Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

hakuna haja ya kuwa na bunge la bajeti, ngosha anatosha kuandaa bajeti na kuitekeleza

Kuna sehemu niliuliza hivi kuna haja gani ya kodi zetu kutumika kugharimia watu karibu 400 Dodoma kwa miezi mi4 kujadili kitu ambacho hakiheshimiwi na hakitusaidii kwa lolote?
 
CAG hawezi pewa hizo hela coz ataenda kukagua zile ndege zetu ambazo siku sionyingi tutazipeleka kule tulikopeleka ile meli, ili msitufuate fuate na maneno yenu ya uchokonozi
 
bajeti ya CAG 2015/16 ilikuwa karibu 80 bilioni kwenye hiyo stationary bajeti ya stationary tu ilikuwa 30% rim moja ikiwa imewekwwa dollar 110 kwa rim na biki dola 60
Wewee, ukitaka kumtetea Juma Maharage wako wewe mtetete tu huna haja ya kutengeza legitimacy entry, nimefanya kazi serikalini more than 20 years tena katika taasisi tofauti. Hakuna afisa bajeti mjinga akaweke rim 1 ya karatasi zinazouzwa 10,000+ kuwa 200,000+. Kweli watu wanapiga serikalini lakini sio hivi. Wacha uzushi.
 
Miaka ya hivi karibuni ofisi za cag zmekuwa zitumwa na wanasiasa kufanya ad hock auditing kinyume na katiba iliyoanshwa idara hiyo.Hapo ndo wanaoneka mhimu.Hizo auditng zingweza kufanywa na wakaguzi wa ndani ili cag andelee na majukumu ya kikatba
 
Hili jambo halijakaa sawa kabisa, sijui tunaelekea wapi kama taifa, isijekuwa kiongozi mkuu tunayemwamini ndio akatuangusha vibaya mno tushindwe kusimama tena
 
...Msingi wa malalamiko ya CAG ni kwamba ofisi yake imepata pesa kidogo sana zilizoizinishwa na bunge kiasi kwamba atashindwa kukagua ofisi za serikali ya kuwasilisha ripoti yake, ambayo lazima iwasilishwe binge lijalo la bajeti. Na akaenda mbali kusema ili asikwame kuwatuma maofisa wake kwenda mikoani ilibidi amueleze mukulu hali halisi.

Pili ametahadharisha kwamba wakati kuna Wizara zimepata below 50% ya bajeti iliyoidhinishwa na bunge kuna zingine zimepata more than 200% !!! na implication ya hii ni kwamba kuna Wizara pendwa zinapata more than kilichoidhinishwa na bunge, jambo ambalo ni hatarin kwani kama una watoto 5 na kwenye mgao wako wa pesa, ambao ni fixed, ukimzidishia mmoja maana yake mwingine atapunjika hivyo malengo yake hayatatimia.
Mimi sijawahi fanya kazi huko kwa watu wazembe wa serekalini, but huku private mkishaandaa budget na ikawa approved kila quarter huwa kuna forecast ambapo hii forecast inaoveride original budget
 
Wanabodi,
Wanabodi, hili ni bandiko kuhusu Kitu Very Serious Kuhusu Mustakabali wa Taifa Letu na Vipaumbele Vyetu ambapo CAG Prof. Mussa Asad Amekisema!. Kama Hii ni Kweli, This is Not Right At All, Hivyo Kwa Mambo Kama Haya, Jee Tanzania Tunakwenda Wap?!.

Tanzania ni nchi yetu sote na sio mali ya mtu na inaendeshwa kwa misingi ya katiba kwa mujibu wa sheria, taratibu kanuni, haiwezekani jambo lililopitishwa na Bunge kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, halafu lisitekelezwe kama sheria ilivyoelekeza, halafu wakati huo huo kuna jambo jingine ambalo halijajadiliwa, halijatengewa budget, hivyo halijaombewa budget, ikawasilishwa bungeni, ikajadiliwa, ikapitishwa, lakini likatekelezwa. Jee limetekelezwa kwa fedha kutoka vote gani, ikiyoidhinishwa na nanI na kwa mamlaka gani, au sheria ipi?!.

Ninavyofahamu mimi ( I stand to be corrected), serikali hutekeleza majukumu yake yote kupitia bajeti ikiyoidhinishwa na Bunge kupitia vifungu mbalimbali yaani Vote na Sub Vote. Hizi fedha hutungiwa sheria na kupitishwa na Bunge kama sheria ya fedha/budget.

Kabla fedha zozote za serikali zilizopitishwa na Bunge haziwezi kutumika kwanza Kabla hazijaidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, na hii ndio role ya CAG kama Mdhibiti Mkuu wa Matumizi ya serikali, kudhibiti matumizi ya serikali yaliyoidhinishwa na Bunge, na kisha baada ya matumizi, CAG hurejea kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo kama zilitumika kama zilivyokusudiwa na hii ndio role ya CAG kama Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Naomba umsikilize kwa makini hapa, CAG, Prof. Mussa Assad kuna kitu very very serious anakizungumza kupitia Habari ya Channel Ten.

CAG Prof. Assad amesema kuna wizara mpaka sasa the final quoter of the budget year, zimeishapewa mgao wa asilimia 16% tuu ya bajeti zake, kwa hoja kuwa serikali haina fedha, lakini at the same time, kuna wizara nyingine zimefanya matumizi ya ziada ya zaidi ya asilimia 230% na serikali hiyo hiyo!.

Hii maana yake kuna maeneo serikali imefanya matumizi makubwa ambayo hayakuwepo kwenye budget ya serikali, hayakuletwa bungeni, hayakujadiliwa wala kuidhinishwa na Bunge na hivyo hayana Vote wala hayakudhibitiwa na CAG, lakini serikali ikafanya matumizi hayo kinyume cha sheria, taratibu na kanuni za fedha za serikali.

Maswali ni
1. Kama serikali imeshindwa kulipa OC za baadhi ya taasisi kwa hoja kuwa haina fedha, jee hizo fedha zilizotumika kufanya matumizi ambayo they were not budgeted for, zimetoka wapi?!. Kama kulikuwa na pot fulani yenye fedha ambazo ziliwafanyiwa ring fencing mapema kabla ya budget zikachimbiwa mahali na kufukiwa na sasa ndio zimefukuliwa, tuelezwe serikali iwe very open na transparent kweli hili kama sehemu ya utekelezaji wa Open Government Initiatives, vinginevyo kuna double standards za hali ya juu sana katika kupanga vipaumbele vyetu vya kibajeti, haiwezekani huyu apewe 16% na mwingine 230% na wote ni watoto wa baba mmoja!. Unless kuna wizara ni watoto wa ndani na kuna wengine au ni wanaharamu au watoto wakufikia!.

2. Matumizi yoyote ya serikali lazima yaidhinishwe na Bunge na kuidhinishwa na CAG katika the Principles of Check and Balance and Separation of Powers. Hii maana yake kuna mtu yeye amejifanya ndio serikali akapanga budget, kisha akajifanya Bunge akaipitisha hiyo budget, akajifanya CAG, akaidhinisha hiyo budget na kujifanya PPRA kwa kutotangaza tenda yoyote ya manunuzi, na kumalizia kwa kufanya matumizi na kuitumia fecha za uma bila id hino ya Bunge, bila kudhibitiwa na CAG, bila kutangazwa Tenda, na bila kuulizwa na yeyote !. How can this be?.

3. Aliyefanya hayo kuidhinisha matumizi ya serikali bila kibali cha Bunge, jee ametumia mamlaka ipi na sheria ipi ndani ya katiba yetu? . Naomba niwakumbushe kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977, hakuna aliye juu ya katiba na japo Rais wa JMT ana kinga ya kutokushitakiwa mahakamani kwa kosa lolote linalohusu utekelezaji wa majukumu yake, lakini akikiuka Katiba ya JMT, hata rais anaweza kuondolewa madarakani na Bunge. Hivyo rais pia yuko chini ya Katiba na atatekeleza majukumu yake yote kwa mujibu wa katiba, kama katiba inasema Bunge ndilo litaidhinisha matumizi ya serikali, then matumizi yote ya serikali yataidhinishwa na Bunge and no one else!.

Ingekuwa ni nchi za wenzetu kamwe wasingekubali hili lifanyike huku na wao wapo tuu na wanaangalia!.

To be honest, nina mashaka sana na Ripoti ya CAG itakayotoka kuelezea madudu hayo haswa kwa kuzingatia kabla Ripoti ya CAG haijawasilishwa Bungeni na kuwa ni public document, lazima kwanza ipitishwe mahali mtu fulani aione, aridhike ndipo iende Bungeni. Kwa vile Ripoti hii itaonyesha haya madudu ya jinsi Bunge linavyokuwa undermined na jinsi CAG anavyokuwa
undermined!. Jee Ripoti hiyo ikapitishwa hivyo hivyo ilivyo? ,au itarudishwa na CAG kulazimishwa kuficha madudu haya kwa kuandaa Ripoti nyingine isiyo muonyesha huyo anayejifanya serikali, kisha anajigeuza Bunge na kujigeuza CAG kwa kufanya matumizi bila kuidhinishwa na Bunge na CAG, ningekuwa mimi GAC, baada ya kufanyiwa haya, sijui ningekuwa wapi maana zamani angeishaikuta barua yangu mezani kwake kitambo kulinda heshima yangu.

Ila kama matumizi haya unbudgeted ni ya fedha zake binafsi kutoka mfukoni mwake, then it's ok, lakini kama ni fedha za serikali, fedha za Watanzania, hatuwezi kuacha fedha zetu zikatumika bila kufuata taratibu za matumizi ya fedha za umma no matter how matumizi hayo ni mazuri kiasi gani, unless ni dharura kama Tetemeko la Bukoba, lakini kwa nchi inayojitapa ni nchi yenye kufuata katiba na kuheshimu the rule of law, lazima ifuate sheria, taratibu na kanuni. Sasa kama hili ni kweli, huu nao sio ufisadi?.

NB. Kama matumizi haya yaliyoidhinishwa na Bunge ni yale yaliyotumika kununulia zile Bombardier za ATC na haya yaliyotumika kuhamia Dodoma, then huu ni ufisadi mzuri, ufisadi wa kimaendeleo ambao mimi naaunga mkono kama ninavyounga mkono udikiteta ukifanyika kwa nia njema.

Jumatano Njema.
Paskali
Rejea
Tangazo hili la serikali halimhusu CAG.
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Prof. Assad amlipua Magufuli kwa ufisadi uuzaji wa nyumba za Serikali
Update

Hii ni taarifa muhimu ya kujua tuko wapi na tunaelekea wapi.
 
Comments zetu kwenye maswala ya msingi zinatuonesha sisi ni watu wa aina gani. Hatujuwi nini hasa tunataka, Taifa gani tunataka kulijenga. Tunachukulia mambo ya msingi ya kujenga Taifa letu kishabiki utafikiri mashabiki wa mpira! Akinatrump wakitutukana tunalalamika; tukiambiwa IQ zetu ndogo tunasema ubaguzi. A well stated argument lkn mtu analeta ushabiki! Tutaendelea kukandamizwa na watawala, kumnyima haki zetu na kuendelea kuwa masikini mpaka mwisho wa dunia kama upo. We will only move forward if we become free from ignorance. Bad enough, our education doesn't free us from poor mind we have.
Naomba nieleweshe kidogo hivi CAG katika kukagua anatumia budget ya Other Charges? Mi nikajua hii OC ni kwa ajili ya vitafunwa na mambo madogo madogo ya ofisi lakini sikujua ndo inatumika kwenye main objective ya taasisi, yaani ni kama wizara ya ujenzi itumie OC kujenga madaraja, naomba msaada tu mimi huko kwa wazembe wa serekali sijawahi fanya kazi
 
Mayala ujuzi wako wa habari unaufukia ktk kina kirefu cha tope. Umeshindwa kuwa moto au baridi ila umebaki vuguvugu kwa hiyo tumekutapika toka ndani ya mawazo yetu na kukuona kila unachopost hakuna maana.
Haya mambo sisi tuliisha yapigia kelele sana ya mtu mmoja kufanya kazi zote za mihimili mingine lkn wewe pamoja na vikaragosi wenzako mmekuwa mstali wa mbele kupingwa na kuonyesha wazi kuwa wenye mawazo kama hao na wavivu wa kufikiri, wivu, na wasiojua kitu.
Sasa unapokuja na post kama hii, inabidi watu wakushangae tu kwa kujiuliza are you serious au ni zile drama zako za kuuma na kupuliza?
IMG_20170221_154603_1-1.jpg
la ofisini standing
IMG_20170221_155608-1.jpg
.
 
Ukijaribu kumsoma, unatambua bayana hata yeye haitaki tena kazi hiyo. Huyu mzee ni makini hapendi dharau.
Tatizo la watanzania wengi ni immaturity, Assad ni moja wao, na uhakika hajawahi fanya private sector walahi asingepanda hata ngazi moja tatizo JK kamuokota huko kutoka Chuoni bila kuangalia level ya maturity yake!!!!
 
Pascal,mi kwa uelewa wangu mdogo naona kazi kubwa ya CAG imetawaliwa na MASWALA YA UCHUMI,tujuilize je mkuu anaufahamu mkubwa juu ya mswala ya uchumi? Hasa hasa katika nchi kama hii ambayo uchumi wake uko kwenye brackets()? Uchumi ambao unahitaji combination ya muundo wa zamani na wa kisasa kuikwamua?

Paskali,kuwa mkuu wa inji,si mchezo! Si kukoroma ukadhani ndio kufanya kazi,inahitaji ufahamu mwingi wa mambo mbali.
Nina wasi wasi kitakacho fuata hapa ni kubadilishwa kwa CAG.
 
Leo umeamkia wapi pascal. Naona umeamua kuweka mahaba pembeni. Katika utendaji ikiwa wizara moja inafikia asilimia 200+ na nyingine 16 hapo huwezi kuisifia hiyo serikali hata kidogo. Hongera kwa kuweka unazi pembeni
 
Back
Top Bottom