Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Awali nyumba hiyo ilidaiwa ilinunuliwa kwa gharama ya shilingi milioni 75 ambapo Julai 23, 2026 katika Ukumbi wa Mkapa ilidaiwa nyumba hiyo ya ofisi za Bajaj ilinunuliwa kwa gharama ya Sh milioni 45.
Hali hiyo hiyo imesababisha Mwenyekiti wa Bajaj, Lucas Mwakyusa kuahirisha kikao ilhali madereva Bajaj wakiamua kususia chakula kilichoandaliwa na kukimwaga wakidai kutokusomewa taarifa ya mapato na matumizi ya chama hicho kwa muda mrefu pamoja na tozo kubwa pindi wanapofanya makosa.
Muhula wa Viongozi wa Bajaj Jiji la Mbeya utatamatika mwaka huu 2026 kwa mujibu wa katiba yao ya uongozi kudumu kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu.