Madeni ya TALA na Branch

Madeni ya TALA na Branch

Tatizo la TALA na BRANCH ni kuwa unakopa elfu 20, mfano. Utatakiwa ulipe elfu 23,000. Wao wanakutumia elfu 20 yao. Siku ya kulipa....unalipa elfu 23 yao plus gharama za kutuma pesa. Wakati wamejisajili lipa kwa mpesa kwanini isiwe malipo bure kama tunavyolipia ving'amuzi.

There are hidden costs.

Sent using my Nokia Torch
 
Habar, nahitaji kujua madhara ya kutowalipa hawa tala na branch mkopo uliochukua, maana kuna jamaa yang anadaiwa na elfu 70 tala na laki moja branch na hajawalipa miez kadhaa imepita ila jamaa wanamtumia mesej za vitisho sana hadi namim naogopa kuwakopa ili nitokomee.

MADHARA GANI UTAYAPATA MAANA HATA WAO HAWAJAWEKA BAYANA AU KAMA USHAPATA HAYO MAAFA NIJUZE

Sent using Jamii Forums mobile app
Moja ya mesej ya kitisho
WEWE ENDELEA TU KUWA MKAIDI.WE NI MTU MZIMA UNASHINDWA KUJITUMA UNAAMUA KUJIPATIA KIPATO MTANDAONI KWA NJIA ZA KITAPELI.SI HAUTAKI KULIPA DENI.JIPE MASAA MACHACHE USHUHUDIE FEDHEHA ULIOJITENGENEZEA MWENYEWE. PESA YAKO HAINA THAMANI TENA KWETU MAANA UMETUPA HASARA KUBWA SANA TUPO TAYARI KUTUMIA GHARAMA ZAIDI YA PESA ULIOKOPA KUKUPATA NA KUKUFANYA WA MFANO KWA WOTE WENYE NIA KAMA YAKO ILI IWE FUNZO KWA WOTE ...TUMECHOSHWA NA UTAPELI WAKO!
Ni wewe hapo, acha kumsingizia jamaa yako,
 
Inachukua muda gani hao branch na tala waanze kukukopa laki3 na kuendelea
 
Taarifa kwa wateja wa tala
IMG_20190411_124910_778.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar zenu wakuu?
Leo nimetumiwa meseji mbaya sana na Tala inayosomeka hivi:
"Baada ya Taarifa za mkopo wako unaodaiwa Tala kufikishwa mahakamani, mtuhumiwa lazima uitikie wito wa mahakama mara utakapo pokea taarifa, mtuhumiwa lazima ulipe gharama za usumbufu uliojitokeza. Hii ni kwakua umevunja makubaliano yetu ulioweka awali kabla hujachukua mkopo. Malipo yafanyike TALA haraka".
Je hii ni kweli,na je Kuna watu ambao wamewahi kupelekwa mahakamani na Tala?
Naombeni taarifa juu ya hilo.
 
Mikwara hio hawana uwezo huo..watu wa account wanasema wew ni bad debts
 
Back
Top Bottom