Madhara ya kwenda kutafuta utajiri kwa waganga

Madhara ya kwenda kutafuta utajiri kwa waganga

Red black

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2019
Posts
18,719
Reaction score
60,636
Niaje wakuu,

haya ni baadhi ya madhara utakayopata ukienda kutafuta utajiri kwa mganga.

Utapeli wa kifedha; Waganga wengi feki hutumia saikolojia ya hofu na tamaa kuwaibia watu kiasi kikubwa cha fedha kwa kisingizio cha "kusafisha nyota" au "kununua vifaa vya mizimu,sadaka

Masharti magumu na ya kikatili; Baadhi ya taratibu hujumuisha vitendo vinavyovunja sheria na maadili, kama vile kudai kafara za watu, viungo vya binadamu,ufirauni au kufanya mambo yanayodhalilisha utu.

Mifarakano ya kifamilia; Mara nyingi waganga huwataja ndugu au marafiki kuwa ndio wanaozuia mafanikio ya mtu, jambo linalosababisha chuki na utengano.

Athari za kisaikolojia: Watu walioingia kwenye harakati hizi mara nyingi huishi kwa hofu kubwa, msongo wa mawazo, na hatia, hasa pale mambo yanaposhindikana au masharti yanapokuwa mazito.

Cc Mshana Jr any additional point
 
Hivi utajali wa kufuga nyoka ni kua unamfuga tu ndani chumba cha pekee ake au kuna mengine
 
Utajiri wa short cut ni janga kuu, just imagine unakuwa tajiri mkubwa but huruhusiwi kulala chumbani kwako inakubidi ukalale chooni, au unakuwa tajiri mkubwa lakini huruhusiwi kuvaa nguo nzuri na safi au huruhusiwi hata kula vizuri, just imagine hata kula kitimoto rosti uruhusiwi, inakubidi ule ugali tembele mpaka ufe
 
Ujinga sana
 
Aaaa wapi! Inategemea. Ukipewa masharti magumu unakataa. Pia inategemea huyo mganga mizimu yake siku hiyo imeamka inataka nini. Kuna ndagū zingine masharti yake ni ya kutimiza mara moja tu basi ukifaulu ndo imetoka hiyo....

Jamaa wa kwenye machimbo huku Katoro wanatanua tu na karibu kila mmoja ana lake jambo. Mimi siongei habari za kusimuliwa!
 
Aise
 
Back
Top Bottom