Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Nishawahi kudai hadi mtu alijuta

Nikiwa darasa la 4 nilipewa elfu 10 ya shule wiki nzima.
Muda wa mapumziko nikampa rafiki yangu anishikie tukawa tumesimama duka la nje ya shule.
Wakaja mwanamke na mwanaume wakatulaghai kiufupi wakatapeli ile hela.

Nilimdai rafiki yangu ile elfu 10 kuanzia darasa la 4 mpaka tulipomaliza darasa la 7 deni halikuisha.
Alikua akinilipa mara sh.100 mara 50 hivyohivyo.
Wewe binti nimevulia kofia 😀😀
Sasa mlitapeliwa mkiwa pamoja
 
Wewe unaniuliza kama nani?

Inakuhusu nini?

Unakereka nini?

Umejuaje kama nipo full time?

Tuseme ananilipa sawa amekopa hela kwako?

Usiniulize tena swali kama hili mimi sio mke wako

Red black jibu lenu acheni upumbavu wa kunihoji
Tumieni ignore kama nawakera

Maxence Melo kuna ukomo wa kuposti jukwaani?
Hajauliza kwa ubaya mbona anataka kujua na kujifunza isije kuwa unalamba asali mkuu

Acha kuchukulia vitu personal
 
Shida siyo kudaiwa tu, shida ni unadaiwa na nani?

Mimi roho yangu ni ndogo sana Hata nikidaiwa 50,000 tu siwezi kulala usingizi mpaka nilipe
Nakosa amani kabisa

Twende kwenye mada

Madeni yanaweza kumharibu na kumuathiri mdaiwa kwa kiwango kikubwa kuliko tunavyofikiria, hasa pale anapogundua uwezo wake wa kulipa umekuwa mdogo

Hali inakuwa mbaya zaidi kama anaanza kupokea presha kutoka kwa anayemdai

Yaani kuna watu wanadai vibaya 🤣

Baadhi ya madhara ambayo mdaiwa anaweza kuyapata ni:

Kukosa utulivu
Kila akikumbuka ana deni, mood inabadilika

Kutumia muda mwingi kuwaza namna ya kulipa deni, mpaka anapata msongo wa mawazo na kushindwa kuzingatia mambo mengine

Kuwa na hasira za hapa na pale bila sababu

Kukosa hamu ya tendo la ndoa, au hata mkiwa katikati ya tendo, mood inakata... babu analala yoo! 🤣 Kwa mwanamke pia inaweza kusababisha ukavu

Kuogopa kupokea simu, hasa namba usizozijua

Mwisho wa siku unaweza ukaacha kupokea simu muhimu yenye dili zuri kwa sababu ya hofu

Kukosa uhuru wa kutembea kwa kuogopa kukutana na anayekudai

Na mara nyingi mtu akiwa na deni huwa mnyonge sana

Halafu kuna watu wanajua kudai vibaya sana! 🤣

Kwa hiyo, kama huna ulazima mkubwa, usikope pesa za watu

Na ukilazimika kukopa, basi iwe ni kwa jambo la msingi na ukiwa huna njia nyingine

Je, wewe umewahi kukopa pesa za watu zikataka kukutokea puani?

Ukakosa amani na kujuta?

Baada ya hapo uliendelea kukopa, au ulikula kiapo kwamba hurudii tena?

Ongezea pia ni madhara gani mengine ya kihisia anayoweza kuyapata mdaiwa hasa pale anapogundua kua hana uwezo wa kulipa kwa wakati huo

ShesRise_1 ✋️
Mimi ni mgumu kulipa so huwa sikopi coz nimeshajua udhaifu wangu, pesa ikishafika mikononi mwangu kutoka ni ngumu sana😅...

Hongera, uko na idea nzuri ya nyuzi, ndio maana nyuzi zako naona muda mwingi zinatrend humu jukwaani.
 
Wewe unaniuliza kama nani?

Inakuhusu nini?

Unakereka nini?

Umejuaje kama nipo full time?

Tuseme ananilipa sawa amekopa hela kwako?

Usiniulize tena swali kama hili mimi sio mke wako

Red black jibu lenu acheni upumbavu wa kunihoji
Tumieni ignore kama nawakera

Maxence Melo kuna ukomo wa kuposti jukwaani?
Bibiee mbona una masiriko hivyo upo sawa kweli?
Get a life
 
Wewe binti nimevulia kofia 😀😀
Sasa mlitapeliwa mkiwa pamoja
Rafiki yangu alikua ameishika hela kwa madoido kila anayepita anaiona.
Mwanamke akaniambia nimpeleke ofisi ya mwalimu mkuu nikaenda, pale akabaki rafiki yangu na mwanaume.

Kwa M/mkuu hata hatukufika rafiki yangu akaja akasema yule mwanaume kasema turudi wameghairi kuonana na M/mkuu.
Tuliporudi pale dukani hatukumkuta mtu.

Yule mwanamke akasema tusubiri pale dukani akamtafute yule kaka, tukasubiri hawarudi ndo nikaikumbuka hela yangu nikamuuliza rafiki yangu hela ipo wapi,
Akaniambia yule mwanaume alimwambia amshikie ili asiipoteze wakati anatufuata kuturudisha tusiende kwa mwalimu mkuu.

Tulisubiri hawakurudi, hela ikawa imeenda hivyo.
 
Back
Top Bottom