Madhara ya maji ya chumvi kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani

Madhara ya maji ya chumvi kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Wakuu,

Kuna kautafiti kadogo nafanya kuhusiana na matumizi ya maji ya kisima yenye chumvi kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani.

Ningependa kujua madhara, kama yapo ya maji hayo katika vipengele vifuatavyo:
1. Kunywa - yana athari zozote kiafya kwa mnywaji? Je, yakichemshwa?
2. Kupikia - yana athari zozote kwa mlaji?
3. Kufulia - yanaweza kuharibu nguo?
4. Kuogea - yana athari zozote za ngozi?

Naomba majibu yaendane na maswali niliyouliza hapo juu. Natanguliza shukrani.
 
Madhara ni mengi
 
Nashukuru. Unaweza ku-Share kile unachojua wewe kuhusu mada hii
Kwenye kunywa yana ladha mbaya, nisijue madhara yake huko mwilini, maji yasiyo ya chumvi yakitulia kwenye ndoo muda mrefu huweka utando unaoteleza hiyo ni tofauti na maji ya dodoma, ndoo hutengeneza ugumu wa magadi inayofanania kutu, kwahiyo hapo pata picha yakifika kwa tumbo inakuwaje!

Kupikia hayana tatizo kutegemeana na vyakula vingi huwa tunaweka chumvi
Kwa kutumia kufua ni yanapausha nguo balaa

Kwenye kuoga ukimaliza ni kukimbilia kujipakaa mafuta/lotion yenye glycerine kinyume na hapo ngozi inapauka hata kupasuka kabisa km umepakaa chokaa
 
Hata yakichemshwa hali ni hiyo hiyo tena chumvi inajichuja chini baada ya muda inabadilika rangi kama kutu
Hatari sana. Vilevile kuna kipindi nilikuwa mikoa ya kati nikagundua idadi ya kutosha ya wanawake wenye miguu minene, na hapa naongelea unene ule ambao si afya. Sijajua hili linahusiana na maji au ni issue nyingine au ni maumbile tu.
 
Back
Top Bottom