Safi sana, pima wote wanaong'ang'ania kuingia Kenya, ingekua hawa Watanzania ndio wanapima Wakenya na kugundua wengi kiasi hiki sasa hivi wangekua wanalialia eti Kenya ina ajenda ya kuwaambukiza, yaani juzi waligunduliwa 78 wote kwa siku moja, leo 51 yaani wanataka kuja mamia yao wakiwa na kirusi, kama vipi maafisa waongezwe kwenye huo mpaka, hawa watatumaliza.
Niliskliza hotuba ya mkulu wao nikachoka, eti anadai dereva hana haja ya kupimwa kisa kaendesha lori mwenyewe kilomita zaidi ya 1,000. Ukweli rais Magufuli kuna mambo anafanya mazuri ila kuna maneno humtoka mpaka unasshindwa kweli kama alihudhuria darasa hata moja la sayansi, au labda ana washauri wabovu sana kuwahi kutokea.
Wataalam wameeleza jinsi hiki kirusi kinaambukiza na kusambaa, uwezekano upo mkubwa kwa dereva kuendesha lori kilomita zote hizo bila kugundua, maana kawaida wengi husafiri kama siku nne au tano, ila kirusi hadi kijitokeze vizuri kinahitaji siku kama kumi hivi, sasa mheshimiwa rais anataka mamia ya madereva wake walioathirika waachiwe waingie kwenye mataifa majirani kisa wamejiendeshea malori wenyewe.
Hotuba zake zimejaa kejeli dhidi ya mataifa ambayo yamechukua hatua za tahadhari, halafu watu wanahoji kwanini Tanzania inatengwa na SADC na EAC, maana hivi kwa kweli wakikutana marais wote wanajadili mikakati halaafu mmoja wao hana mikakati zaidi ya kukejeli wenzake, ni dhahiri hawataendana, hapa inabidi Watanzania wafungiwe wabaki huk huko kwao watajuana wenyewe, wakujifia atajifia na wa kupona atapona. Yeyote kati yao anayetaka kuvuka mpaka apimwe tena sana na kuhakikisha yuko salama, au raia yeyote anayetokea Tanzania hata iwe mtalii, mzungu, Mchina wote wapimwe mara mbili mbili na hata ikitokea hawana, zchukuliwe namba zao za simu na wenyeji wao, na wapi wanakwenda, wafuatiliwe huko hadi ziishe siku 14.