Elections 2010 Madhara ya kutokumtambua Rais

Elections 2010 Madhara ya kutokumtambua Rais

Wabunge wa CHADEMA hawatakiwi kuudhuria wakati JK anahutubia, utamsikilizaje mtu ambaye humtambui? Mimi mwenyewe simtambui kwa hiyo hata hotuba zake za TV na redio nimeshaamua sitazisikiliza au kuangalia. Huo ndo mgomo tunaoutaka otherwise it could be construed to be a double standard.
 
NA Huyu NAE KAIBUKIA WAPI NA MAGWANDA YA MAFISADI?
 
Swali kwa wanasheria:
Zaidi ya kutoka nje anapoongea JK bungeni, je utaratibu na sheria ya Bunge inaruhusu wabunge kumzomea mwongeaji? Kwani kama tunafuata utaratibu sheria na kanuni za bunge la Uingereza hiyo nayo ni option!
Yaani wabunge wa Chadema wakimzomea JK itakuwa ni tukio la maana kuliko kutoka nje :smile-big:
 
people nahitaji maelekezo zaidi. hivi si Dr. slaa alisaini matokeo ya urais au?
na je kama alisaini si maanaka alikubali?? na kama alikubali then why the change now au hakujua kama hawa mabandidu walishaiba kura???
naomba msaada hapa!!!:doh:
 
Slaa hakusaini matokeo mzee Kamonga, hivyo maswali yako yaaoypfuata yamekuwa redundant! natumaini wansheria wa chadema walisha chakatua jambo hili kisheria, pamoja na busara za wazee wazoefu wa chama kama kina E. Mtei aliyetofutiana wazi na mwalimu. Kutokutambua matokeo, kutomtambua raisi, kutokutambua waziri atakayeteuliwa na raisi.... halafu kuingia bungenu kupigana mm napata wasiwasi kidogo na mfumo wetu utakavyofanya kazi ipasavyo kama tutaaamua kuboycot kwa namna hii. wenzetu CUF zanz waligomea mpaka marupurupu ya wabunge hata vikao hawakuudhuruakwa sababu walikuw jasiri. sina uhakika na upande wa bunge la muungano.
mm binafsi siungi mkono jinsi uchaguzi ulivyo fanyika, at the same time nataka nipambane... sasa hapa kwa kweli tunapswa kuply wise and smart!!!
 
people nahitaji maelekezo zaidi. hivi si Dr. slaa alisaini matokeo ya urais au?
na je kama alisaini si maanaka alikubali?? na kama alikubali then why the change now au hakujua kama hawa mabandidu walishaiba kura???
naomba msaada hapa!!!:doh:

kwa mujibu wa sheria,tume ya uchaguzi itatangaza matokeo either yasainiwe or yasisainiwe,kwa hiyo dr slaa hakusaini yale mtokeo lakini tume wakatangaza tu yale matokeo kwa kuwa sheria inawaruhusu.
 
Ungekatta kumpisha barabarani wangekushukia walinzi wake na kukufanya kitu mbaya. lakini message ingekuwa sent kwa wale wanaoelewa madhumuni ya kufanya hivyo. Ujumbe mzito na wa uhakika wa jinsi sisi CHADEMA tulivyokerwa na process yote ya uchaguzi, utafikishwa kwa JK na mafisadi wenzake pale wapinzani wote wanaoamini kuwa JK hakushinda kwa haki, watakapotoka nje wakati Jk akianza kuhutubia bunge. Mimi nitafurahi sana wakitoka nje wacheze draft na karata mpaka amalize kughutubia! Hapo message itakuwa sent!
 
Kitu ambacho nasubiri nione ni je kama wabunge wa Chadema watatoka nje ya bunge pindi Kikwete atakapokuwa anahutubia

Nimesoma kwenye gazeti kama sio tzdaima ni mwananchi wamesema hawata toka
 
Kitu ambacho nasubiri nione ni je kama wabunge wa Chadema watatoka nje ya bunge pindi Kikwete atakapokuwa anahutubia

Mwenyekiti wa CHADEMA amesema wabunge watakuwepo kwenye hotuba ya Kikwete. Hata mie sitaji kuwa ni rais.
 
End justify the means, Mkwere ana thibitisha usemi wanamna hii kwa katiba ya jamhuri.Mtaniwia radhi wana jamvi marana hii ni mara yangu ya tatu nina andika kitu hikihiki nadhani na weza kuruka kichaa kama imanini yangu ita kuwa tofauti

CDM please nategemea yafuatayo kabla ya 2015

1.Mabadiliko ya katiba ya nchi
2.Tume ya uchaguzi huru
3.UWT kuvunjwa na kuundwa upya
4TAKUKURU kuvunjwa na kuundwa chombo kingine
Nisaidieni ndoto yangu ikamilike
 
Nimeshangaa hata makinda aliporuhusu kiushabiki maswali kwa akonay yanayohusu matukio ya nje ya bunge ya kumtambua au kutomtambua jk kama rais . Wangesubiri waone kama wabunge wa chadema watatoka nje ya jengo jk atakapoonyesha mwelekeo wa kuwahutubia wabunge.
Ninabashiri slaa hatakuwepo vivyo hivyo nitafurahi kuona wabunge wa chadema kutoka nje. Litakuwa fundisho ili juhudi za kuweka utaratibu mpya wa uchaguzi zianzishwe. Na kisaikolojia itamuumiza jk kwani ulimwengu utajua kwa mara ya kwanza kwa ile tz waliyoizoea na kila aendako watamtazama kwa jicho la dharau kama vile mwanaume aliyekimbia kutiwa jando
 
Kwa sheria zenu watatoka lakini kwa sheria ya jamuhuri ya muungano wa tz, hawatatoka maana wameshaapa, tutumie sheria kuongea na sio kuongea ongea bila kujua sheria inasemaje,
 
Leo nimesoma gazeti la mwananchi,ambapo inasemekana Wabunge wa CHADEMA wameamua kuendelea kukaa bungeni wakati rais atakapokua anahutubia bunge!!mimi binafsi sikubaliani nao,ningependa watoke bungeni wakati rais atakapokua anahutubia!!

Tukumbuke pia kuna kanuni za bunge, na najua vijana wetu ni waelewa, wasije wakafanya kitu kitakachowapa ccm nafasi ya kusema na kuwapaka matope. Mimi napendekeza wakae tu humo ndani, lakini ni marufuku kupiga makofi kwa chochote atakachokisema.
 
Mimi siwatambui Wabunge wote maana wamechaguliwa na katiba iliyochakachuliwa na kutangazwa na NEC iliyochakachuliwa..2015 Watakwenda kwenye uchaguzi na baada ya uchaguzi watalalama kama kawaida yao.Hivi hatuwezi kulalamika kabla ya Uchaguzi?Kwanini tunakwenda kushiriki uchaguzi wakati tunajua nkuna mapungufu? OYAAAAAA MIMI SIWATAMBUI WOTEEEEEEEEE
 
Mimi siamini kabisa katika huo mpango wa kumkimbia mdhulumu wao. kutoka nje maanake umkwepa m babe wako. kutoka nje ni ishara ya woga. JK atatanga baraza lake la mawaziri kuunda serikali, inamaana serikali dhalimu ikiwa bungeni basi wasusie bunge kwa ujumla wake? Physchological battle haiendi hivyo. CHADEMA wanatakiwa wafanye kile walichomfanyia PINDA, wakati wao wanashangilia CHADEMA piga kimya, kwenye kura mnamkataa. ile kitu imemuuma sana Pinda. maana anaelewa kwanini imekuwa hivyo. hawakumkataa Pinda kama Pinda bali wamkataa kama ishara ya kuikataa serikali dhalimu.

Hakuna kususia vikao vya bunge hata akija nani bungeni. cha kukataa ni kile atakachokileta huyo asiekubalika.

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani wanatakiwa kuisikiliza kwa makini hiyo hotuba ya JK ana kutumia fursa ya wakati wa kuijibu fungua madukuduku yao yaliowakaa moyoni kuhusu uhalali wa JK na NEC yake.

CHADEMA lazima watumie vizuri zana chache walizo nao. hivi sasa wana zana kuu tatu:
1. Uongozi wa upinzani Bungeni. 2. Wabunge imara 3. Wananchi.

Iwapo watatumia hizo zana tatu kwa ustaha hakika watawafanya baya CCM A na B pamoja na serikali yao.

CHADEMA Mungu kawajalieni top management team zaidi 90% yote ipo bungeni tutawashangaa kama mkituangusha
 
Ungejaribu kukataa kumpisha then uone mkono wa dola la Jei kei... naona ungefia segerea

Ila hata mimi ningeafiki chadema wangesusia speech kwa kuwa hawamtambui rais, ila ninachohisi watabaki bungeni ila hawatasupport hotuba yake, kama walivyouchuna jana kwa Pinda
 
Madhara yapo sana hasa kwa JK mwenyewe ndo maana hata wabunge wa CHADEMA walioko Dodoma wanatakiwa kutoka nje ya ukumbi wa bunge mara JK atakapoanza kuhutubia..tena ikiwezekana wachukue draft na karata wawe wanacheza kabisa muda wote wa hotuba yake..akimaliza basi warudi ndani au waende zao chako ni chako kula kuku..Hiyo itatuma salamu very clear kuwa JK hupendwi na umeiba kura kuwa rais

Hapa ndipo ninapoona immaturity ya Wana-CHADEMA!!!!! I hope wanachokipinga wao ni utaratibu mbovu wa NEC ambao wanahisi umeipendelea CCM!!! So the question come; huo uchaguzi wa wabunge ambao wana-CHADEMA ni kama wanaukubali umesimamiwa na nani? Kitimoto, haramu nyama yake lakini mchuzi si haramu?!
 
Madhara yapo sana hasa kwa JK mwenyewe ndo maana hata wabunge wa CHADEMA walioko Dodoma wanatakiwa kutoka nje ya ukumbi wa bunge mara JK atakapoanza kuhutubia..tena ikiwezekana wachukue draft na karata wawe wanacheza kabisa muda wote wa hotuba yake..akimaliza basi warudi ndani au waende zao chako ni chako kula kuku..Hiyo itatuma salamu very clear kuwa JK hupendwi na umeiba kura kuwa rais

Madhara yapo
1. Rais ataathirika kisaikolojia kwa hisia kwamba amebaka na kuingia ikulu kwa nguvu. Kwa muda mwingi atakuwa na ile guilt conscious. Na hii ni kawaida ya binadamu watu wanapokwita mwizi kwa sababu waliona umeiba na wewe ukasema hapana huku ukiujua ukweli umeiba roho lazima itakuuma na huenda kuna siku ukamrudia Mungu.
2. Ujumbe wa kutotambuliwa utaenea sehemu mbalimbali duniani na hivyo na kuwapa watu wa mataifa mbalimbali kuhoji nafasi ya democrasia nchini na kumpa changamoto rais kushughulikia mambo yanalalamikiwa ikiwemo kuunda tume huru
 
Back
Top Bottom