Shida siyo kudaiwa tu, shida ni unadaiwa na nani?
Mimi roho yangu ni ndogo sana Hata nikidaiwa 50,000 tu siwezi kulala usingizi mpaka nilipe
Nakosa amani kabisa
Twende kwenye mada
Madeni yanaweza kumharibu na kumuathiri mdaiwa kwa kiwango kikubwa kuliko tunavyofikiria, hasa pale anapogundua uwezo wake wa kulipa umekuwa mdogo
Hali inakuwa mbaya zaidi kama anaanza kupokea presha kutoka kwa anayemdai
Yaani kuna watu wanadai vibaya 🤣
Baadhi ya madhara ambayo mdaiwa anaweza kuyapata ni:
Kukosa utulivu
Kila akikumbuka ana deni, mood inabadilika
Kutumia muda mwingi kuwaza namna ya kulipa deni, mpaka anapata msongo wa mawazo na kushindwa kuzingatia mambo mengine
Kuwa na hasira za hapa na pale bila sababu
Kukosa hamu ya tendo la ndoa, au hata mkiwa katikati ya tendo, mood inakata... babu analala yoo! 🤣 Kwa mwanamke pia inaweza kusababisha ukavu
Kuogopa kupokea simu, hasa namba usizozijua
Mwisho wa siku unaweza ukaacha kupokea simu muhimu yenye dili zuri kwa sababu ya hofu
Kukosa uhuru wa kutembea kwa kuogopa kukutana na anayekudai
Na mara nyingi mtu akiwa na deni huwa mnyonge sana
Halafu kuna watu wanajua kudai vibaya sana! 🤣
Kwa hiyo, kama huna ulazima mkubwa, usikope pesa za watu
Na ukilazimika kukopa, basi iwe ni kwa jambo la msingi na ukiwa huna njia nyingine
Je, wewe umewahi kukopa pesa za watu zikataka kukutokea puani?
Ukakosa amani na kujuta?
Baada ya hapo uliendelea kukopa, au ulikula kiapo kwamba hurudii tena?
Ongezea pia ni madhara gani mengine ya kihisia anayoweza kuyapata mdaiwa hasa pale anapogundua kua hana uwezo wa kulipa kwa wakati huo
ShesRise_1 ✋️