Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
22,235
Reaction score
51,111
Shida siyo kudaiwa tu, shida ni unadaiwa na nani?

Mimi roho yangu ni ndogo sana Hata nikidaiwa 50,000 tu siwezi kulala usingizi mpaka nilipe
Nakosa amani kabisa

Twende kwenye mada

Madeni yanaweza kumharibu na kumuathiri mdaiwa kwa kiwango kikubwa kuliko tunavyofikiria, hasa pale anapogundua uwezo wake wa kulipa umekuwa mdogo

Hali inakuwa mbaya zaidi kama anaanza kupokea presha kutoka kwa anayemdai

Yaani kuna watu wanadai vibaya 🤣

Baadhi ya madhara ambayo mdaiwa anaweza kuyapata ni:

Kukosa utulivu
Kila akikumbuka ana deni, mood inabadilika

Kutumia muda mwingi kuwaza namna ya kulipa deni, mpaka anapata msongo wa mawazo na kushindwa kuzingatia mambo mengine

Kuwa na hasira za hapa na pale bila sababu

Kukosa hamu ya tendo la ndoa, au hata mkiwa katikati ya tendo, mood inakata... babu analala yoo! 🤣 Kwa mwanamke pia inaweza kusababisha ukavu

Kuogopa kupokea simu, hasa namba usizozijua

Mwisho wa siku unaweza ukaacha kupokea simu muhimu yenye dili zuri kwa sababu ya hofu

Kukosa uhuru wa kutembea kwa kuogopa kukutana na anayekudai

Na mara nyingi mtu akiwa na deni huwa mnyonge sana

Halafu kuna watu wanajua kudai vibaya sana! 🤣

Kwa hiyo, kama huna ulazima mkubwa, usikope pesa za watu

Na ukilazimika kukopa, basi iwe ni kwa jambo la msingi na ukiwa huna njia nyingine

Je, wewe umewahi kukopa pesa za watu zikataka kukutokea puani?

Ukakosa amani na kujuta?

Baada ya hapo uliendelea kukopa, au ulikula kiapo kwamba hurudii tena?

Ongezea pia ni madhara gani mengine ya kihisia anayoweza kuyapata mdaiwa hasa pale anapogundua kua hana uwezo wa kulipa kwa wakati huo

ShesRise_1 ✋️
 
Unajua kazi ya hizo ndimi?
Screenshot_20260717-093702~2.jpg
 
Duuh nilikopa finca ,Sina hamu....!
 
Sitaki kabisa kukumbuka vile vipindi.. Kila simu iliyokuwa inaingia ilikuwa ya deni
BANK 3
SACCOS 2
Mitandao ya simu🙌🏿🙌🏿
Ila hakuna marefu yasiyo na ncha nili clear mikopo yote ndani ya miaka 2💪🏿
 
Nishawahi kudai hadi mtu alijuta

Nikiwa darasa la 4 nilipewa elfu 10 ya shule wiki nzima.
Muda wa mapumziko nikampa rafiki yangu anishikie tukawa tumesimama duka la nje ya shule.
Wakaja mwanamke na mwanaume wakatulaghai kiufupi wakatapeli ile hela.

Nilimdai rafiki yangu ile elfu 10 kuanzia darasa la 4 mpaka tulipomaliza darasa la 7 deni halikuisha.
Alikua akinilipa mara sh.100 mara 50 hivyohivyo.
 
Sitaki kabisa kukumbuka vile vipindi.. Kila simu iliyokuwa inaingia ilikuwa ya deni
BANK 3
SACCOS 2
Mitandao ya simu🙌🏿🙌🏿
Ila hakuna marefu yasiyo na ncha nili clear mikopo yote ndani ya miaka 2💪🏿
Juzi kuna bank Moja imemfata CEO wa kampuni yangu inataka kuikopesha company 5B nimemwambia aache nifkrie kwanza ntawapa jibu

Jokes 😁
 
Inatakiwa kwanza ujue Kati ya Mkopo na Deni.
Mkopo nikile unachopewa baada ya makubaliana maalumu mfano Riba na mkopeshaji.
Deni linakuja baada ya kushindwa kulipa mkopo hii ndio mbaya.
Mimi nadhani Deni ndio linaleta fedhea ila kuhusu mkopo sioni kama ni kitu kibaya kama unaweza kuutumia vizuri kuongeza wigo wa mambo yako ya msingi kama biashara
 
Melo anakulipa hapa JF?
Mbona umegeuza JF full time job.

Au JF wanalipa kwa engagements na sijui?
Wewe unaniuliza kama nani?

Inakuhusu nini?

Unakereka nini?

Umejuaje kama nipo full time?

Tuseme ananilipa sawa amekopa hela kwako?

Usiniulize tena swali kama hili mimi sio mke wako

Red black jibu lenu acheni upumbavu wa kunihoji
Tumieni ignore kama nawakera

kuna ukomo wa kuposti jukwaani?
 
Back
Top Bottom