Madeleka: Nitakwenda Tabora kumtetea Sophia, kumtongoza Mkuu wa Mkoa siyo Jinai

Madeleka: Nitakwenda Tabora kumtetea Sophia, kumtongoza Mkuu wa Mkoa siyo Jinai

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X, Wakili Peter Madeleka ameandika:

"Nitakwenda Mahakmani kule Tabora kumtetea Sophia kwa kuwa, kwa mujibu wa sheria siy jinai kwa Sophia kumtongoza Mkuu wa Mkoa."

Ikumbukwe kuwa Septemba 7, 2026, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha wakati akikabidhi Ofisi na madaraka kwa Mkuu wa Mkoa mpya, alisimulia namna alivyokuwa akipokea jumbe za Sophia akimtongoza, mwishowe akaamua kulifikisha suala hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC).

Soma pia Chacha kuna mwananchi ambaye ni mwanamke alinitongoza, nikabidi nilifikishe kwa RPC

1788870522926.png
 
Labda huyo mdada angekuwa stalker basi angeshitakiwa na kuambiwa asisogelee ofisi ya Chacha wala nyumbani kwake wala mahali alipo kwani atafunguliwa shtaka.

Lakini kutongozwa sio kosa kabisa na hata kama alikuwa anamsumbua angepewa onyo tu
Maana imegeuka usumbufu
 
Chacha amewatia aibu wanaume.....na kama alikuwa kimada wake ametumia mbinu hiyo kujisafisha kwa mkewe, ni jambo la kishamba sana.........kwanza kusimama hadharani kusema unatongozwa ni jambo la kitoto sana,hata Police wamekosa kazi,kwasababu kutongoza au kutongoza si kosa
Mayb alikuwa anajisafisha mbele ya mkewe hii inawezekana pia..
 
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X, Wakili Peter Madeleka ameandika:

"Nitakwenda Mahakmani kule Tabora kumtetea Sophia kwa kuwa, kwa mujibu wa sheria siy jinai kwa Sophia kumtongoza Mkuu wa Mkoa."

Ikumbukwe kuwa Septemba 7, 2026, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha wakati akikabidhi Ofisi na madaraka kwa Mkuu wa Mkoa mpya, alisimulia namna alivyokuwa akipokea jumbe za Sophia akimtongoza, mwishowe akaamua kulifikisha suala hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC).

Soma pia Chacha kuna mwananchi ambaye ni mwanamke alinitongoza, nikabidi nilifikishe kwa RPC

Labda mkuu wa mkoa alikuwa anajua anategwa aingie kwenye 18 kama yule RC aliyemlawiti binti kule Mwanza.
 
Ila hii nchi bhanaa.....😜
Penye miti hakunaga wajenzi kabisa....🤣
 
Sasa kutongozwa si ndio uanaume wenyewe, mtu anatongozwa halafu anatoa siri, si angekaa kimya tu? Huko ni kumdhalilisha dada wa watu
 
Duh,
Huyo Chacha amejua kudhalilisha wanaume wenzie. Unaburuza manzi polisi kwa kukutongoza??

Mbona sisi mademu hawatuburuzi na tunawatongoza kila wakati?
 
Back
Top Bottom