Madeni ya kampeni za 2020 yaibuka, wadai watishia kuipeleka CCM Mahakamani

Pac the Don

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2021
Posts
6,170
Reaction score
7,710
Tenda ya kuzalisha vipeperushi vya CCM wakati wa kampeni za mwaka 2020 ilikuwa ni kubwa, hivyo ikatulazimu kukopa ili tuweze kutimiza lengo la mahitaji tukitaraji kuwa baada ya mwezi fedha ingerudi, lakini hadi sasa hakuna tulicholipwa" Salum Mussa

Kwa kuwa Uhuru Media Group ni kampuni ya CCM, tunakiomba chama kuingilia kati suala la madai yetu ya kuzalisha vipeperushi vya CCM mwaka 2020. Tutaandika barua ya mwisho ya kutaka kulipwa, tusipopata mrejesho mzuri tutakwenda mahakamani" Salum Mussa

Eliatosha Muganyizi: Tunamuomba Mhe. Rais Mama aingilie kati suala la madai yetu, tunapitia kipindi kigumu sana sisi ambao tuliingia mkataba wa kuzalisha vipeperushi vya Chama cha Mapinduzi wakati wa kampeni mwaka 2020 lakini hatujalipwa hadi sasa"

Elifadhar Mdassa: Tumefilisika na hali zetu kiuchumi sio nzuri, tulivyotarajia katika kazi hii, imekuwa ni kinyume chake. Ahadi tunazopewa hazikidhi mahitaji yetu kwa sasa
 
Hakika mambo yaliyofanyika awamu ya 5 yanaendelea kutu umiza watanzania .

Wachilia mbali ufisadi ulio kufuru bado tena kuna madeni lukuki tunatakiwa kulipa kama watanzania yaliyo wachwa na awamu hiyo.

Tazama gazeti ili mjionee kinacho endelea.

 
Naona hili jukumu wamekupa wewe kwa huko chadema.

Kila post moja ya kumtusi Magu unalamba buku mbili.
 
Ninyi ni mafisadi mnataka kuiua nchi kwa drama zenu kumbe sasa hivi kila jambo ni kusingizia awamu ya tano???Huo ni ujinga.
 
Ndio tabia yao? Baada ya uchaguzi wa 2015 Shigongo alilalamika hivi hivi. Sijui kama walimlipa pesa au walimaliza kura za maoni 2020.
 
Mtafuteni Erick Shigongo awape mbinu ya kuidai madeni ccm
 
Maghufuli hayupo, Pole pole hayupo , Bashiru hayupo...!!! Maelekezo ilikuwa uchaguzi ukiisha watalipwa , Maghufuli akafa mapema , Uhalisia ni kuwa wamepigwa....!!
Waliifanyia kazi Ccm (taasisi) na sio watu binafsi, hivyo watalipwa na Ccm na sio hao uliowataja.
 
Kipindi cha awamu ya nne walichapisha fulana na khanga kiasi kwamba waligawa mpaka wakakosa wakuwapa! Kama watu walipenda chama kwanini wasinunue!
Mafisadi wamerudi
 
MLIJITOLEA MUNGU MTU Ashinde kwa KISHINDO SASA MNADAI NINI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…