Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Muambieni huyo waziri wenu asiye mbunifu.
1. Aboreshe usafiri wa mwendokasi kwanza.
2. Akachukue yale mabasi yanayoendelea kuoza pale Ubungo ICD yaongeze nguvu kwenye mwendo kasi.
3. Serikali na TRA wafahamishwe kwamba yale mabasi yaliyoletwa yaliyo pale ICD hayauziki kwenye mnada hata wauze milioni ishirini.
4. Mwambieni huyo waziri maana najua haya jf haijui kwamba atamfundisha dereva wa daladala kitu gani au matusi gani asiyoyajua. UDA imekufa daladala zimeimarika wakati barabara na abiria ni walewale isitoshe kila daladala ilikua ikiilipa UDA kwa matumizi ya vituo.
Itaendelea kwani nimepata hasira sana. Daladala ndio tumpe waziri mafunzo sio waziri atupe sisi elimu.
Boresheni mwendokasi.
Itaendelea.........
Dereva alisoma vets ndio akapewa leseni C kavu ya kubeba abiria akasome Tena masters ya udereva, au? Konda akisoma bila mmiliki kusoma shida iko palepaleWaziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Injinia Isack Kamwelwe amesema serikali iko mbioni kuwasajili madereva na makondakta wa daladala ili kuboresha Huduma hiyo hapa nchini.
Mh Kamwelwe amesema kabla ya kusajiliwa watendaji hao wa kwenye daladala watalazimika kupelekwa darasani na kupatiwa mafunzo maalumu.
Hii yote ni katika kuboresha Huduma ya usafiri wa abiria ambapo hata sheria ya usafiri wa bajaj na bodaboda itaboreshwa, amesisitiza waziri.
Source ITV habari
Maendeleo hayana vyama!