Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

So kuna point gani ya kuwalipa wabunge hela zote kumbe wanajadili tu upupu? basi tusiwe na bunge au tubadili vigezo vya mtu kuwa mbunge??
Tulishaomba siku nyingi juu ya ubora wa wabunge. Uganda huwezi kuwa mbunge bila academic degree, Kenya sikumbuki sana lakini hawa ndo tulionao EAC. Wao wanaweka vigezo vya juu sisi tunasema kusoma na kuandika, hata kuhesabu haimo! Watu kama hao ndo watupangie sera za nchi? Watunge sheria za nchi? Wachanganue mitego ya ulaji kama hiyo ya chai maofisini?

sasa eti wakishapitisha wewe mkuu wa nchi ufuatishe hivyo hivyo! NO!
 
Miaka ya hivi karibuni ofisi za cag zmekuwa zitumwa na wanasiasa kufanya ad hock auditing kinyume na katiba iliyoanshwa idara hiyo.Hapo ndo wanaoneka mhimu.Hizo auditng zingweza kufanywa na wakaguzi wa ndani ili cag andelee na majukumu ya kikatba
Mkuu ni bora kukaa kimya tu,acha kupotosha!rudi kasome tena katiba pamoja na sheria ya ukaguzi wa umma na kanuni zake,acha maneno maneno
 
CAG anafanya kazi ya wapizani!!!¡
,yeye kila siku ni kukosoa tu serikali!!!!!! ikibidi ifutwe kubana matumizi!!!!!!
 
NIONYESHE MIMI SIONi
Umeangalia kiwango cha deni la Taifa ukilinganisha deni lililokuwepo na hili la sasa? Shule yako ya jirani watoto wangapi bado wanakaa chini? Ndege si tunazo sasa, je, umegundua nauli ya kukupeleka KIA na kurudi kwa fastjet sasa hivi siyo 1Mil? Nahisi hata mkopo wa bandari mpya ya Bagamoyo umezimwa kinyume na ilivyopitishwa na Bunge. Logical!
 
labda niulize swali rahisi serikali gani ambayo ilienda sawaswa kama ilivyopangwa? yapo mapungufu makubwa katika eneo hili ambayo kikawaida hayaanzii katika serikali tu bali toka katika familia zetu wengi hatuna matumizi tunayokusudia.
haijalishi baba mwenye nyumba ni mkali kiasi gani lakini kilicho sicho ni vizuri ashauliwe na sio kunyamaza eti unaogopa kazi itaisha.
serikali iliyopita tulifikia hata kuhesabu safari za rais na hakuna aliyeangalia positive impact ya safari hizo na ingawa siko huko lakini zilizidi budget.
serikali bado inabadget tano ndo kwanza ya kwanza wacha tuone nini kitafuata kwa budget ijayo nafikiri taratibu ataelewa.
 
Ni vyema bunge luweze kuchukua hatua kali sana dhidi ya wote wanao geuza bajeti ya nchi kuwa kama bajeti ya send-off, kwa sababu haiwezekani bunge liwepange bajeti halafu watu wachache waivuruge kutokana na hisia zao
 
Pasco, bandiko reefu, ukweli ni kuwa tatizo kubwa ni Bunge lenyewe, limeshindwa kujitambua na kutimiza wajibu wake, limekubali kujidhalilisha na sio ajabu halina heshima kwa serikali na watendaji wa serikali, Bunge limekubali dhihaka hii, linekubali kung'olewa meno na sasa halina umuhimu, limepoteza hadhi.

Vv
 
Wanabodi,
Wanabodi, hili ni bandiko kuhusu Kitu Very Serious Kuhusu Mustakabali wa Taifa Letu na Vipaumbele Vyetu ambapo CAG Prof. Mussa Asad Amekisema!. Kama Hii ni Kweli, This is Not Right At All, Hivyo Kwa Mambo Kama Haya, Jee Tanzania Tunakwenda Wap?!.

Tanzania ni nchi yetu sote na sio mali ya mtu na inaendeshwa kwa misingi ya katiba kwa mujibu wa sheria, taratibu kanuni, haiwezekani jambo lililopitishwa na Bunge kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, halafu lisitekelezwe kama sheria ilivyoelekeza, halafu wakati huo huo kuna jambo jingine ambalo halijajadiliwa, halijatengewa budget, hivyo halijaombewa budget, ikawasilishwa bungeni, ikajadiliwa, ikapitishwa, lakini likatekelezwa. Jee limetekelezwa kwa fedha kutoka vote gani, ikiyoidhinishwa na nanI na kwa mamlaka gani, au sheria ipi?!.

Ninavyofahamu mimi ( I stand to be corrected), serikali hutekeleza majukumu yake yote kupitia bajeti ikiyoidhinishwa na Bunge kupitia vifungu mbalimbali yaani Vote na Sub Vote. Hizi fedha hutungiwa sheria na kupitishwa na Bunge kama sheria ya fedha/budget.

Kabla fedha zozote za serikali zilizopitishwa na Bunge haziwezi kutumika kwanza Kabla hazijaidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, na hii ndio role ya CAG kama Mdhibiti Mkuu wa Matumizi ya serikali, kudhibiti matumizi ya serikali yaliyoidhinishwa na Bunge, na kisha baada ya matumizi, CAG hurejea kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo kama zilitumika kama zilivyokusudiwa na hii ndio role ya CAG kama Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Naomba umsikilize kwa makini hapa, CAG, Prof. Mussa Assad kuna kitu very very serious anakizungumza kupitia Habari ya Channel Ten.

CAG Prof. Assad amesema kuna wizara mpaka sasa the final quoter of the budget year, zimeishapewa mgao wa asilimia 16% tuu ya bajeti zake, kwa hoja kuwa serikali haina fedha, lakini at the same time, kuna wizara nyingine zimefanya matumizi ya ziada ya zaidi ya asilimia 230% na serikali hiyo hiyo!.

Hii maana yake kuna maeneo serikali imefanya matumizi makubwa ambayo hayakuwepo kwenye budget ya serikali, hayakuletwa bungeni, hayakujadiliwa wala kuidhinishwa na Bunge na hivyo hayana Vote wala hayakudhibitiwa na CAG, lakini serikali ikafanya matumizi hayo kinyume cha sheria, taratibu na kanuni za fedha za serikali.

Maswali ni
1. Kama serikali imeshindwa kulipa OC za baadhi ya taasisi kwa hoja kuwa haina fedha, jee hizo fedha zilizotumika kufanya matumizi ambayo they were not budgeted for, zimetoka wapi?!. Kama kulikuwa na pot fulani yenye fedha ambazo ziliwafanyiwa ring fencing mapema kabla ya budget zikachimbiwa mahali na kufukiwa na sasa ndio zimefukuliwa, tuelezwe serikali iwe very open na transparent kweli hili kama sehemu ya utekelezaji wa Open Government Initiatives, vinginevyo kuna double standards za hali ya juu sana katika kupanga vipaumbele vyetu vya kibajeti, haiwezekani huyu apewe 16% na mwingine 230% na wote ni watoto wa baba mmoja!. Unless kuna wizara ni watoto wa ndani na kuna wengine au ni wanaharamu au watoto wakufikia!.

2. Matumizi yoyote ya serikali lazima yaidhinishwe na Bunge na kuidhinishwa na CAG katika the Principles of Check and Balance and Separation of Powers. Hii maana yake kuna mtu yeye amejifanya ndio serikali akapanga budget, kisha akajifanya Bunge akaipitisha hiyo budget, akajifanya CAG, akaidhinisha hiyo budget na kujifanya PPRA kwa kutotangaza tenda yoyote ya manunuzi, na kumalizia kwa kufanya matumizi na kuitumia fecha za uma bila id hino ya Bunge, bila kudhibitiwa na CAG, bila kutangazwa Tenda, na bila kuulizwa na yeyote !. How can this be?.

3. Aliyefanya hayo kuidhinisha matumizi ya serikali bila kibali cha Bunge, jee ametumia mamlaka ipi na sheria ipi ndani ya katiba yetu? . Naomba niwakumbushe kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977, hakuna aliye juu ya katiba na japo Rais wa JMT ana kinga ya kutokushitakiwa mahakamani kwa kosa lolote linalohusu utekelezaji wa majukumu yake, lakini akikiuka Katiba ya JMT, hata rais anaweza kuondolewa madarakani na Bunge. Hivyo rais pia yuko chini ya Katiba na atatekeleza majukumu yake yote kwa mujibu wa katiba, kama katiba inasema Bunge ndilo litaidhinisha matumizi ya serikali, then matumizi yote ya serikali yataidhinishwa na Bunge and no one else!.

Ingekuwa ni nchi za wenzetu kamwe wasingekubali hili lifanyike huku na wao wapo tuu na wanaangalia!.

To be honest, nina mashaka sana na Ripoti ya CAG itakayotoka kuelezea madudu hayo haswa kwa kuzingatia kabla Ripoti ya CAG haijawasilishwa Bungeni na kuwa ni public document, lazima kwanza ipitishwe mahali mtu fulani aione, aridhike ndipo iende Bungeni. Kwa vile Ripoti hii itaonyesha haya madudu ya jinsi Bunge linavyokuwa undermined na jinsi CAG anavyokuwa
undermined!. Jee Ripoti hiyo ikapitishwa hivyo hivyo ilivyo? ,au itarudishwa na CAG kulazimishwa kuficha madudu haya kwa kuandaa Ripoti nyingine isiyo muonyesha huyo anayejifanya serikali, kisha anajigeuza Bunge na kujigeuza CAG kwa kufanya matumizi bila kuidhinishwa na Bunge na CAG, ningekuwa mimi GAC, baada ya kufanyiwa haya, sijui ningekuwa wapi maana zamani angeishaikuta barua yangu mezani kwake kitambo kulinda heshima yangu.

Ila kama matumizi haya unbudgeted ni ya fedha zake binafsi kutoka mfukoni mwake, then it's ok, lakini kama ni fedha za serikali, fedha za Watanzania, hatuwezi kuacha fedha zetu zikatumika bila kufuata taratibu za matumizi ya fedha za umma no matter how matumizi hayo ni mazuri kiasi gani, unless ni dharura kama Tetemeko la Bukoba, lakini kwa nchi inayojitapa ni nchi yenye kufuata katiba na kuheshimu the rule of law, lazima ifuate sheria, taratibu na kanuni. Sasa kama hili ni kweli, huu nao sio ufisadi?.

NB. Kama matumizi haya yaliyoidhinishwa na Bunge ni yale yaliyotumika kununulia zile Bombardier za ATC na haya yaliyotumika kuhamia Dodoma, then huu ni ufisadi mzuri, ufisadi wa kimaendeleo ambao mimi naaunga mkono kama ninavyounga mkono udikiteta ukifanyika kwa nia njema.

Jumatano Njema.
Paskali
Rejea
Tangazo hili la serikali halimhusu CAG.
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Prof. Assad amlipua Magufuli kwa ufisadi uuzaji wa nyumba za Serikali
Update

Kaisome Cap 439 kwanza halafu urekebishe habari yako. Wewe si lawyer?
 
Ole wake Mbunge wa CCM atakayekosoa Serikali,atakiona cha moto,nahata wale wanaowapa Muda wapinzani watakiona cha moto.

Mpaka hapo bado una Bunge au Una mfano wa Bunge?
Mkuu sio kweli, unadhani kwa nini CCM waliamua 'kumsamehe' Kimbisa? Hawajiamini kama wangeweza kutetea kiti chake cha ubunge.

Vv
 
  1. Mhimili uliojikita kuliko yote upo kazini. Waganga njaa wanaweza kikaa kimya ili njia ya kwenda msalani isiote nyasi.
  2. Kwa Mwendo huu, anaweza kuona waliomzinguka wakiimba, kumbe moyoni wapo kwenye mgomo baridi.
 
Ilimradi hizo fedha zimetumika kuwanufaisha watanzania na hakuna ufujaji wowote ule (Hili naamini hivyo maana Rais akikujua wafwaaa) Tuvuvumilie,bajeti ijayo hizo wizara zitapewa pia. Maana ni wizara za Tz,pia ndio kwanza mwaka mmoja umeisha.
 
Tatizo la watanzania wengi ni immaturity, Assad ni moja wao, na uhakika hajawahi fanya private sector walahi asingepanda hata ngazi moja tatizo JK kamuokota huko kutoka Chuoni bila kuangalia level ya maturity yake!!!!
Unamjua vizuri Assad? Assad hana maturity? Are you serious? Hebu tafuta cv yake usipate shida.
 
Mengi kama haya yapo nchi hii

na umeweza kugundua kwa sababu ya utashi wako murua

watanzania wengi wako bize na habari za umbeaumbea , ukuda ukuda, wako bize na bashite!!

mambo kama haya huwezi kut wanafuatilia na wanakuwa serious!! haipo
Na ubashite + unyumbani ndio unaoleta maumivu yote hayo,na waunga mkono na utetezi ndio nyie wadandia treni kwa mbele kama ufanyavyo sasa
 
Kabisa. Kama alianza kumnanga mheshimiwa tangu akiwa waziri, then something gonna happen!
Raisi hana mamlaka ya kumg'oa CAG madarakani labda astaafu, afe, awe kichaa au ikibainika mbele jopo la majaji wa jumuiya ya madola kuwa amefanya kinyume na matakwa ya kazi yakee ndio CAG anaweza kung'oka
 
Mengi kama haya yapo nchi hii

na umeweza kugundua kwa sababu ya utashi wako murua

watanzania wengi wako bize na habari za umbeaumbea , ukuda ukuda, wako bize na bashite!!

mambo kama haya huwezi kut wanafuatilia na wanakuwa serious!! haipo
Suala la Bashite ni muhimu na hili ni muhimu vile vile, wacha watu wajadili kwa mapana kila jambo.
 
Back
Top Bottom