Madhara ya bunge kujaa WanaCCM yameonekana

Madhara ya bunge kujaa WanaCCM yameonekana

Hata wapinzani wangekuwepo si wangegoma tu na kutoka nje halafu tozo zingepitishwa kwa sauti ya ndioooo !
 
Cha ajabu Mkuu maamuzi ya kuwafukuza wale COVID-19 mjengoni hataki kuyagusa!!! Maccm walidai kwamba Samia hawezi kuliingilia Bunge!!! Bunge FEKI wapuuzi wanagonga gonga meza na kupiga ukelele ndiyoooooo huku kukiwa hakuna la maana lolote walilolifanya.

Kabisa mkuu. Angalia hivi Sasa eti mtu mmoja tu (rais) anatamka kutengua maamuzi ya bunge lililokaa kwa miezi 3 na posho wamelipwa. Sasa kama rais anafuta maamuzi ya bunge, uwakilishi wa wabunge kwa wananchi uko wapi?
 
Ni shida kujadili hoja kwa undani kwa kuonyesha 'cons and pros' na kufikia uamuzi on the basis of weight of evidence and deliberation.
 
Tena hao wapuuzi wakisaidiana na Zitto walifuta fao la kujitoa,na bado Jaffo alivyoleta hoja binafsi sheria ifungwe,Ziito na Mchungaji Msigwa wakiwa wamehongwa na NSSF wakaipigia debe sheria ibaki kama ilivyopitishwa na bunge kwamba fao la kujitoa lifutwe
 
Madhara ya bunge
(a) Kujaa wanaccm,
(b) Kuwa chombo cha kuimba nyimbo za sifa badala ya chombo cha kuisimamia na kuikosoa serikali,
.....yamedhihirika katika sakata la tozo za miamala. Rais anaanza SSH ameanza kupata tabu.

Wakati wa vikao vya bunge kujadili bajeti 2021/2022, wabunge wengi walijikita kutoa sifa kwa rais badala ya kuangalia mijadala iliyopo mezani na kuichambua ipasavyo.

Sasa mama SSH amelazimika kuagiza tozo hizo ziangaliwe upya wakati kulikuwa na zaidi ya watu 365 waliolipwa posho nene kufanya kazi hiyo.

Ndugai ameboronga, tena amebutua ajitafakari ktk hili kisha ajiuzulu.
.
Kwani Bunge linahusika na kutunga kanuni zenye viwango vya tozo,? Au ni waziri tusichanganye mambo.
 
Yaani hili bunge la ndugai yamejaaa mabogus tupu,mda wa kujadili bajeti yenyewe yanaimba mapambio,mwisho wa siku mambo ndo hayo, hao hao mabogus ndo washauri na mawaziri wa raisi,bajeti imepita bungeni raisi naye kwa sababu kazungukwa na mabogus kapitisha tu yaani hatuna pa kutokea
 
Huyu hapa

IMG-20210718-WA0139.jpg
 
Kwani Bunge linahusika na kutunga kanuni zenye viwango vya tozo,? Au ni waziri tusichanganye mambo.
Tozo zimejadiliwa bungeni. Kama walipendekeza tozo bila kujadili viwango ni Udhaifu mwingine huu
 
Madhara ya bunge
(a) Kujaa wanaccm,
(b) Kuwa chombo cha kuimba nyimbo za sifa badala ya chombo cha kuisimamia na kuikosoa serikali,
.....yamedhihirika katika sakata la tozo za miamala. Rais anaanza SSH ameanza kupata tabu.

Wakati wa vikao vya bunge kujadili bajeti 2021/2022, wabunge wengi walijikita kutoa sifa kwa rais badala ya kuangalia mijadala iliyopo mezani na kuichambua ipasavyo.

Sasa mama SSH amelazimika kuagiza tozo hizo ziangaliwe upya wakati kulikuwa na zaidi ya watu 365 waliolipwa posho nene kufanya kazi hiyo.

Ndugai ameboronga, tena amebutua ajitafakari ktk hili kisha ajiuzulu.
.
Magufuli alituharibia sana nchi yetu
 
Back
Top Bottom