Madereva wa Bodaboda: Mazuri na vituko vyao

Madereva wa Bodaboda: Mazuri na vituko vyao

samakinchanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
2,024
Reaction score
1,233
Baadhi yao wana mazuri na wengi wao wana vituko vya hatari vya kuhatarisha usalama wao na abiria wanaowabeba baadhi nimeviona vituko ni kama hivi-

1. Nimemwona akiendesha kwa kasi huku akijiangalia kivuli chake wala haangalii mbele.
2. Mmoja alikuwa kasi huku akiangalia vumbia analotimua nyuma
3.
4.
5.

Weka na vingine visa vyao hao boadaboda
 
3. Siku hizi wakipewa tu hizo bodaboda za mikataba, wanazitoa zile side mirrors (sight mirror 🙄)!! Sasa sijui huwa wanawaza nini hawa viumbe, kuendesha pikipiki bila ya hivyo vioo vya pembeni!

4. Kuweka vyuma kwenye lile bomba la kutolea moshi, halafu pikipiki inatoa mlio mkubwa kuliko! Yaani wakipita sehemu ni kero tupu!

NB: Ukiona bodaboda kanyoa kiduku, hajavaa helmet, pikipiki yake haina side mirrors, pikipiki yake ina makelele kupitiliza akivuta mafuta, na pia anapenda kuning'iniza kandambili/yeboyebo za kimguu chake cha kushoto aendeshapo hiyo bodaboda yake! Kamwe usijaribu kupanda kama una akili timamu.
 
Hawa ndio wenye fedha kwa wakati huu (reason akiharibu leo kesho zitaingia tena) ndio wachafuzi huko mtaani, lakini hali hii ni bora nani ubunifu mzuri wa JMK, Hv hawa vijana wote imagine wakose kazi hali ungekuwaje ukichunguza wengi ni vibaka lakini kwa sababu wanapata riziki uizi hawataki kusikia lakini ukijipindua wanakupiga tu.
 
Hawana ubinadamu hao vijana.Unakosea kumpa hela,kwa mfano anadai "harufu moja",unampa elfu kumi ukidhani ni elfu mbili,yeye anakurudishia elfu moja.Hakustui.Noma ajabu!
 
Kuna Hawa bodaboda vishandu...
Utamkuta kavaa vindala, T-shirt kubwa na kipensi Cha jinsi kina nyuzi nyuzi...akikaa bega moja linainamia upande mmoja...ana virasta flani hivi kasokotwa na demu wake...ha bargain sana bei...yeye hata ikipungua buku anakupeleka...
Mwendo wao ni Wakasi hata kama anaenda Safari ya mita 100...
Wanakesha karibia kila siku...Wana mageto wanakaa wawili au yupo kwao...
Hawa kama wapo mtaani kwako ishi nao kwa akili...ukiwa na jambo waulize wao na uwaheshimu sana wanaweza kuwa waume wenzio au wakwe zako
 
3. Siku hizi wakipewa tu hizo bodaboda za mikataba, wanazitoa zile side mirrors (sight mirror 🙄)!! Sasa sijui huwa wanawaza nini hawa viumbe, kuendesha pikipiki bila ya hivyo vioo vya pembeni!

4. Kuweka vyuma kwenye lile bomba la kutolea moshi, halafu pikipiki inatoa mlio mkubwa kuliko! Yaani wakipita sehemu ni kero tupu!

NB: Ukiona bodaboda kanyoa kiduku, hajavaa helmet, pikipiki yake haina side mirrors, pikipiki yake ina makelele kupitiliza akivuta mafuta, na pia anapenda kuning'iniza kandambili/yeboyebo za kimguu chake cha kushoto aendeshapo hiyo bodaboda yake! Kamwe usijaribu kupanda kama una akili timamu.
kama hili la kutoa mlio wa kupasuka kama bomu au risasi inaudhi sana na usalama barabarani wanaliona hilo kabisa
 
Hawa jamaa Wana roho ngumu Sana

Nimeshawaona wanawekeana dau la buku tano (5,000) kisha wanabishana Nani anaweza ingia barabara kubwa Bila kuangalia kama gari inakuja au laa!

Yaani hawa jamaa Wana moyo mgumu Sana, Putin akijasahau na kuja kuvamia huku bongo,hawa Boda boda ndio wakae mstari wa mbele vitani!
 
Ukipata ajali kwenye boda uwezekano wa kufa au kuvunjika ni mkubwa, binafsi sizipendi. Mpaka leo sitaki hata kujifunza kuendesha.
 
maeneo kama hakuna gari au kwa kuwa unaishoi mjini
Nipo bush huku, hapa navyoongea wiki iliyopita tumezika kijana wa miaka 20 na kuna mtoto kagongwa kavunjika miguu huyo boda mbavu zimevunjika,

Kiukweli pikipiki ni shida tu.
 
Back
Top Bottom