Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Raid Samia yuko sahihi.Mkuu Petro E. Mselewa, kwanza asante kwa bandiko hili Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?
Very objective, mimi msimamo wangu kuhusu Bunge letu, kwenye hoja ya bunge kuisimamia serikali, bado haujabadilika ni ule ule wa bunge lililopita Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
Na hapa Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?
Japo Rais Samia ametoa maelekezo makali kwa maofisa masuhuli, hii ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere!.
Kilichopaswa kufanywa on the first place ni kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG, alipaswa apishe kwanza, akiwa cleared ndipo arudishwe!.
P
Baada ya CAG kuwasilisha ripoti yake kwa Bungeni hatua zinazofuata ni kama ifuatavyo;
1. Ripoti hiyo hujadiliwa na kamati husika za Bunge kama vile Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
2. Kamati hizo husikiliza na ufafanuzi kutoka kwa viongozi au taasisi za serikali ambao zimeorodheshwa kwenye ripoti ya CAG ili kueleza kuhusu masuala yaliyoibuliwa katika ripoti hiyo ya CAG.
3. Kamati hizo hutengeneza ripoti yao ya maoni kuhusu ripoti ya CAG na huwasilisha kwa Bunge kwa ajili ya majadiliano na kupitishwa.
4. Bunge hupitia ripoti ya kamati na kuamua hatua stahiki za kuchukua, kama vile kutoa maagizo kwa serikali, kuwajibisha watendaji waliohusika na matumizi mabaya ya fedha za umma, au kufanya marekebisho ya sheria na kanuni.
5. Serikali huchukua hatua stahiki kulingana na maagizo ya Bunge na kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unafuatiliwa na CAG kuhakikisha uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha za umma nchini Tanzania.
Ni muhimu kujua ripoti ya CAG inapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na sio mihemko kwani CAG hukagua kwa njia mbali mbali ikiwemo kukagua nyaraka.
Kazi za CAG nchini Tanzania zinasimamiwa na Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008. Sheria hii inatoa mamlaka kwa CAG kufanya ukaguzi wa hesabu za umma kwa niaba ya Bunge na kuwasilisha ripoti kwa Rais, Spika wa Bunge,bunge, Kamati za PAC na LAAC, na kwa umma kwa ujumla.