Madeleka: Hatuhitaji kutumia hela kuunda Tume ya Jaji Lila wakati tuna Tume ya haki za binadamu na Jeshi la Polisi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

Wakili Peter Madelekea akizungumza kwenye mahojiano na Crown Media Julai 30, 2026 amesema kuwa nchi tayari ina Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyoundwa kwa mujibu wa Ibara ya 129(1) ya Katiba, yenye mamlaka kamili ya kikatiba na kisheria kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamuambayo ina mamlka ya kushtaki mahakamani hivyo hakuna tija ya kuunda Tume ya Jaji Shaaban Ally Lila kwa aajili ya upepelezi wa wahusika wa Mauaji ya Oktoba 29

Madelekea ameongeza kuwa kazi ya upelelezi wa makosa ya jinai ni takwa la kisheria linalopaswa kutekelezwa na Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi chini ya Mkurugenzi wake, Kamishna Ramadhan Kingai na kwamba majaji walioteuliwa kwenye tume hiyo hawajawahi kuwa makachero au wapelelezi wa polisi, bali uzoefu wao upo katika kusikiliza, kuchambua ushahidi na kutoa haki mahakamani.

Aidha, Wakili Madelekea amesema kuhamisha majukumu ya kikatiba ya Tume ya Haki za Binadamu na ya kisheria ya Jeshi la Polisi na kumpa Jaji Lila hakuwezi kuleta matokeo yoyote ya maana. Alisisitiza kuwa vyombo vilivyopo vya kikatiba na kisheria vilipaswa kuachiwa vifanye kazi yake ya kuchunguza matukio hayo na kuleta majibu ya haki kwa wananchi.
 
Screenshot_20260415-144632~2.png
 
Hizo alternatives anazofikiria Madeleka pia hazifai kwasababu hazikidhi kigezo cha independence.

✍️Polisi ni watuhumiwa wa hayo mauaji—hawapaswi kujichunguza wenyewe.

✍️Commissioners wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni wateule wa Rais ambaye (katika context hii) naye ni mmoja wa watuhumiwa!
 
Back
Top Bottom