Mmoja alishanifanyia hilo suala la kupaki nyuma yangu halafu akaambiwa na wahudumu kutoa gari yake akasema hii nchi ni huru kila mtu anapaki anapoamua na atatoa muda atakapojisikia(sijui hayo maneno aliyaongea kwanini),tulikua washkaji watatu kila mtu na ka usafiri kake na watu wako maji tayari,hapo maamuzi lazima yawe ya tofauti.
Mshkaji mmoja akatoa wazo tukalipitisha,akasema tupande gari yake then gari ya mshkaji mwingine ipaki nyuma ya hio Altezza then tuiache hapo hata kwa siku 2 afu yeye atatupeleka home,tukaona hii iko vzr.
Jamaa akapaki Gari yake hapo tukasepa zetu ilikua ijumaa na uzuri mwenye bar ni homeboy wetu,so nilimjulisha akasema huyo dogo mwenye hio Altezza hua anazingua wateja kwa hio nyie mshughulikieni tu mtakavyoona.
Ile gari tuliiacha hapo kuanzia ijumaa mpk j5,nikawa mtaani nazugia na ka rav 4 old model fresh tu,yule dogo mwenye Altezza alihaha kinyama kunitafuta kuanzia hio Ijumaa mpk J5 alitutafuta mpk kutishia kuleta breakdown nikamwambia we itoe tu hio gari ya mwana na mkiinyanyua vibaya ikaharibika chochote kile ndipo utajua haujui.,chalii akaogopa.
Mwishowe braza ake ndio alikuja kuomba yaishe na tukatoa ile gari hapo nyuma ilipoblock na mwenye bar anasema baada ya tukio hilo dogo alibadilika kabisa.