Ila wengi wao wana tabia zote mdau alizozitaja...
Nitatoa mfano halisi kilichotokea mwezi uliopita..
Tumeenda sehemu nikapaki usafiri wangu kama wengine walivyopaki kufuatana na maelekezo ya mlinzi wa pale..tuakaendelea na kilichotupeleka hapo..
Wakati naondoka nikakuta Alteza imepaki vibaya, sikuwezi kutoka..nikawaomba wahudumu wamwambie jamaa asogeze gari...mhudumu akarudisha jibu jamaa hajigusi wala hajibu kitu...
Meneja wa sehemu hiyo akaenda mwenye, kakanyanyuka kajamaa kamenyoa kiduku, mezani kameweka K vanti, suruali mnyonyo...kanavyotembea sasa nikadhani anakuja kuwasha Range Rover sport ya 2019.
Akawasha Alteza yake, akapiga resi kile kibuyu pale nyuma kikaharibu usikivu, basi akaipaki pembeni.....nikaondoka zangu..
Hawa watoto wakishaendesha hizo gari, wakazifunga vibuyu kwenye exhaust, wanahisi wameshamaliza maisha yote.