Mademu wa kishua ni mzigo

Mademu wa kishua ni mzigo

Sharti unapooa mtoto wa kishua ili ufurahie mahusiano nae ni mambo mawili ya msingi uzingatie.

1. Akupe access ya mkwanja yaani unapokuwa na shida zako za mkwamo wa kifedha yeye awepo kukufadhili bila masharti yoyote yaani awe na ile care ya huruma na wewe.

Hii itakusaidia kumudu gharama za kumpa maisha mazuri kwa wakati wa sasa na ujao huku ukijijenga kifedha. Jitahidi sana uwe na pesa ya backup maana kinyume chake utamtesa na kumfedhesha mtoto wa mama mkwe.

2. Awe mzuri wa kukuvutia sana kiasi kwamba maudhi yake uone kama ni sehemu ya vituko vya kupuuza tu na sio kero. Uweze kumdekeza na kumpa care kama wazazi wake ili aendelee kukupenda.

Kuna mshikaji wangu kipindi fulani alikutana na demu wa hivyo anaitwa Nora. Aisee mtoto ni chotara mzuri balaa. Demu hajui vitu vingi zile sampuli za kufanyiwa kila kitu. Ila mwamba sasa alikuwa anaweza kumcontrol vizuri sana.

Kufua kuna dada alikuwa anakuja kufua na mwingine usafi wa nyumba na mazingira yake ila hawakai hapo nyumbani.

Matumizi,shoppings jamaa anatoa ila binti alikuwa ana mspoil sana mshikaji aisee. Baba wa binti anafanya kazi kenya kwenye kampuni ya mawasiliano ya minara ya simu, mama yake ana asili ya south Africa ni half cast wa kikaburu mzuri balaa mtoto kachukua asili ya mama yake so ni kama mzungu hivi.

Akipewa vitu kama simu sijui raba kali anamletea mwamba, akakomaa atoke kwao kwenda kukaa kwa mshikaji wazazi waligoma ila wakaja kubali baadae. So akawa anaishi na mwamba mikocheni hapo. Walichukua ki apartment.

Jamaa hakuwa na mishe wala nini ila siku zilivyokwenda wazazi walimshinikiza akasome ili aweze kupewa ruhusa ya kukaa na mtoto wao. Jamaa alitii akasomea IT ndipo wazazi wakamsaidia kupata kazi Vodacom.

Akaanza kukaa na binti hapo mikocheni. Walikuja kupata watoto 3.

Ila jamaa demu anamjali sana. Na jamaa anajua kwenda na upepo wa demu. Sasa nilichokiona pale ni demu mzuri halafu anampa jamaa access ya pesa alihitaji atampambania atapigia hata ndugu zake huko majuu wampatie pesa then jamaa anashikishwa. Kwasasa wapo vema sana.

Kuna watu huwa wanamazali yao aisee. Demu mzuri na kwao wanapesa hapo ni wewe tu uharibu.
 
Back
Top Bottom