Madhara ya kula nyama ya Nguruwe/Kitimoto kwa afya yako...

Madhara ya kula nyama ya Nguruwe/Kitimoto kwa afya yako...

Nguruwe ambapo katika mwili wake hukusanyika jumla ya vijiumbe maradhi visivyoondoka kwa kuoshwa
Mdomo ni maficho ya vijidudu, bakteria na virusi vinavyokwenda kwa binadamu na wanyama.
Baadhi yake vinamhusu nguruwe, mfano wa kidudu kiitwacho Trchinella, nywelenywele ziitwazo Balantidium Dysentery, wadudu wa tumbo (Taenia Solium) na mchango wa nguruwe (Spiralis). Baadhi yake huingizwa kwenye maradhi mengi ya pamoja baina ya binadamu ( Cysticercosis & Influenza) na wanyama.

Minyoo (Ascaris na Fasciolopsis Buski) hupatikana kwa wingi nchini China.

Maradhi ya Balantidiasis hupatikana kwa wachunga nguruwe na wenye kuchanganyika nao, na yanaweza kuenea kwa sura ya mlipuko kama ilivyotokea katika moja ya visiwa vya bahari ya Pacific baada ya kimbunga. Maradhi yanakuwepo panapokuwepo nguruwe katika nchi zilizoendelea kiviwanda kinyume na madai ya uwezekano wa kuushinda uchafu wake kwa kutumia teknolojia mpya zinazoharamisha kula nyama bila ya kibali, hasa nchini Ujerumani, Ufaransa, Philippines na Venezuela.
Kwa kula minofu ya nyama ya nguruwe, (Trichinellosis) hupatwa na ugonjwa wa Balantidium Dysentery. Kwani mke hubungua kuta za matumbo kwa ajili ya kuweka mayai ambayo yanafikia kiasi cha 10,000. Mayai hayo huingia kwenye misuli kupitia damu na kugeuka kuwa ni vijiyai vyenye kuambukiza.
Ama kupata maradhi kupitia mchango wa nguruwe, ni kuwa hiyo hupatikana baada ya kula minofu ya nguruwe mwenye ugonjwa.

Minyoo hukua kwenye mchango wa binadamu na urefu wake unaweza kufikia meta saba, na unakuwa na kichwa chenye miba inayosababisha kukwaruzika kwa kuta za michango na mchupo mkubwa wa damu, na ana mirija minne na shingo. Aina za mke huzaliwa kama kwamba ni wanyama pekee na hufikia maelfu. Na katika kila mmoja kati ya mnyama, huzaliwa zaidi ya mayai elfu moja iwapo utakula Cysticercosis.

Kupatwa na ugonjwa wa minyoo ya tumbo la binadamu, hutokana na kula chakula kilichoingia mayai na kutoa lava, na huingia katika damu kupitia kiungo chochote. Na hatari yake hukisiwa kwa mujibu wa umuhimu wake.
Maradhi haya hayatokei kabisa kutokana na kupatwa na mchango usio na miba katika kichwa na wenye madhara madogo
kabisa Taenia Saginata ya ng’ombe.

KIIMANI
kwa upande wa Quran
"Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).

KWA UPANDE WA BIBILIA
“Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao” wala msiguse mizoga yao (Walawi 11: 7 – 8).

Nakubaliana na wewe kiafya na kiimani Nguruwe hafai kabisa ni Uroho na urafi wawanadamu ndo unawafanya kuvagaa na visivyo halali! Mkuu nikuombe Pia uzungumzie mara ingine ulaji wa samaki na viumbe wa majini na pia wanyama wa nchi kavu kiimani na kiafya! Maana Ulaji wa pweza na makaa na Ngiri na viboko nautilia Mashaka!
 
kama huli kitimoto ni bora pia usile na nyama nyingine pia kama kuku, n'gombe, mbuzi au kondoo coz nao wanabeba magonjwa mengi tu.

so kutokula nyama moja wakati nyingine unafakamia ni unafiki tu.

halafu, ume-assume kama huyo kitimoto tunamla akiwa mbichi. kwa jinc ninavyojua, kitimoto huwa kinapikwa muda mrefu sana. kwanza kinachemshwa, then kukaangwa and kama ni rosti wanakiunga fresh.

so najiuliza hayo ma-pathogens yanaweza kusurvive kweli kwenye moto wa muda mrefu kama huo.

kitimoto ni tamu acheni kabisa babangu........

aaaafffuuuu mbuzi si ndo anasababisha gauti...??? Huwasikii wakisema lolote.....
 
Kusema jambo bila kujua ni ujinga sana

Nyie hamjui hata maandiko yanasema nini
1 Timotheo 4:1-5

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Kama hujui jambo ni bora ukauliza!!!!!!!!!!!

Endeleeni kufuata mafundisho ya mashetani!
 
Ngoja nimalizie kula hii kitimoto yangu hapa,nikimaliza ndio nije hapa kuisoma vizuri hii thread,
 
Kusema jambo bila kujua ni ujinga sana

Nyie hamjui hata maandiko yanasema nini
1 Timotheo 4:1-5

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Kama hujui jambo ni bora ukauliza!!!!!!!!!!!

Endeleeni kufuata mafundisho ya mashetani!
Ikiwa hivyo ndivyo basi kitabu chenu (Bible) kitakua kina tombesha maneno (kinaji kanganya) Maana kinaanza kukataza Nguruwe asiliwe, Kisha kina ruhusu kila mnyama naaliwe tu. Ndio maana Waislam tuna mashaka na hiyo dini yenu.
 
Ikiwa hivyo ndivyo basi
kitabu chenu (Bible) kitakua kina tombesha maneno (kinaji kanganya)
Maana kinaanza kukataza Nguruwe asiliwe, Kisha kina ruhusu kila mnyama
naaliwe tu. Ndio maana Waislam tuna mashaka na hiyo dini yenu.

mkuu hiyo lugha uliyotumia sidhani kama ni kiswahili fasaha, utakula ban bure tukumisi jukwaa letu lile.
Achana na kitimoto ndgu, tanu balaaa!
 
Ikiwa hivyo ndivyo basi kitabu chenu (Bible) kitakua kina tombesha maneno (kinaji kanganya) Maana kinaanza kukataza Nguruwe asiliwe, Kisha kina ruhusu kila mnyama naaliwe tu. Ndio maana Waislam tuna mashaka na hiyo dini yenu.

Hapo mi naimani ndugu yangu umeteleza ulimi kidogo kusema biblia ime....... maneno!
Lkn ni kweli kabisa. Upande mmoja Yesu anawakataza viti moto. Pombe, uliberali Mungu hana mtoto n.k!

Upande wa pili kuna PAULO nawruhusu vyoote hivyo na ni mtu wa kwanza kumpa cheo cha uungu yesu! Na kusema Mungu ana watoto!
Ndio maana wafuasi wa Yesu walikuwa wanaitwa wayahudi na hawa wanaitwa WAKRISTO!
 
Mtoa mada mbona umeruka Ngamia hiyo hiyo walawi 11:4... Unasemaje hahahahah
 
Kaaa ukijua hilo ni Agano LA kale...Paulo aliidhinisha vyote
 
Kusema jambo bila kujua ni ujinga sana

Nyie hamjui hata maandiko yanasema nini
1 Timotheo 4:1-5

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Kama hujui jambo ni bora ukauliza!!!!!!!!!!!

Endeleeni kufuata mafundisho ya mashetani!

Nina swali kwako mkuu! Huu walaka wa Paul kwa Timothy ulikua na maana gani na kwanini Paul aliandika hivo? Tukishajua nini kilijiri wakati ule mpaks Paul akaandika hivo basi uhalali wa kula vyakula tu kama ulivoyaandika hayo mafungu haupo!
 
Kusema jambo bila kujua ni ujinga sana

Nyie hamjui hata maandiko yanasema nini
1 Timotheo 4:1-5

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Kama hujui jambo ni bora ukauliza!!!!!!!!!!!

Endeleeni kufuata mafundisho ya mashetani!

Hayo mafundisho ya mashetani ni yepi?
 
Haujaambiwa uache kula, ila ujue ina madhara (kama yalivyo orodheshwa hapojuu) pia kama wewe ni mfuasi wa vitabu hivi Qur-an na Bible jua una fanya makosa kumla Nguruwe kwani vitabu vivyo vime kataza kumla mnyama huyo.
Biblia haijakataza kula "mbuzi mtakatifu" bana.

Imesema alaye asimdharau asiyekula na asiyekula asimdharau alaye, kwani "CHAKULA NI KWA TUMBO, NA TUMBO NI KWA AJILI YA MWILI NA VYOTE BWANA ATAVITOWESHA"

Pia imesema kila kimuingiacho mtu hakimtii mtu unajisi ila kimtokacho, kwa maana kila kiingiacho hupita katika mwili na mwisho husihia katika choo lakini humo(moyoni) ndimo kuliko na unajisi haswaa, maana huko kuna husuda, na uzinzi, na uchoyo na fitina na takataka zoote...
 
Back
Top Bottom