Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Soda kwa mjamzito ina madhara gani mkuu.?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app

MADHARA YA SODA.jpg

Mkuu Soda kwa mtu wakawaida ina madhara makubwa itakuwa kwa mwanamke mja mzito?

Dr William Mtanzania Wa USA America

Washenzi ninyi wote
Mnaokunywa soda za Pepsi na Coca cola.
Wajinga wote mtakao soma ujumbe huu na kisha kuupuza, Ni nani kati yetu asiyependa vitu vitamu kama hizo soda.
Ila unajua kwenye chupa moja ya soda ya coca cola au Pepsi kuna zaidi ya vijiko 10 vya sukari yani unahesabu 1,2,3,4,5,6,7,8,9 hadi 10.
Kwa kawaida ukinywa vijiko 10 vya sukari ulistahili kutapika au kushikwa na kichefuchefu ila asante kwa phosphoric acid iliyomo kwenye soda hizo ule ukakasi wa radha ya sukari unapotea ndio maana hutapiki unakunywa kwa raha zako.
Baada ya dakika 40 sukari yote inazama kwenye mishipa ya damu yako, Asante Mungu kama ulikuwa na pressure ya kushuka madakitari watakwambia kunywa coca cola moja maana ndani ya hizo dakika 40 blood pressure yako itapanda juu.
Baada ya B.P kuwa juu mapigo ya moyo wako yataanza kubadilisha fomula ya utendaji kazi wake moja kwa moja utaanza kukaribisha ugonjwa moyo.
Asante Mungu kwenye mishipa yako tayari kuna cholesterol zimeanza kujitengeneza zinausongelea moyo bila kusahau kwa wiki ukiwa unaweza kunywa kati ya chupa mbili (2) za soda basi figo lako limeanza kutunga mafuta kwenye kuta zake.
Unywaji wa soda ni chanzo cha magonjwa ya " Moyo"
"kuziba kwa mishipa ya damu"
"Kupata cholesterol ambayo inaongeza kisukari
" Kuharibu mishipa ya moyo "
"Kutungisha mafuta kwenye figo na figo moja kulinunua ni zaidi ya $336,000"
"Kupandisha pressure kuwa juu ya damu"
"Hutanua mishipa ya damu"
"Husababisha kukosa usingizi hasa kutokana na caffeine iliyomo kwenye kinywaji cha coca cola"
"Ni chanzo cha kutoboka kwa meno na kungooka"
"Huzuia kupata choo"
"Saratani"
"Inachumbua tumbo =Vidonda vya tumbo"
 
Mm soda sizipendagi tu yaan inaweza pita hata miezi mitatu cjanywa soda.
 
Mimi nakunywa soda mwaka wa 47 huu na sijawahi pata tatizo lolote lile. Tusitishane maana wengine pombe hatunywi soda tamu baba ..yani niache kunywa soda wakati kufa nitakufa tu alaah..
Kula soda, kula bia maana ukishasepa huko mbele mbele hakuna tena soda wala bia.

Yani kwa ufupi kula maisha maana njia za kufa ziko karibu Million 16.
 
mi pepsi ndo itanimaliza nimeshakuwa teja wake! sijui naanzia wap kuweka uhasama na pepsi.
 
Uzi huu umenifanya nigundue kwamba unywaji wa bia ni afadhali kuliko unywaji wa soda kiafya!
 
Back
Top Bottom