Madeleka: Jeshi la Polisi liliundwa kwa sura ya ukandamizaji

Madeleka: Jeshi la Polisi liliundwa kwa sura ya ukandamizaji

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Mwandishi:"Na unahisi hawa wanaosema ugaidi, wanasema kuwa bahati mbaya..."

Peter Madeleka:"Wanamhujumu Rais. Wanamhujumu Rais tuliyonaye huyu. Anajitahidi sana lakini kundi la watu waliopo pembeni yake wanamhujumu. Kwa mfano kesi ya Mbowe, tulihakikisha kabisa Mbowe ni gaidi. Yaani kwamba Mbowe na Osama, unavyomwona Mbowe na Osama... leo hii afya yake Mbowe anaachiwa, anaenda Ikulu, wanapiga picha, wanakunywa chai."

Mwandishi:"Aisee hizi tuhuma za ugaidi kwamba Tanzania tuna watu kadhaa wanatuhumiwa kwa ugaidi, zinatuletea taswira gani kwa nchi zingine?"

Peter Madeleka:"Nchi zingine zinaona sisi ni watu tuliotachanganyikiwa, tusiojitambua. Waziri anasema hivi, mwingine anasema nchi sio salama. Mpaka sasa hivi, sio Serikali wala taasisi nyingine yoyote ina majibu kwamba wanaoteka watu ni kina nani. Hakuna majibu ya msingi, ni blah blah tu. Watu wanapotea, watu wanakufa, watu wanateswa, hakuna usalama. Ni uoga uoga tu, huwezi kutembea. Kila mtu anatembea na mashaka, anageuka kushoto na kulia."

Mwandishi:"Na ni kitu gani kilikusukuma kutoka kuhudumu kwenye Jeshi la Polisi?"

Peter Madeleka:"Jeshi la Polisi, kusema ukweli, tangu limeundwa limekuwa na taswira ya kikoloni. Na ninaposema taswira ya kikoloni, ni taswira ya ukandamizaji kwa sababu Jeshi la Polisi liliundwa kwa ajili ya maslahi ya mtawala wa wakati ule ambaye alikuwa ni mkoloni. Lakini kwa bahati mbaya sana, tulishindwa kulibadili jeshi hilo liweze kuakisi taswira ya uhuru kwa maana ya kuwatumikia Watanganyika na baadaye Watanzania."

Mwandishi:"Ni kweli kwamba ulikuwa ni mtoro kazini au kuna vitu vingine vinaendelea ambavyo tulikuwa hatuvijui?"

Peter Madeleka:"Katika maisha yangu sijawahi kuwa mtoro popote, iwe ni shuleni au kazini, sijawahi kuwa mtoro popote. Na waliosema kwamba mimi ni mtoro kazini, nadhani walikuwa ni waambata tu wa kutosoma historia, lakini ni wavivu wa kufuatilia mambo."

Mwandishi:"Kipi ambacho kilikusukuma kujiunga na ACT-Wazalendo na kuondoka CHADEMA?"

Peter Madeleka:"Nilipoona CHADEMA hawakubaliani na huu mtazamo wangu, ikabidi mimi niondoke kwa sababu wengi... busara kwamba kama hukubaliani na wengi basi wewe ndio uondoke. Inawezekana kwa wakati huo ukawa wewe ndio tatizo, lakini baadaye wakaja kuona wewe sio tatizo, ulikuwa uko sahihi. Kwa nini nilitoka ACT? Nilitoka ACT kwa sababu kile ambacho nilikuwa natarajia pengine ACT ingekuwa inakifanya kama chama cha siasa, sijakiona."

Mwandishi:"Kama kitu gani ulichokitarajia ambacho hakijatokea?"

Peter Madeleka:"Zanzibar kule kuna maridhiano yamefanyika kati ya ACT na CCM. Na unajiuliza maridhiano ya nini? Mnamaridhiana na nani wakati tatizo linaloikabili Tanzania sasa hivi ni kujua ukweli wa kile kilichotokea tarehe 29 Oktoba."

Mwandishi:"Kwa unavyoona, hii tume iliyoundwa na Rais ni Tume ya Kijaji kama ile uliyokuwa ukipendekeza?"

Peter Madeleka:"Mimi najua Rais Samia ana dhamira njema sana. Sasa hivi wanasema waende wakachunguze waliochechemea na waliofadhili... yaani dodoso la urejesho ni mbili: waliochechemea na waliofadhili. Waliouawa je?"
 
Back
Top Bottom