KERO Madereva wa Taksi Mtandao wananyonywa sana na Makato, wakilalamika wanaonekana wajeuri

KERO Madereva wa Taksi Mtandao wananyonywa sana na Makato, wakilalamika wanaonekana wajeuri

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Jaman hebu tazameni katika suala la taksi Mtandaoni hasa huduma ya Bolt.

Madereva wanalia 😢 sana kisa commission zao, na ni kweli ni kandamizi sana, 25% ya nauli kweli 😢 kwa mfano safari ya Sh 10,000 Bolt wanakata takribani Sh 2,500 inabaki 7,500.

Hapo hutoa pesa ya mafuta kwa hiyo safari ambayo ni zaidi ya Sh 4,000 inabaki Sh 3,500, je ni sahihi?

Hapohapo dereva lazima chombo chake akilipie;
1. Mapato (TRA)
2. LATRA
3. Bima
4. Service kwa kila wakati
5. Muda (mvua & jua) vyote vyake

Je, ndio huduma ambayo mnataka iwe kwenye jamii kwa ukandamizaji huu?
 
Back
Top Bottom