Madhara ya kufeli kwa bajeti ya Mwigulu tutayaona kwenye deni la Taifa

Madhara ya kufeli kwa bajeti ya Mwigulu tutayaona kwenye deni la Taifa

Na ndio itavokuwa hivo.. kwa hiyo volume ya miamala itapungua na kuathiri hata zile income za makampuni ya simu.

Na hii ndo inakuambia kwamba bei ya kitu haistahimiliki.. na usitegee watu watakuja kuzoea hizi tozo .haiwezi kuwa kirahisi kiasi hicho
Serikali nyingi hutengeneza sheria, kanuni, miongozo na tozo (interest rate) ili kuongoza bishara bila kushirikisha wafanyabiashara (wananchi) matokea yake huwa havifanikiwi nimeandika hivi kwenye kitabu changu cha ujasiriamali nanukuu:Governments,local government and urban authorities might or spend a lot of money and time to establish many rules, regulations and rate-setting to guide business, in the final analysis prove to be ineffective and unnecessary, considering that, business are not integral to the establishment of these .......
 
Mimi pengine nahisi kila wizara iajiri Waziri ambae ni msomi wa fani husika ; kama ni sheria then mwanasheria ndio awe waziri, kama ni uchumii kuwe na mchumi,Mwigulu kupitisha bajeti iliyoandaliwa na Mpango ni dhahiri hakujua afanye nini na hio bajeti,utaona mapungufu au ku critique kitu hauko familiar nacho ??
Mwigulu mwenyewe anasema yeye ni 'Daktari wa Uchumi'... nadhani wanachokosea haswa hao wanaowachagua, huwa wanaangalia vywti hawaangalii competence ya mtu.. mtu kama Mwigulu inawezekana amesoma ila bado hafahamu vyema haya masuala ya kiuchumi mbali na kusema yeye ni Daktari wa uchumi, ila ni mweupe sana... ni kwenye hizi tozo amethibitisha hilo
 
Serikali hutengeneza sheria na kanuni na miongeza na tozo (interest rate) ili kuongoza bishara bila kushirikisha wafanyabiashara (wananchi) matokea yake huwa havifanikiwi nimendika hivi kwenye kitabu chaungu cha ujasairiamali nanukuu:Governments,local government and urban authorities might or spend a lot of money and time to establish many rules,regulation and rate-setting to guide business in the final analysis prove to ineffective and unnecessary
Kabisa mkuu, nadhani kabla ya kuja na hivi vitu wangepaswa kwanza kufanya utafiti kuanzia chini halafu ndo waje na proposal zao, ila hichi kitu naona hakifanyiki hapa Tanzania, ni kama vile maamuzi yote ya bajeti yanaamuliwa juu.

Hongera sana pia kwa Kitabu... Nawezaje kukipata kama hutojali
 
Bajeti ya Mwigulu imeshaonesha kwamba haitakuwa na matokeo mazuri kwenye uchumi. Hisia za kodi kuwa kubwa tena kwenye bidhaa muhimu ni dhahiri.

Kwenye uchumi, kuna kitu tunakiita 'Equillibrium Price' - yaani ile bei ambayo mnunuzi na muuzaji wataafikiana. Sasa kuna baadhi ya bidhaa ambazo kulingana na kupanda kwa bei, imesababisha 'price equillibrium' imepotea kabisa.

Maana yake ni kwamba bei mpya baada ya kodi na tozo, imesababisha wanunuzi kutokuhisi uhalali wa kununua kwa bei mpya. Mfano mdogo tu, mimi nilikuwa namiliki line mbili za simu, ila tangu tarehe moja, ni kama line moja nimeitelekeza na sijafanya muamala wowote wa kutuma wala kutoa pesa kwa wakala, kwasababu, akili yangu inaniambia hii bei ya sasa ni kubwa mno kulinganisha na huduma ninayopata.

Matokeo yake ni nini sasa?
Muitikio ukiwa mdogo kwa walaji, itakuwa ngumu sana kwa Mwigulu kuweza kukusanya kiasi ambacho amakitegemea. Kumbuka serikali ime target zaidi ya Tzs 1.5 Trillioni itoke kwenye miamala ya simu na tozo.

Sasa kwa upepo ulivo, sidhani kama hata nusu ya hii itapatikana. So maana yake, bajeti ya Mwigulu mpaka sasa ina shimo la karibu zaidi ya Tzs 1 Trillioni ambayo ili liweze kujazwa, itabidi serikali ikope, maana kumbuka kuna miradi ya SGR na Bwawa la umeme bado inahitaji pesa.

Ni kama kusema, tayari nakisi ya bejeti yetu tayari ipo kubwa zaidi ya walivoitabiri, kwasababu kuna kodi na tozo hazitaweza kukusanywa kama hii ya miamala ya simu.

Ama kwa kweli Mwigulu amefeli sana, tena sana.. Anasema eti hizi tozo zitatumika kuunda mfuko wa kizalendo, ila ni uwongo kwa sababu huwezi kuwa na mfuko wa kizalendo wakati bajeti yako siku zote ipo kwenye nakisi.

Ni kama kusema eti mtu uweke akiba ya mtoto kwenda shule wakati unadaiwa kodi ya nyumba.. Ni kitu hakiwezekani ni kuwadanganya tu watu, maana ameshabugi.

Kama inawezekana kurudia bajeti, nashauri Mwigulu afanye hivo mapema, la sivo.. naona deni la taifa likiendelea kupaa just kwa mtu kushindwa kufanya kazi yake vema.
Mimi leo nimefuta laini nne: 2 za airtel, 1 ya voda na 1 ya halotel. Bado najishauri kati ya voda na tigo zilizobakia, nifute ipi. Suala la miamala ndiyo kabisa watanisamehe maana itatumia benki kama zamani.
 
Unajua mtu ulikuwa unapata incentive ya kutumia ma line mengi kwa sababu ya urahisi, sasa walivominya, lazima watu tubaki na line moja tu ya kuweka LUKU
 
Unajua mtu ulikuwa unapata incentive ya kutumia ma line mengi kwa sababu ya urahisi, sasa walivominya, lazima watu tubaki na line moja tu ya kuweka LUKU
Kama walipiga mahesabu ya kutukamua matrilioni , watajuta maana ni mwendo wa kuacha kutumia mitandao kufanya miamala. Makampuni ya simu nayo yalipangwa maana naona nayo yataadhirika vibaya sana
 
Ni kama kusema eti mtu uweke akiba ya mtoto kwenda shule wakati unadaiwa kodi ya nyumba.. Ni kitu hakiwezekani ni kuwadanganya tu watu, maana ameshabugi.
Awamu iliyopita fedha za kujenga hii miradi zilikuwa zinatoka wapi!?
 
Mwigulu atakuwa waziri wa fedha mbovu zaidi kuwahi kutokea nchini,unarundikaje kodi kwenye miamala ya simu wakati tayari wamilikaji wa mitandao hiyo wanalipa kodi kwa ajili ya kazi hiyo.

Hakuna mwananchi mpumbavu atakayekubali kutunza pesa zake kwenye mitandao, wakati anajua siku ya kutoa lazima atakatwa kodi ya kufa mtu tofauti na makato ya kawaida yaliyowekwa na mitandao pia huku ni kuwaharibia wenye mitandao biashara.
 
Awamu iliyopita fedha za kujenga hii miradi zilikuwa zinatoka wapi!?
Akaunti zote za matajiri ziliwekwa chini ya ulinzi maalumu kikikutwa kibunda kikubwa kinakwapuliwa kinapelekwa kwenye miradi mikubwa, kodi ya mapato ilikuwa inakusanywa kwa nguvu chini ya mtutu wa bunduki, ukibisha kesi ya uhujumu uchumi isiyo kuwa na dhamana inakuhusu hivyo inabidi ukubali kutoa kiunyonge.
 
Ila mwingulu ana nyota mbaya ya kutopendwa hi bajeti sio yake aliikuta imeshaandaliwa na Mpango, na imepitishwa na Bunge baada Raisi kulidhia nayo. Ila sasa mslaba wote kaubeba yeye......sema tu nalyeshewe lina upumbavu fulani kujipendekeza na unafiki paka litimuliwe ndo lipate akiri unasapoti je tozo kubwa la miamala kama hilo jinga kabisa
Mwigulu hakuwa smart hata kidogo kwanini hakuirekebisha kutoa hayo mapungufu hapo wangeongeza hata jero tusingeshutka na Kodi ingekuwa nyingi kuliko Sasa watu tumegoma acha tu akakope huko nje kufidia. I think Sasa waziri wa mipango wamweke hata mango mwenye genge ni mzoefu kuliko hawa wasomi madesa Hadi PhD huku practibility Yao kwenye field ni zero experience kabisa. Dah Mwigulu kaniangusha Sana aisee, Mimi sio mchumi ila kwa akili ya kuvukia barabara najua something was wrong kwenye hyo budget na ukichangia Sasa tuna bunge la kinyumbu na watu wasio fikiria basi ni hasara kwa taifa
 
Bajeti ya Mwigulu imeshaonesha kwamba haitakuwa na matokeo mazuri kwenye uchumi. Hisia za kodi kuwa kubwa tena kwenye bidhaa muhimu ni dhahiri.

Kwenye uchumi, kuna kitu tunakiita 'Equillibrium Price' - yaani ile bei ambayo mnunuzi na muuzaji wataafikiana. Sasa kuna baadhi ya bidhaa ambazo kulingana na kupanda kwa bei, imesababisha 'price equillibrium' imepotea kabisa.

Maana yake ni kwamba bei mpya baada ya kodi na tozo, imesababisha wanunuzi kutokuhisi uhalali wa kununua kwa bei mpya. Mfano mdogo tu, mimi nilikuwa namiliki line mbili za simu, ila tangu tarehe moja, ni kama line moja nimeitelekeza na sijafanya muamala wowote wa kutuma wala kutoa pesa kwa wakala, kwasababu, akili yangu inaniambia hii bei ya sasa ni kubwa mno kulinganisha na huduma ninayopata.

Matokeo yake ni nini sasa?
Muitikio ukiwa mdogo kwa walaji, itakuwa ngumu sana kwa Mwigulu kuweza kukusanya kiasi ambacho amakitegemea. Kumbuka serikali ime target zaidi ya Tzs 1.5 Trillioni itoke kwenye miamala ya simu na tozo.

Sasa kwa upepo ulivo, sidhani kama hata nusu ya hii itapatikana. So maana yake, bajeti ya Mwigulu mpaka sasa ina shimo la karibu zaidi ya Tzs 1 Trillioni ambayo ili liweze kujazwa, itabidi serikali ikope, maana kumbuka kuna miradi ya SGR na Bwawa la umeme bado inahitaji pesa.

Ni kama kusema, tayari nakisi ya bejeti yetu tayari ipo kubwa zaidi ya walivoitabiri, kwasababu kuna kodi na tozo hazitaweza kukusanywa kama hii ya miamala ya simu.

Ama kwa kweli Mwigulu amefeli sana, tena sana.. Anasema eti hizi tozo zitatumika kuunda mfuko wa kizalendo, ila ni uwongo kwa sababu huwezi kuwa na mfuko wa kizalendo wakati bajeti yako siku zote ipo kwenye nakisi.

Ni kama kusema eti mtu uweke akiba ya mtoto kwenda shule wakati unadaiwa kodi ya nyumba.. Ni kitu hakiwezekani ni kuwadanganya tu watu, maana ameshabugi.

Kama inawezekana kurudia bajeti, nashauri Mwigulu afanye hivo mapema, la sivo.. naona deni la taifa likiendelea kupaa just kwa mtu kushindwa kufanya kazi yake vema.
T moja itafikiwa vizuri tuu,impacts ya kukwepa sio kubwa,wiki hii yote Niko nafanya miamala na nikienda kwenye vibanda watu wamejaa sema hisia zako tuu.

Ni hivi ni rahisi kukwepa hii kodi kama uko ndani ya eneo unaloweza tumia njia mbadala kukwepa gharama lakini ukiwa mbali no way out lazima utumie na njia rahisi ni mitandao ya simu kuliko mabenki na bahati mbaya au nzuri WaTzn wengi hawana utamaduni wa kutumia mabenki,wanadhani mabenki ni kwa wenye nazo.
 
Mnaongea kwa hisia zenu,wengi humu mumenunua bando ambapo tayari mushalipa kodi,huko mitaani kwenu mumekuta vibanda vya mawakala hivifanyi Kazi?

Sema hivi mna wish hivyo ila haitatokea
 
Deni la Taifa safari hii litafika mawinguni ukizingati wanatakiwa kununua chanjo mpya kwa kila wimbi jipya la korona

Fikiria kwa sasa tuko wimbi la 3 la korona mpaka kufika wimbi la 1000 watakuwa wamemalizia pesa kwenye barakoa(matambala),chanjo O²

Tuseme tu ukweli kwa sasa serikali haina kitu kabisa nadhani itafikia hatua waanze kuuza mabomu ya machozi na yale magari ya maji ya washawasha I'll angalau walipe elfu mbili 2 kwa walimu & manesi
 
Mwigulu hakuwa smart hata kidogo kwanini hakuirekebisha kutoa hayo mapungufu hapo wangeongeza hata jero tusingeshutka na Kodi ingekuwa nyingi kuliko Sasa watu tumegoma acha tu akakope huko nje kufidia. I think Sasa waziri wa mipango wamweke hata mango mwenye genge ni mzoefu kuliko hawa wasomi madesa Hadi PhD huku practibility Yao kwenye field ni zero experience kabisa. Dah Mwigulu kaniangusha Sana aisee, Mimi sio mchumi ila kwa akili ya kuvukia barabara najua something was wrong kwenye hyo budget na ukichangia Sasa tuna bunge la kinyumbu na watu wasio fikiria basi ni hasara kwa taifa
Kabisa mkuu.. hawa watu wanajiita Phd wanatia aibu sana
 
Back
Top Bottom