Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

soda kitu gani bhana..mbona watu wanaambiwa waache ngono zembe
kuna UKIMWI lakin bado wanapga kav kav...maisha mafupi, tafuta pesa..
kesho haina mwenyewe..
 
Leo nmetumiwa video ikionesha hatariii na madhara ya soda asee wakuu acheni kunywa soda, vinginevyo wakati unakunywa andaa na bajeti ya matibabu, nmeshindwa kui attach, mwenye nayo ataiweka,,,,

Ila wakuu soda mmmm basi

Hata kama umeshindwa ku attach basi unge eleza madhara yake na ungeweza sema soda gani au zote haya masuala ya ku post kitu ambacho hakina maelezo ueche kabisa sawa,uwe na maelezo ya kina kisha wafahamishe watu wengine,sasa hapo tuelewe vp?
Wewe mwenyewe unahisi umeeleweka?
 
Leo nmetumiwa video ikionesha hatariii na madhara ya soda asee wakuu acheni kunywa soda, vinginevyo wakati unakunywa andaa na bajeti ya matibabu, nmeshindwa kui attach, mwenye nayo ataiweka,,,,

Ila wakuu soda mmmm basi

Sasa unasema madhara yapo hutaji hata moja? Ni mpaka video tu? Sema hapa madhara yapi maana sio kila mtu ataona video.

Pili, kama umezaliwa Africa na unaishi Africa, labda uache kula kabisa, uache kunywa kabisa chochote na pia usitie dawa yoyote ukiugua. Maana kuna dawa itakuta imetoka Italy imeandikwa "for Africa". Utatokea wapi?

Secret societies have so many killing missions not easy to escape individually.
 
Leo nmetumiwa video ikionesha hatariii na madhara ya soda asee wakuu acheni kunywa soda, vinginevyo wakati unakunywa andaa na bajeti ya matibabu, nmeshindwa kui attach, mwenye nayo ataiweka,,,,

Ila wakuu soda mmmm basi

Kwani ulikuwa hujui?
 
mkuu hoja c ku consum ngap, hoja ni matumizi, nikupe mfano ukiambiwa kuwa chakula unacho kula n kitamu sana ila kimewekewa sum kidogo tu, je utaendelea kula??

Mkuu m nadhan anzia pale unapojua madhara yake, tafakari chukua hatua

kama suala ni matumizi na si kiwango...basi naamini hutumii vyote kati ya hivi..
  1. sukari
  2. chumvi
  3. mafuta
  4. maji ya kisima
  5. vyakula vya kusindika
  6. nyama/mayai ya kisasa/kuku wa kisasa
  7. hata baadhi ya mbogamboga na matunda
  8. MADAWA YA KISASA...
....je ni kweli hutumii hivi vyote???unafiki mbaya sema kweli...ukitaka kudadafuliwa kila point sema tu....SIKATAI SODA INA MADHARA LAKINI USEME NI KIWANGO GANI KATIKA CONSUMPTION....HATA PC/SIMU UNAYOTUMIA KUPOST JF INA MADHARA...JE UTAACHA KUITUMIA..???TAFAKARI CHUKUA HATUA..
 
.....usiogope...watu wanatisha badala ya kueleza kwa kina..inategemea unaconsume ngapi na kwa muda gani..na kiasi kipi ni hatari kwa afya..ukijua hayo utafahamu upo katika nafasi gani...

I drink lots when am not high
 
Lakini tuelewe kuwa kila chenye faida kina hasara zake.


ADVaNTAGES Vs DISsADVANTAGES



MIZAMBWA
INANUMA SANA!!!
 
..how much is lots and how often...?....to much of anything is harmful however...

It substitutes water. I wouldnt want my precious lil man to emulate such unhealthy habits.
 
Habari wana Jf, Naomba kushiriki madhara yatokanayo na unywaji wa soda.
Soda inakiwango cha sukari, Sukari yeyote ni hatari katika mfumo wa mwili, Wataalam wanathibitisha uwepo wa takribani vijiko 10 vya sukari katika kila chupa moja ya soda, kwa maana hiyo unapokunywa soda 5 kwa siku maanake unakula vijiko 50 vya sukari iliyo kwenye maji yaliyochanganywa na sukari (soda) pamoja na kemikali inayolinda soda isiharibike, kitaalam pia kwenye soda kuna kiwango kikubwa sana cha ACID (PH 2-3). Kiwango cha kemikali kilichopo ndani ya tumbo la binadamu kinadaiwa kuwa na Ph ya 3 ambayo huweza hata kusaga mfupa uliomezwa kwa bahati mbaya,Hivyo basi, kemikali iliyopo kwenye soda ni kali zaidi ya hata iliyopo tumboni mwa mwanadamu.

INSULINI kemikali iliyoundwa katika kongosho (pancrease). Husaidia kusawazisha kiwango cha sukari mwilini,Kongoshoina kazi ya kutengenza insulin na homoni zingine za kusaidia uyeyushaji wa chakula (Mmeng’enyo).

Ikumbukwe kwamba kiwango cha sukari mwilini huchujwa sehemu ya kongosho, kongosho linapofail kuchuja ndipo sukari huanza kupanda taratibu, kiasi kwamba mtu hupata kisukari na magonjwa mengine, kongosho inapofail hapo ndipo binadamu huanza kutapata, hapo ni sawa na dreva kuambiwa apunguze speed anakaidi akitegemea BREAK, na Break inapofail hapo ndipo CHANGAMOTO huanzia.

Yamkini huenda BIA ikawa ni bora zaidi kuriko kunywa soda hizi tunazokimbilia kila siku.

Dalili za kisukari

a. Kukojoa mara kwa mara

b. Kiu Isiyoisha:

c. Njaa Kali:


d. Kuongezeka kwa uzito (unene):

e. Kupungua uzito kusiko kawaida:

f. Uchovu wa mwili:

g. Hasira:

h. Kutoona vizuri:


i. Vidonda kutopona vizuri au haraka:

j. Magonjwa ya ngozi:


k. Kuwashwa kwa ngozi:

l. Kuwa na fizi nyekundu au zilizovimba:

m.Uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa:

n. Ganzi mikononi au miguuni:

Zifuatazo ni baadhi ya Athari za sukari ;

i.Sukari huweza kuathiri ukuaji wa homoni mwilini ( kitu ambacho ni muhimu kwa kumfanya mtu kuishi na afya njema wakati wote )

ii.Sukari ndiyo chakula cha saratani mwilini.

iii.Sukari huongeza lehemu ( cholesterol ) mwilini.

iv.Sukari huweza kusababisha kizunguzungu na kudhoofisha mwili kwa watoto.

v.Sukari huweza kudhoofisha nguvu ya macho

vi.Sukari huweza kuzuia utembeaji wa protini mwilini

vii.Sukari huweza kusababisha mzio wa chakula ( Food allergies )

viii.Sukari huchangia ugonjw a wa kisukari

ix.Sukari huweza kusababisha ugonjwa wa moyo.

x.Sukari huweza kuharibu, umbo la vinasaba vya mwili ( D.N.A )

xi.Sukari huweza kusababisha utukutu, utundu na kukosa umakini kwa watoto.

xii.Sukari huweza kuchangia kupunguza n kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yatokanayo na wadudu aina ya bacteria ( infectious diseases )


Hizo ni baadhi tu ya sababu karibu takribani 146. Je, kwa kujua sababu zote zilizo thibitishwa kuhusu madhara yatokanayo na sukari, kuna sababu gani ya kuendelea kupenda kutumia sukari jamani? Ingawa Hatuwezi kuiepuka sukari moja kwa moja kwani baadhi ya vyakula huwa havitamkwi moja kwa moja jina la kuwepo kwa sukari bali hutumia majina kama Glucose, fructose n.k Yakupasa wewe mwenyewe utokomeze ulaji wa sukari kwa kujiwekea mikakati yako, punguza matumizi ya soda, kuna watu wakipata kiu badala ya kunywa maji hukimbilia soda, Soda ni kinywaji hatari sana kuriko BIA, Hasara ya Bia ipo kwenye gharama na ulevi unaomfanya mtu asijitambue, Lakini madhara ya soda/sukari ni Makubwa sana.
unaweza punguza matumizi ya sukari kwenye chai, kwa kukamulia ndimu kwenye chai ukizoea ni taam sana.

pia kuepuka unywaji wa soda tujitahidi tunywe maji badala ya soda;
 
Asante jomba hapa nilitaka nikapate Pepsi bariidi ngoja ninywe maji taka toka tajiri mwenye timu na bot
 
Uzi mzuri, hata hivyo una mapungufu kidogo ya kiufundi. Unavosema soda ina madhara kuliko bia ulitakiwa ujenge hoja pande zote mbili lakini hujafanya ulinganifu wowote zaidi ya kuizungumzia soda pekee. Ulivesma soda moja ni sawa na vijiko kadhaa vya sukari ulitakiwa useme je bia moja kwa volume hiyohiyo ya soda ina vijikovingapi vya sukari??
Vilevile tukumbuke kuwa too much of a good thing is harmful. Chumvi pia ina madhara, ugali, wali, maji n.k. Cha msingi ni watu watumie kila kitu kwa uangalifu mkubwa.
 
Uzi mzuri, hata hivyo una mapungufu kidogo ya kiufundi. Unavosema soda ina madhara kuliko bia ulitakiwa ujenge hoja pande zote mbili lakini hujafanya ulinganifu wowote zaidi ya kuizungumzia soda pekee. Ulivesma soda moja ni sawa na vijiko kadhaa vya sukari ulitakiwa useme je bia moja kwa volume hiyohiyo ya soda ina vijikovingapi vya sukari??
Vilevile tukumbuke kuwa too much of a good thing is harmful. Chumvi pia ina madhara, ugali, wali, maji n.k. Cha msingi ni watu watumie kila kitu kwa uangalifu mkubwa.
sawa mkuu; ila nimefanya hivo kufupisha uzi, ingawa pia ucjali nitakuwekea updates, madhara yatokanayo na bia
 
Back
Top Bottom