Madhara ya bunge kujaa WanaCCM yameonekana

Madhara ya bunge kujaa WanaCCM yameonekana

Ila kweli Hawa wabunge mbona kama wapo wapo tu, Kuna shida mahali! ni lazima watanzania tutafute suluhu, hatuwezi kuwa na Bunge la namna hii ambalo bila shaka LINADEMKA kwa hakika.
Kilaza kama babu Tale unategemea aseme nini zaidi ya kukenua kenua na kugonga meza
 
Madhara ya bunge
(a) Kujaa wanaccm,
(b) Kuwa chombo cha kuimba nyimbo za sifa badala ya chombo cha kuisimamia na kuikosoa serikali,
.....yamedhihirika katika sakata la tozo za miamala. Rais anaanza SSH ameanza kupata tabu.

Wakati wa vikao vya bunge kujadili bajeti 2021/2022, wabunge wengi walijikita kutoa sifa kwa rais badala ya kuangalia mijadala iliyopo mezani na kuichambua ipasavyo.

Sasa Rais Samia amelazimika kuagiza tozo hizo ziangaliwe upya wakati kulikuwa na zaidi ya watu 365 waliolipwa posho nene kufanya kazi hiyo.

Ndugai ameboronga, tena amebutua ajitafakari ktk hili kisha ajiuzulu.
.
Tunapaswa kudai katiba mpya kwa nguvu zaidi la sivyo mambo yetu yatakuwa mabaya zaidi.
 
Madhara ya bunge
(a) Kujaa wanaccm,
(b) Kuwa chombo cha kuimba nyimbo za sifa badala ya chombo cha kuisimamia na kuikosoa serikali,
.....yamedhihirika katika sakata la tozo za miamala. Rais anaanza SSH ameanza kupata tabu.

Wakati wa vikao vya bunge kujadili bajeti 2021/2022, wabunge wengi walijikita kutoa sifa kwa rais badala ya kuangalia mijadala iliyopo mezani na kuichambua ipasavyo.

Sasa Rais Samia amelazimika kuagiza tozo hizo ziangaliwe upya wakati kulikuwa na zaidi ya watu 365 waliolipwa posho nene kufanya kazi hiyo.

Ndugai ameboronga, tena amebutua ajitafakari ktk hili kisha ajiuzulu.
.
Watanzania HAMKENI BANAA hakuna mtu kwa kujiuzuru kwa hiari yake. Tuungane BUNGE livunjwe au serikali iwajibike basii.

Nani ajiuzuru aache mshahara wa 22M monthly!!
 
a) Kujaa wanaccm,
(b) Kuwa chombo cha kuimba nyimbo za sifa badala ya chombo cha kuisimamia na kuikosoa serikali,
.....yamedhihirika katika sakata la tozo za miamala. Rais anaanza SSH ameanza kupata tabu.
Na hili ndio linatu-cost, wabunge hawa wa ccm kwanza sio watu wa kusoma makabrasha zaidi ya upigaji kelele za ndiooooooooo.
Ndio maana limekuwa ni bunge dhaifu na lisilo na faida kwa mwananchi wa kawaida.
 
Twambie kipindi kina Lisu wamejazana bungeni waliwahi kuzuia nini kisipitishwe?
Ila waliongea na wananchi waliwasikia na bunge lilikuwa na mvuto wakusikiliza hoja kiuchambuzi.
Siku hizi mbunge Mama kipenzi chetu,mama atatuvusha sijui mini ovyoovyo.Haya Leo mama eti msikivu kwenye tozo.Yeye ndio alikuwa anajadili bungeni.
 
Twambie kipindi kina Lisu wamejazana bungeni waliwahi kuzuia nini kisipitishwe?
aibuuuuuuuuuu, sasa mnaanza kujilaumu wenyewe. kumbuka kina lissu hawapo bungeni bwashee, huu msala ni wa sisiemu. madhara ya bunge la chama kimoja yameonekana live
 
Halafu Shaka anasema CCM wanalifuatilia. Na ni bunge lao
Huyo shaka nadhani kichwani kumeyumba.

Wabunge wa CCM ni wajumbe wa kamati ya CCM ya Bunge, na kwa sasa hata wakiwa Bungeni wanaendesha vikao vyao kama vikao vya CCM. Sasa hiyo CCM inayofuatilia ni CCM ya wapi?
 
Twambie kipindi kina Lisu wamejazana bungeni waliwahi kuzuia nini kisipitishwe?
Mwulize Spika Msataafu Anne Makinda atakuambia.

Katika hitimishonlake Anne Makinda alisema, Mh. Tundu Lisu alikisaidia sana Bunge. Maana kuna wakati Serikali ilikuwa inaleta mambo yaliyofichwafichwa kishetia, ni Tundu Lisu ndiye aliyekuwa anatufungua macho". Unaelewa maana ya hiyo sentensi?
 
Huyo shaka nadhani kichwani kumeyumba.

Wabunge wa CCM ni wajumbe wa kamati ya CCM ya Bunge, na kwa sasa hata wakiwa Bungeni wanaendesha vikao vyao kama vikao vya CCM. Sasa hiyo CCM inayofuatilia ni CCM ya wapi?
Ni lini chama kitaielekeza serikali,kufuata sheria na katiba ya taifa hili?Akiuliza swali la nyoongeza mbuge wa kujitegemea wa wananchi.
 
Haya ni madhara ya nchi kutokuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Ukiwauliza waliupataje huo Ubunge kuna baadhi yao hata hawafahamu jinsi walivyoshindishwa.
Jiulize kwa hoja IPI wagombea wa CCM washinde Uchaguzi Tanzania nzima?Pamoja na madhila yote tuliyopitishwa kwa miaka 5+ ya awamu ya 5!
Tunajidanganya wenyewe na kujishangilia.Hii inatufanya kama mazuzu.
Tunataka Katiba ya Wananchi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Baadaye utasikia anaupiga mwingi sana sijui nini , nchi imebakwa sana hii na kulawitiwa
 
Back
Top Bottom