Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Raid Samia yuko sahihi.

Baada ya CAG kuwasilisha ripoti yake kwa Bungeni hatua zinazofuata ni kama ifuatavyo;

1. Ripoti hiyo hujadiliwa na kamati husika za Bunge kama vile Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

2. Kamati hizo husikiliza na ufafanuzi kutoka kwa viongozi au taasisi za serikali ambao zimeorodheshwa kwenye ripoti ya CAG ili kueleza kuhusu masuala yaliyoibuliwa katika ripoti hiyo ya CAG.

3. Kamati hizo hutengeneza ripoti yao ya maoni kuhusu ripoti ya CAG na huwasilisha kwa Bunge kwa ajili ya majadiliano na kupitishwa.

4. Bunge hupitia ripoti ya kamati na kuamua hatua stahiki za kuchukua, kama vile kutoa maagizo kwa serikali, kuwajibisha watendaji waliohusika na matumizi mabaya ya fedha za umma, au kufanya marekebisho ya sheria na kanuni.

5. Serikali huchukua hatua stahiki kulingana na maagizo ya Bunge na kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unafuatiliwa na CAG kuhakikisha uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha za umma nchini Tanzania.

Ni muhimu kujua ripoti ya CAG inapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na sio mihemko kwani CAG hukagua kwa njia mbali mbali ikiwemo kukagua nyaraka.

Kazi za CAG nchini Tanzania zinasimamiwa na Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008. Sheria hii inatoa mamlaka kwa CAG kufanya ukaguzi wa hesabu za umma kwa niaba ya Bunge na kuwasilisha ripoti kwa Rais, Spika wa Bunge,bunge, Kamati za PAC na LAAC, na kwa umma kwa ujumla.
 
Nimefarijika sana hiki kichwa kinaingia tena kazini this time, kumsaidia Mama. Nina imani na hii Tume kwasababu baadhi ya wajumbe wake nawafahamu kwa karibu ni watu niliofanya nao kazi, naelewa uwezo wao, uimara wao na uadilifu wao, watu wa type hii, ndio wanamsaidia Samia kwa kumwambia ukweli na sio wasaidizi wake uchumi wakiongozwa na msaidizi mkuu wa uchumi, the chancellor of exchequer ambaye ni chawa, atamsaidia nini Samia na kuisaidia nchi!
Juzi kati niliandika humu na magazetini Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..? hiki kikosi kazi kitamsaidia ila Mama nae akubali kuambiwa ukweli na afuate ushauri.

Kile kikosi kazi cha siasa jilijazwa machawa na badala ya kumsaidia ndio kwanza kimeyarudia Madudu yale yale!.
Nina imani sana na Prof. Assad, nimeisha zungunza nae sana na haya ni baadhi ya kauli zake
Huyu ataisaidia sana hii Tume na atamsaidia sana Samia kwa kumweleza ukweli.
P
 
Kaka Pascal nikupongeze kwa maandiko yako yenye manufaa. Shida ya watawala wetu ni moja, utashi wa kutekeleza mapendekezo. Zinaandikwa ripoti nyingi na zinatoa mapendekezo mengi mazuri. Ila serikali haina political will ya kutekeleza mapendekezo/maboresho hayo ya tume. Toka enzi za Mkapa na tume za Jaji Francis Nyalali (marekshisho ya sheria mbovumbovu), tume ya Jaji Kisanga, tume ya Jaji Warioba na tume zingine kibao. Hizi tume huwa zinaandika taarifa nzuri sana na kuainisha mapungufu yanayotakiwa kufanyiwa kazi, lakini serikali haina utashi wa kutekeleza maboresho hayo. Hata tume ije na mapendekezo mazuri kiasi gani, serikali huwa haitekelezi.
 
Acha kuchafua watu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…