PostGE2025 Madeleka: Matukio ya Oktoba 29 yale ni Mauaji siyo Vurugu, kuzungumza Vurugu ni kudogosha “Mauaji”

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakili Peter Madeleka akiwa kwenye Mjadala wa Kitaifa kuhusu hatma ya Nchi uliofanyika leo Mei 16, 2026 amesema;

"Nchi yetu ipo kwenye msiba. Na kwa mara ya mwisho tangu mwaka 1907... mwaka 2025 nchi imeshuhudia mamia ya Watanzania wakiuawa bila sababu za msingi na bila uwajibikaji wowote mpaka sasa hivi."

"Swala la mauaji, kwa sababu hili swala linadogoshwa sana, linaitwa vurugu. Kwenye sheria, Profesa Shivji anajua, kwamba yanapotokea makosa mengine madogo madogo yakachanganyika na kosa kubwa la mauaji, basi yale makosa madogo yote yanafutika linabaki kosa moja la mauaji kwa sababu uzito wake ni mkubwa kuliko makosa mengine. Tunapo-address jambo hili la tarehe 29 October na siku chache zilizofuata baada ya hapo, hatupasi kuzungumza kwamba kuna vurugu zilitokea; tuzungumze kwa uwazi kwamba kuna mauaji yalitokea na sio vurugu. Kuzungumza vurugu maana yake ni kudogosha kilichotokea."

"Leo tunapokuja kuambiwa kwenye ripoti... kwamba moja ya mapendekezo ni kuunda Tume ya kupeleleza yale yaliyotokea ili watu wawajibike kijinai; wanawajibikaje watu kijinai kwa kutumia hiyo tume itakayoundwa wakati tayari watu walishapelekwa mahakamani na ushahidi upo? ...Mimi naamini kwa kuwa tulishakwenda mahakamani tukawashitaki watu kwa uhalifu/uhaini, maana yake upelelezi ulishakamilika. Leo kuja na mapendekezo ya kuunda tena tume ya kupeleleza ni kuwatukana Watanzania ambao wamepoteza ndugu zao."

huyu wakili mlevi nae anatafuta kiki tu but hana jipya kabisa
 
Screenshot_20260514-220943~2.png

Back
Top Bottom