Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Wengi tunazijua gari zinazotumika kwenye mashindano ya FIA, especially ya Formula 1. Magari na team kama Ferrari, Mercedes Benz, nk yanaonesha uwezo wao.
Vile vile madereva wa hayo magari, kama Lewis Hamilton, Max Verstappen nk wakionesha ubabe nyuma ya steering.
Ukichukulia poa, utasema vile ni vigari tu vya kawaida. Ila hapana aisee. Na ukichukulia poa zaidi, utasema ata mimi wakinifundisha kuendesha ile gari, ndani ya week naweza kuendesha kwa speed kali. Hapana kwa kweli.
Tukumbuke, kama ilivyo FIFA na Football, basi FIA (Fédération Internationale de l'Automobile) wao wanasimamia sheria na taratibu zoote za aya mashindano kuanzia viwanja, magari, constructors (team) na madereva.
Tuanze na race yenyewe:
Hii ndio fastest racing cars duniani. Kila weekend magari 20 yakiwa na team 10 (kila team inatoa magari 2) yanashindana, na mwishoni washindi 10 wa mwazo wanapewa points, namba moja akipata 25 points, wa pili 18, watatu 15 ivyo ivyo zinashuka hadi wa 10 anapata 1. Izo point unakua unazikusanya kila mechi (kama Ligi kuu ya Mpira) na mwisho wa msimu mshindi ni mwenye point nyingi.
Mfano, hadi leo May 2024, msimamo wa F1 kwa upande wa madereva ni huu hapa chini:
Na msimamo wa F1 kwa upande wa team (constructors) huu hapa:
Kuna makombe mawili kwa pamoja yanatolewa kila msimu. La kwanza la Dereva na la pili la Constructor (team). Kwahiyo dereva wa team Ferrari mfano akishinda, anapata point zake. Ila kampuni linapata point kutoka kwa madereva wote wawili.
Hadi leo L Hamilton na M Schumacher ndio wanaongoza kwa kushinda makombe ya dunia mengi zaidi (7). Ila debate bado ni kali kua nani ni dereva mkali wa wote katik F1 history. Wengi wanaamini ni Hamilton, kwakua anasupportiwa na statistics. Na ndio ilipelekewa apewe official cheo cha SIR.
Hii racing inafanyika siku tatu, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Ijumaa ni siku ya Practice. Hapa dereva anaujua uwanja kujua corners challenge etc.
Jumamosi kutengeneza Grid. Yes. Kama unavyoonaga mnavyoanza anakua yupo wa kwanza wa pili hadi wa 20. Inaitwa Grid. Hii inatengenezwa siku ya jumamosi, mnashindana aliefast ndio atakaa mbele. Ila mnavyoshindana kila mtu anarace against time sio against rival driver.
Jumapili ndio race yenyewe. Mnajipanga kwenye formation (grid), then Green light, then off we go.
Zaidi ya nchi 34 zimewahi host F1 race, kwa Africa ni South Africa tu miaka ya 90 aliwahi host. Kuna uwezekano Zanzibar, Kenya, Rwanda waka host miaka ya karibuni.
Kuangalia hii race ya siku tatu sio bei ndogo, ni kubwa. Bei zinatofautiana kutokana na jukwaa na aina ya race, China GP ikiwa ndio cheapest kwa $200 kwa weekend nzima.
Gari lenyewe:
Gari la F1 ni la siti moja lenye open cockpit na open wheels, likiwa na injini nyuma na aerodynamics wings kwote mbele na nyuma. Haya magari yako fast na very powerful.
Baadhi ya sifa inayoyafanya magari ya F1 yawe special ni:
Aerodynamics ndio kila kitu kwenye aya magari. Yana wings za kutosha zinazopeleka downward force hadi ya 750kg katika speed ya 160km/h.
Sasa ukichukulia uzito wake na downward force inayotengeneza, F1 inaweza kuemdeshwa juu ya celling bora nyumba yako (T&C zitahusika).
Uzito haya magari sio mazito. Uzito unapimwa kwa gari n dereva akiwemo.
Haya magari hayana engine displacement kubwa. Mfano, kwa mwaka 2024 wanatumia 1.6L V6 Hybrid engine. Ila engine zao zinatoa power kubwa knm, mfano Redbull RB 17 engine inatoa 1200+ hp.
Hizi chuma zina accerelation kubwa sana. On average zinaweza kutoka 0-100km/h ndani ya 2.4 sec.
Breki zake ni hatari. Mfano ikiwa kwenye speed ya 200km/h inaweza kupiga breki hadi ikasimama ndani ya sekunde 3 tu, ikiwa inecover urefu wa 65 mita.
Hii braking inapelekea diski kupata joto hadi la 1000°C.
Ingawa ni Manual transmission, ila miguuni ina pedal 2 tu. Breki na Accerelation. Clutch ipo kwenye paddle shifters.
Maximum speed ya F1 kwenye straight line ni 370+ km/h. Ila kwakua kuna kona nyingi, mara nyingi speed ya kawaida inakuaga 150-250km/h. Magari yanauwezo wa kukata kona hadi kwenye speed kali, ila Monaco wana kona kali ambayo dereva aliewahi kupita kwenye iyo kona kwa speed kali alikua na 48km/h tu.
Engine ya Corolla inaweza kudumu hadi kilometa 500,000 ila Engine ya F1 inadumu kilometa 1,500 hadi 2,000 tu. Kwahiyo baada ya race kadhaa wanabadirisha engine.
Hii gari ni gharama sana. Inakadiriwa kua na bei ya $12-18 Million. Steering wheel tu peke yake inazidi $50,000 na engine ndio inafika hadi $8 Million.
Tyre za F1 zinatengenezwa na kampuni moja ya Pirreli. Kuna tyre za aina nne, hard, medium, soft na wet. Soft tyres ndio zipo fast ila tatizo zinaisha haraka kwahiyo utakua unaenda kubadirisha mara kwa mara, na kubadirisha means unapoteza muda.
Weekend nzima unapewa set 13 ya tyres utakazo zitumia kwenye practice, grid na race.
Tukirudi kwenye issue ya kubadirisha tyre, kuna team ya watu zaidi ya 20 ambao wanabadirisha tyre zote nne kwa chini ya sekunde 3 kushuka chini.
Dereva
Madereva wa F1 lazima wawe na nguvu za kutosha, stamina na focus saaaaana.
Huu ni mchezo pekee ambao una mixed gender (kama nimekosea sorry). Kwamba anaweza akaendesha mwanamke au mwanaume. Yaani hakuna F1 for men na F1 for women. Ingawa wanawake sio mara kwa mara tunawaona kwenye mashindano, ni wanawake watano (5) tu ndio waliowahi kushiriki kwenye GP. Sijajumlisha test drivers.
Dereva anaweza kuresist G-force hadi ya 7G wakati wa kukata kona.
Pilots wa jet wamekua trained kuresist hadi 9G. Hii G force inatengezwa pale wakati gari ina ongeza au kupunguza mwendo (Accerelation au deaccerelation).
Kwa lugha nyepesi, gari inavyoondoka unahisi kama kuna nguvu inakuvuta kwa nyuma, iyo ndio G Force. Kwahiyo 1G ni kama ukiwa tu umelalia mgongo kwenye kitanda au gari likiwa linaondoka kwa 10m/s². Likienda 20m/s² una experience 2G na kuendelea.
Nashindwa kukueleza vizuri, lakini angalia effect ya G force katika headrest ya gari la Oliver hapa chini.
Sisi wa kawaida tunaweza ishia 4-5G kwa sekunde chache sana. Ikizidi izo sekunde au Gs tunaweza zimia.
Kuna sheria ya uzito. Ukiwa umevaa suti full na helmet angalau uwe na uzito wa 80kg, ila urefu na ufupi ni nyinyi na team yako.
Madereva wa F1 wanaandaliwa tokea utotoni. Wanaanza Kart racing wakiwa watoto kabisa.
Mfano L. Hamilton alianza kart racing akiwa na miaka 8 tu. Na akiwa 10 alishinda British Kart Championship.
Pia Russell na Verstappen wameanza tokea watoto sana.
Mbali na mazoezi ya mwili na mind, wanapractise kwenye simulators ambazo ni copy ya race kabisa. Hii inasaidia dereva ajue gari na barabara.
Dereva akirace full race mfano kwenye GP ya Monaco, uwanja wake una urefu wa 3.3 km na mnafanya complete 78 laps, kwahiyo roughly mtakua mmecover distance ya 260km (kama umbali wa Bagamoyo to Tanga) na Charles Lecrec alitumia masaa 2 na dk 24 kukamilisha race, na huku Lewis Hamilton akiongoza kwa fastest lap kwa kutumia dk 1 na sec 14 kukamilisha mzunguko mmoja (wa izo km 3.3).
Huu uwanja wa Monaco, izo namba ni kona.
Kwenye F1 haukai kwa starehe, unakaa kibabe sana.
Unakaa ivyo kwa takribani masaa 2, na inabidi uwe unanyanyua shingo ili uone mbele.
Dereva anapoteza hadi kilo 2 hadi 3 za uzito akikamilisha race moja. Hii inatokana na excessive sweating.
Gari ina AC ila kwakua ni open cockpit, AC haina ubaridi sana. Na ukichangia joto la battery na engine iliopo mgongoni kwako, unaiva.
Mfano mwingine kwenye race ya Qatar 2023, joto lilikua 36°C kwenye uwanja, na ndani ya gari ilikua 56°C. Ilipelekea madereva kadhaa kutomaliza race na mwingine kutapika huku ana race.
Kwakua ligi za mpira zimeisha, ebu jaribu kufuatilia F1. Utapenda.