Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Ulivyotulia hapo mtu hawezi kuamini unadaiwa 254.98 ya Nipige Tafu hujalipa miezi mitatu sasa

1733.jpg
 
Inatakiwa kwanza ujue Kati ya Mkopo na Deni.
Mkopo nikile unachopewa baada ya makubaliana maalumu mfano Riba na mkopeshaji.
Deni linakuja baada ya kushindwa kulipa mkopo hii ndio mbaya.
Mimi nadhani Deni ndio linaleta fedhea ila kuhusu mkopo sioni kama ni kitu kibaya kama unaweza kuutumia vizuri kuongeza wigo wa mambo yako ya msingi kama biashara
Asante mkuu kumbe ipo hivyo deni ndio kasheshe
 
Mimi ni mgumu kulipa so huwa sikopi coz nimeshajua udhaifu wangu, pesa ikishafika mikononi mwangu kutoka ni ngumu sana😅...
Wewe unajijua hii ni nzuri
Sana kujua udhaifu wako maarifa ambayo wengine hatuna pengine
Hongera, uko na idea nzuri ya nyuzi, ndio maana nyuzi zako naona muda mwingi zinatrend humu jukwaani.
Asante brother 🥰
 
Kuna kipindi nilikuwa dhoofu kiuchumi nikawakopa SONGESHA Tsh 500k kwa ajili ya mambo yangu fulani hivi kama isivyo bahati mambo hayakwenda vizuri, kwakweli sitokaa niwasahau songesha nilkuja kujikuta nawalipa zaidi ya 700k hakika sitosahau deni lile, Wana makato makubwa sana..

NB: Samahani kama nitakuwa nimeharibu biashara ya mtu
 
Back
Top Bottom