Madereva na Makondakta wa daladala kusajiliwa na serikali baada ya kuingizwa darasani na kupatiwa mafunzo ya kazi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Injinia Isack Kamwelwe amesema serikali iko mbioni kuwasajili madereva na makondakta wa daladala ili kuboresha Huduma hiyo hapa nchini.

Mh Kamwelwe amesema kabla ya kusajiliwa watendaji hao wa kwenye daladala watalazimika kupelekwa darasani na kupatiwa mafunzo maalumu.
Hii yote ni katika kuboresha Huduma ya usafiri wa abiria ambapo hata sheria ya usafiri wa bajaj na bodaboda itaboreshwa, amesisitiza waziri.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Tupambane na Corona kwanza. Inaelekea wapi nani ajuaye?
 
Safi sana...na wawafundishe kuacha bange na viroba
 
Hapo lengo ni kuwasajili ili wawe wanalipa kodi

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Hata mie nilisikia mpango wa kuwasajiri ili nao watambulike,hapo na wao kuna vitambulisho watapewa vya kuwatambua na kodi watalipa kama machinga walivyofanyiwa
 
Tuwe wazalendo. Tulipe kodi

Hapo lengo ni kuwasajili ili wawe wanalipa kodi

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧

Naam, waingie kwenye mfumo na wao walipe kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huo mpango umeshashindikana kabla hata ya kuanza...

Cha msingi Madereva wa Mabasi ya Abiria, Daladala na maroli wawe na Mikataba ya kazi/ajira ili walipe PAYE... ndio watafanikiwa.

Kule kwa wamachinga wameshashindwa ndio maana vitambulisho havitolewi Tena....
 
Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Injinia Isack Kamwelwe amesema serikali iko mbioni kuwasajili madereva na makondakta wa daladala ili kuboresha Huduma hiyo hapa nchini.

Mh Kamwelwe amesema kabla ya kusajiliwa watendaji hao wa kwenye daladala watalazimika kupelekwa darasani na kupatiwa mafunzo maalumu.
Hii yote ni katika kuboresha Huduma ya usafiri wa abiria ambapo hata sheria ya usafiri wa bajaj na bodaboda itaboreshwa, amesisitiza waziri.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Wataambiwa kulipia vitambulisho vya usajili,mapato mapato
 
Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Injinia Isack Kamwelwe amesema serikali iko mbioni kuwasajili madereva na makondakta wa daladala ili kuboresha Huduma hiyo hapa nchini.

Mh Kamwelwe amesema kabla ya kusajiliwa watendaji hao wa kwenye daladala watalazimika kupelekwa darasani na kupatiwa mafunzo maalumu.
Hii yote ni katika kuboresha Huduma ya usafiri wa abiria ambapo hata sheria ya usafiri wa bajaj na bodaboda itaboreshwa, amesisitiza waziri.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Muambieni huyo waziri wenu asiye mbunifu.
1. Aboreshe usafiri wa mwendokasi kwanza.
2. Akachukue yale mabasi yanayoendelea kuoza pale Ubungo ICD yaongeze nguvu kwenye mwendo kasi.
3. Serikali na TRA wafahamishwe kwamba yale mabasi yaliyoletwa yaliyo pale ICD hayauziki kwenye mnada hata wauze milioni ishirini.
4. Mwambieni huyo waziri maana najua haya jf haijui kwamba atamfundisha dereva wa daladala kitu gani au matusi gani asiyoyajua. UDA imekufa daladala zimeimarika wakati barabara na abiria ni walewale isitoshe kila daladala ilikua ikiilipa UDA kwa matumizi ya vituo.
Itaendelea kwani nimepata hasira sana. Daladala ndio tumpe waziri mafunzo sio waziri atupe sisi elimu.
Boresheni mwendokasi.
Itaendelea.........
 
Ukweli mtupu.
Waanze na mwendokasi kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom