Hii Sasa imeingiaje?
Hivi huwa hamsomi historia ya nchi yetu? Kwa nini mnadhani kila jambo alilolifanya Nyerere alilifanya kulinda nafasi yake?
Hivi Nyerere alikuwa analinda madaraka yake dhidi ya nani hiyo mwaka 1977 wakati Katiba hiyo inatungwa?
Nyerere alikosea kuamini kwenye mfumo wa chama kimoja (Ilikuwa fasheni wakati huo) lakini kusema eti yeye ndiye muasisi wa mateso haya ya Sasa ni kumuonea na kumsingizia asiyohusika nayo.
Mambo ya wakatoliki wenzake kutaka kumfanya awe mtakatifu yanawahusu wao na tuheshimu imani yao.
1997, Nyerere (na watu wake) alitengeneza katiba ya kitu kinachoitwa "
Totalitarian State". Taifa linalotawaliwa kiimla ambapo kiongozi mkuu (Rais) anakuwa na mamlaka kamili juu ya mihimili yote na taasisi zote za kiuongozi, kisiasa, na kijamii pamoja na vyombo vyote vya dola. Maamuzi yake ndio maamuzi ya Taifa. Kauli yake ndiyo ya mwisho katika masuala muhimu ya kitaifa.
Kifupi, Taifa linakuwa ndio yeye na yeye ndio anakuwa Taifa. Ukimsema vibaya, umedhalilisha Taifa. Ukimkashifu, umekashifu/umedharau Taifa. Ukimpinga au kumkosoa basi umesaliti Taifa au hata umefanya uhaini dhidi ya Taifa!
Mwaka 1992, baada ya uamuzi wa vyama vingi vya siasa, kazi muhimu iliyokuwa ifanyike ni kurekebisha katiba kwanza iendane na mahitaji ya demokrasia, na pili iwezeshe vyama vyote vya siasa kushindana kwenye uwanja sawa wa kisiasa nchini. CCM hawakuwa tayari kupoteza nguvu ya mwenyekiti wao aliyekuwa Rais wa nchi kwa mujibu katiba ya 1997. Hivyo waliendelea kuhodhi mamlaka juu ya mihimili, taasisi pamoja na vyombo vya dola vilivyowawezesha kubaki madarakani hadi leo hii.
Huenda Nyerere aliyejua vizuri sana janga la katiba ya 1997 katika mazingira mapya
angesisitiza yafanyike mabadiliko muhimu ya msingi katika katiba, hiyo kazi ya
Reforms ingefanyika bila ubishi. Kama tu alivyoshinikiza vyama vingi na kuvunja jeuri ya G55 kutaka Taifa la Tanganyika. Yaelekea yeye binafsi hakuwa tayari kwa
Reforms na wanasiasa wa upinzani hawakuwa na subira; waliamini wanaweza "kuchukua nchi" hivyo hivyo tu!
CCM hawajawahi kuwa na hawako tayari kuachia karata hiyo Turufu (Katiba ya 1977) kirahisi rahisi tu.
Sad.