleka amesisitiza kuwa sheria inapaswa kuchukua mkondo wake ili kuhakikisha haki inatendeka kwa mlalamikaji, ambaye amedai kukumbana na madhila makubwa.