Madeni ya TALA na Branch

Tatizo la TALA na BRANCH ni kuwa unakopa elfu 20, mfano. Utatakiwa ulipe elfu 23,000. Wao wanakutumia elfu 20 yao. Siku ya kulipa....unalipa elfu 23 yao plus gharama za kutuma pesa. Wakati wamejisajili lipa kwa mpesa kwanini isiwe malipo bure kama tunavyolipia ving'amuzi.

There are hidden costs.

Sent using my Nokia Torch
 
Ni wewe hapo, acha kumsingizia jamaa yako,
 
Inachukua muda gani hao branch na tala waanze kukukopa laki3 na kuendelea
 
Habar zenu wakuu?
Leo nimetumiwa meseji mbaya sana na Tala inayosomeka hivi:
"Baada ya Taarifa za mkopo wako unaodaiwa Tala kufikishwa mahakamani, mtuhumiwa lazima uitikie wito wa mahakama mara utakapo pokea taarifa, mtuhumiwa lazima ulipe gharama za usumbufu uliojitokeza. Hii ni kwakua umevunja makubaliano yetu ulioweka awali kabla hujachukua mkopo. Malipo yafanyike TALA haraka".
Je hii ni kweli,na je Kuna watu ambao wamewahi kupelekwa mahakamani na Tala?
Naombeni taarifa juu ya hilo.
 
Mikwara hio hawana uwezo huo..watu wa account wanasema wew ni bad debts
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…