Sorry kuna kitu mtu kuniuliza, kuhusu zawadi ya mshindi.
Tulisema kuna makombe mawili, ya dereva na team.
Dereva akishinda hapewi hela na FIA, ila tunaamini anapewa bonus kwenye mishahara yake na marupurupu. Naamini hii ni kama kwenye football, team ikichukua ubingwa sio hela ya mchezaji mmoja mmoja ni ya club.
Team (constructors) ikichukua ubingwa ndio wanapata pesa ndefu sana. Mfano, Redbull mwaka 2023 walipata $140 Million.
Hii inamaanisha kwamba F1 ni ushindi wa team, sio wa dereva. Ndio maana ukisikiliza interview ya madereva baada ya race wanaongeleaga "we" wanajua mchango wa kila teammate ata wa kubadirisha tyre.