Madereva 12 wa Tanzania wazuiwa kuingia Kenya baada ya kugunduliwa kuwa na COVID-19

Madereva 12 wa Tanzania wazuiwa kuingia Kenya baada ya kugunduliwa kuwa na COVID-19

kuna kitu naogopa kuuliza.Iwapo sample ikichukuliwa MWANZA inapelekwa DAR na iwapo sample ikichukuliwa LUNGALUNGA ama TAWEETA(mgeni soma TAVETA) majibu yapo hapo hapo nani hasa yuko MAKINI na mwenye tahadhari?
 
Tumeshasema mizigo yote ije ichukuliwr mpakani na hakuna lorry wala dereva atakayeruhusiwa kuvuka mpaka, sasa mnawapima wa nini wakati hawaji Kenya?
 
Wakuu statement hii inafikirisha:

"Majirani...hiki kitu kipo, chukueni tahadhari.... tukiwaachia muingie hivi hivi mtatumalizza, lazima mpimwe kila mmoja baada ya mwingine. Hawa 12 walijaribu kuingia kupitia mpaka wa Lungalunga.
Wamepewa matokeo ya vipimo vyao na kuachiwa warudi kwao huko watajua wenyewe kama watafukiza, au waendelee kutema mbegu na kuambukiza zaidi. Lakini Kenya hawaingii wakiwa katika hiyo hali."
Hivi mgonjwa anatakiwa abaki nchi aliyopatikana na virusi au aurudishwe nchini kwake .. hata mimi sijaelewa ,
 
Hivi mgonjwa anatakiwa abaki nchi aliyopatikana na virusi au aurudishwe nchini kwake .. hata mimi sijaelewa ,

Mkuu hawa wenzetu kwa misamamo yetu yaonyesha nao imewashinda.

Akibaki kwao dawa za kufuka nyungu wala mitishamba ya ugonjwa huu hawana. Mwombeaji wa ugonjwa huu naye hawana. Sasa yaonyesha wameona isiwe taabu tukaja kulaumiana bure.

Una Corona? Basi rejea kwa Matunge Herbalist. Nadhani wako vizuri. Utawalaumu wapi hapo?
 
Back
Top Bottom