Bila shaka ipo tofauti. Natamani tungepata food scientist hapa akatueleza vizuri. Chakula lishe (nadhani inajumuisha na food additives), lakini kwenye kwenye lugha sahihi, wanaita food supplements....hii ni kutokana na kuwa wakati mwingine, kutokana na aida fulani ya vyakula ama life style yetu, vyakula vinapungukiwa na aida fulani ya virutubisho kwenye mwili, na hivyo kuhitaji kufanyiwa food fortification. Hii iko zaidi kwenye unga wa sembe na pengine vingine pia
Sasa ukiongelea viini tete (geni zilizofanyiwa uhandisi), hizi ni kuwa tangu kupandwa ni tayari mbegu husika (ambayo genes zake zimefanyiwa uhandisi. Wakati tunajua wanyama huwa na DNA na mimea RNA, wakati mbegu inapofanyiwa uhandisi wa kigeni, unaweza kuchanganya toka mmea na mnyama, lakini wenye sifa fulani (characteristics/quality) ukaingiza kwenye nyingine ukapata nyingine. Usishangae kwenye GMos, mtu anachanganya genes za panya na mwembe ili apate mmea mwingine tofauti kabisa. Katika hali ya kawaida, haya mambo hayawezi kutokea. Sasa nadhani hao TFDA wao wana mashaka kuhusu food additives/supplements. Mfano, kuna bidhaa nyingi zinaandikwa 50+kwa wanawake na pia kwa wanaume. Labda hizondo zinaweza kuwa zinapigwa marufuku.Mfano ukisikia kuhusu hormone za testosterone unaambiwa inavyopungua kwa wanaume kadri umri unavyoongezeka na kupunguza uwezo wa tendo la ndoa kwa wanaume. Badala ya kutumia viagra, watu wanaweka utaratibu wa kumeza vidonge hivyo vyenye virutubisho hivyo (nadhani vinaweza kuchochea homes husika kuzaliana kwa wingi) na hivyo kuongeza uwezo wa tendo lenyewe. Ni mawazo mimi sio mtaalam