Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Upigaji everywhereMadereva Bajaji na wamiliki wa Bajaj Jiji la Mbeya wamesusia mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wao ndugu Lucas Mwakyusa kufuatia madai yao ya ukiukwaji wa katiba ya Chama cha Madereva Bajaj katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na kudai hati miliki ya nyumba eneo la Ofisi za Bajaj Mbeya iliyopo Soweto, Kata ya Ruanda, jana Julai 23, 2026.
Awali nyumba hiyo ilidaiwa ilinunuliwa kwa gharama ya shilingi milioni 75 ambapo Julai 23, 2026 katika Ukumbi wa Mkapa ilidaiwa nyumba hiyo ya ofisi za Bajaj ilinunuliwa kwa gharama ya Sh milioni 45.
Hali hiyo hiyo imesababisha Mwenyekiti wa Bajaj, Lucas Mwakyusa kuahirisha kikao ilhali madereva Bajaj wakiamua kususia chakula kilichoandaliwa na kukimwaga wakidai kutokusomewa taarifa ya mapato na matumizi ya chama hicho kwa muda mrefu pamoja na tozo kubwa pindi wanapofanya makosa.
Muhula wa Viongozi wa Bajaj Jiji la Mbeya utatamatika mwaka huu 2026 kwa mujibu wa katiba yao ya uongozi kudumu kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu.
Kama wamekirusha rusha kwa dhihaka huo ni ujinga lakini kama ni kwa hasira kutokana na kutokuwepo kwa uwazi taarifa za thamani ya jengo lao urushaji wa chakula utakuwa na maana kubwa sana. Kuna vyama nchi za watu viongozi wanawavalisha wanachama wao kofia na matisheti huku wakiwaimbisha nyimbo,nao wanachama wanafurahia na kushangilia kama mazuzu kumbe wenzao wamepiga pakubwa zaidi ya hizo kofia na tisheti.Sasa kumwaga chakula chini, kukirusha rusha namna hiyo, maana yake nini? 😊
Mimi nakula naondoka kumwanga chakula sio vizuri wangekula wakaondoka zao
Wanapokutana watu wenye maono na angalau umri unaofanana ukijumlisha na hasira,vituko na vibweka lazima vitokee.Sasa kumwaga chakula chini, kukirusha rusha namna hiyo, maana yake nini? 😊
Lucas Mwas....Madereva Bajaji na wamiliki wa Bajaj Jiji la Mbeya wamesusia mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wao ndugu Lucas Mwakyusa kufuatia madai yao ya ukiukwaji wa katiba ya Chama cha Madereva Bajaj katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na kudai hati miliki ya nyumba eneo la Ofisi za Bajaj Mbeya iliyopo Soweto, Kata ya Ruanda, jana Julai 23, 2026.
Awali nyumba hiyo ilidaiwa ilinunuliwa kwa gharama ya shilingi milioni 75 ambapo Julai 23, 2026 katika Ukumbi wa Mkapa ilidaiwa nyumba hiyo ya ofisi za Bajaj ilinunuliwa kwa gharama ya Sh milioni 45.
Hali hiyo hiyo imesababisha Mwenyekiti wa Bajaj, Lucas Mwakyusa kuahirisha kikao ilhali madereva Bajaj wakiamua kususia chakula kilichoandaliwa na kukimwaga wakidai kutokusomewa taarifa ya mapato na matumizi ya chama hicho kwa muda mrefu pamoja na tozo kubwa pindi wanapofanya makosa.
Muhula wa Viongozi wa Bajaj Jiji la Mbeya utatamatika mwaka huu 2026 kwa mujibu wa katiba yao ya uongozi kudumu kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu.
Yupo bize kwenye kibarua cha kuvuna maparachichi.Lucas Mwas....