Madhara ya Ongezeko kubwa la joto kiafya na namna ya kuyakabili

Madhara ya Ongezeko kubwa la joto kiafya na namna ya kuyakabili

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mwili wa binadamu huhifadhi joto lake kwenye wastani wa nyuzijoto 37. Mabadiliko madogo yasiyozidi nyuzijoto 1 yanaweza kutokea muda wowote wa siku kutokana na athari mbalimbali za kimwili na kimazingira.

Katika msimu huu ambao baadhi ya maeneo mengi ya nchi hayapati mvua za kutosha, baadhi ya watu wanaweza kuathirika na ongezeko la joto hivyo kuadhuru afya zao.

Kadri joto la kimazingira linavyozidi kupanda, ndivyo mwili pia huongeza joto lake ili kukabiliana nalo. Ili kuhakikisha usawa huu unatokea, mwili huongeza msukumo wa damu kuelekea kwenye ngozi ili joto husika lidhibitiwe kupitia utoaji wa jasho.

Hata hivyo, katika hali fulani, kasi ya mwili kwenye kuongeza joto inaweza kuizidi ile ya utoaji wa joto hivyo kuufanya mwili upatwe na changamoto mbalimbali za kiafya baadhi yake ikiwa ni-
  • Kiharusi cha joto (heat stroke)
  • Maumivu makali ya kichwa
  • Kizunguzungu na kuweweseka
  • Kiu kali isiyoisha
  • Kuzimia, Degedege na kifafa
  • Kupoteza ufahamu
  • Mwili kuishiwa maji
  • Kukauka na kusinyaa kwa ngozi
  • Uchovu mkubwa
  • Wekundu wa ngozi
  • Uvimbe joto kwenye maungio ya mwili
  • Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
  • Shinikizo dogo la damu
Madhara haya yanaweza kuonekana zaidi kwa watu wenye magonjwa sugu, wazee, watoto pamoja na wanawake wajawazito. Pia, watu wanaokunywa pombe na wale wanaofanya mazoezi mazito ya mwili wanaweza kuathirika na ongezeko kubwa la joto.

Mambo ya kufanya ili kuepuka (Kupunguza) madhara kiafya
  • Kunywa maji ya kutosha kila mara
  • Epuka unywaji wa pombe pamoja na vinywaji vingine vyenye caffeine (mfano kahawa, vinywaji baridi na energy drinks). Huufanya mwili upoteze kiasi kikubwa cha maji.
  • Epuka kufanya mazoezi mazito ya mwili kwa muda mrefu.
  • Kula mlo mdogo mara kwa mara (Epuka ulaji wa chakula kingi kwa wakati mmoja)
  • Vaa nguo nyepesi zisizo bana
  • Fungua madirisha ya nyumba, kaa kivulini pamoja na kuepuka kutembea juani kama siyo lazima
  • Usimuache mtoto, mwanamke mjamzito au mzee kwenye gari iliyofungwa vioo vyote.
Msaada wa haraka
Ikiwa mtu atapatwa na dalili zilizotajwa huko juu ambazo zinahusiana na madhara ya uwepo wa ongezeko kubwa la joto mwilini, mambo yafuatayo anapaswa kufanya kama sehemu ya huduma ya kwanza huku taratibu za kupelekwa hospitalini zikiendelea-
  • Ondoka sehemu yenye joto kali, kaa kivulini
  • Legeza tai na mkanda wa nguo kama umevaa, pia punguza wingi wa nguo ulizovaa ikiwemo viatu na sox
  • Mhusika alowanishwe (amwagiwe) maji ya baridi
  • Kichwa, uso, shingo na sehemu za kwapa zifanyiwe mgandamizo wa kitambaa kibichi, maji au barafu
  • Mhusika asilazimishwe kunywa maji, inaweza kuhatarisha zaidi uhai wake.
Chanzo: Web MD na Canadian Centre for Occupational Health and Safety
 
Back
Top Bottom